16 Nov 2014

Radio japan  ni  moja  kati  ya  radio  kubwa  kabisa  duniani  na  ambayo  hurusha  matangazo  yake  kila  pande  ya  dunia. Radio  japan  idhaa  ya  Kiswahili  ni  sehemu  ndani  ya  radio  japan  ambayo  hurusha  matangazo  yake  kwa  lugha  ya  Kiswahili , idhaa  hii  ilianzishwa  mnamo  mwaka  1964.
Radio  japan  ni  radio  ambayo  ina  maajabu  makubwa, upekee  na  ubunifu  wa  hali  ya  juu. Yafuatayo  ni  maajabu  ambayo  nimeshuhudia  ndani  ya  radio  Japan :-
  
Kuendelea  na  kuenea  kwa  mitambo  ya  FM  na Satelaiti  ya  radio  Japan  kila  pande  ya  dunia, radio  japan  imefanikiwa  kwa  kiasi  kikubwa  sana  kuweza  kurusha  matangazo  yake  katika  nchi  mbalimbali  kwa  lugha  tofautitofauti   mfano  kifaransa  , kihindi , kithai, Kiswahili, kiindonasia,  kiarabu  na  nyingine  nyingi. Hivyo  basi  hili  ni  moja  kati  ya  maajabu  ya  radio  ya  Japan.
  
Maajabu  mengine  ni  jinsi  radio  japan  inavyofungamana  na  mitandao   ya  kijamii  katika  kurusha matangazo  yake, mfano  facebook  na  barua  pepe. Hii  ina  maana  kwamba  unaweza  kupata  matangazo  ya  mbalimbali  ya  radio  japan  kupitia  mitandao  ya  kijamii  mfano  kusikiliza  taarifa  ya  habari  pia  habari mbalimbali  ndani  ya  ukurasa  wa   barua  pepe. Hivyo  basi  haya  ni  moja  kati  ya  maajabu  ndani ya  radio  japan.
  
Mpangilio  mzuri  wa  ratiba  ya  vipindi  vya  radio  japan  idhaa  ya  Kiswahili, mfano  jumatatu 5,2014  malimba  ya kijapani , ijumaa mai 9,2014  karibu  japan  iliyostaajabisha  yanagawa, miji  wa  mifereji,mai 10,2014  utamaduni  mpya  wa  kijapani  kisambaza  filamu  mpya  za  kijapani, jumapili  mei  11, 2014  ukumbi  wa  jumapili. Hivyo  baadhi  ya  vipindi  na  ratiba  zake  kila  inapoisha  ratiba  moja  ndio  mwanzo  wa  ratiba  nyingine. Hivyo  basi  hili  ni  moja  ya  upekee  wa  radio  japan. 

Vipindi  motomoto na matangazo  ya  radio  Japani  mfano   jifunze  kijapan , darasa  la  kujifunza  kijapani  kwa  mtandao  kwa   Kiswahili   ni  kipindi  cha  dakika   10  kinachotangazwa  na  radio   ya  NHK  ya  dunia  kila  wiki,  katika  matangaazo  utapata  taarifa  ya   habari  idhaa  ya  Kiswahili.pia  taarifa  mbalimbali  ndani  ya  mabara  mbalimbali  mfano  Asia  na  duniani  kwa  ujumla. 

Matumizi  ya  njia  mbalimbali katika  urushaji  wake  matangazo , mfano  FM  kipitia  radio  washiriki, TBC  FM , RADIO  KWA NEEMA  FM   98.2 MHz (Mwanza)  pia  radio  mbalimbali  sehemu  kama  Bujumbula, Nairobi  na  maeneo  mbalimbali  duniani. pia  kwa  njia  ya  setelaiti  nayo  pia  hurusha  matangazo  yake  kwa  urahisi  kila  kona  ya  dunia. hivyo  basi  radio   japan  ina maajabu  makubwa  sana  ndani  ya  huu  ulimwengu. 

Ajabu  la mwisho  ambalo  sito  kuja  kulisahau  na  ambalo  limenifurahisha  sana   ni   juu  ya taarifa  ya  vyoo  vya  kisasa  vilivyogunduliwa  na  kuanza  kutumika  nchini  Japan. Hivi  ni  vyoo  vya  kisasa  kabisa  ambavyo  vimetengenezwa  nchini  Japan  na  vimeanza  kutumika  hii  ni  taarifa  ambayo  niliipata  kupitia  njiia  ya mtandao. Haya  ni  maendeleo makubwa  sana. 

Mwisho  radio  Japani  ni  ya  pekee  sana  kwa  sababu  hutoa  fursa  kwa  wadau  kutoa  maoni  juu  ya  maendeleo  na  maboresho  ndani  ya  radio  japani  mfano  radio  Japan  idhaa ya Kiswahili.hivyo  basi  radio  japan ni  radio  iliyojikamilisha  katika  kufanikisha  yale  waliyoyaadhimisha.
                                                                                               




















SHAIRI  KWA  AJILI  YA  SIKU  YA  JUMUIYA  SAUT –MWANZA

                            NOVEMBER  20, 2014


1.     kwanza  mungu  mtukufu ,ndio  nampa  heshima,
           kwa  huba  wake  wasifu ,mbele  yenu  kusimama,
           nina  mengi  masurufu ,yametoka  chawakama,
           leo  siku  jumuiya ,tulonge  na  Kiswahili.

2.     pili  niwape  salamu ,wote  mlo  udhuria,
           wanafunzi  na  walimu ,wajumbe  nawapungia,
          ninayo  mengi  matamu ,naitaji  wapatia,
          leo  siku  jumuiya ,tulonge  na  Kiswahili

3.     Tatu  wageni  walikwa  ,mabibi  pia  mabwana,
          Mikoa  mwanza  na  rukwa, na wale  wa  nyamagana,
          Nawashukuru  kufika ,tupeane  yenye  mana,
          leo  siku  jumuiya ,tulonge  na  Kiswahili.

4.     heshima  rasmi  mgeni  ,ahsanste  kuudhuria,
          kutoka  kwako  kazini ,hadi  hapa  kuingia,
          nina  machache  moyoni ,ningependa  kuongea,
          leo  siku  jumuiya ,tulonge  na  Kiswahili.

5.     paukwa  ninatamka  ,pakawa  muitikie,
          sitapenda  kupayuka ,radhi  nyote  mniwie,
          ila  kubwa  nalotaka ,ni  faida  yetu  sie,
          leo  siku  jumuiya ,tulonge  na  Kiswahili.

6.     SAUT  ndio  mlezi ,watupatia  malezi,
           Watupa  mengi  mapenzi ,kama  nazi  na  mkwezi,
           Au  kichwa  na  kinyozi ,jibu  mgonjwa  na  dozi,
           leo  siku  jumuiya ,tulonge  na  Kiswahili.

7.     uongozi  nausifu,  nausifu  tena  sana ,
          utii  uwadilifu ,leo  tena  kukutana  ,
          huu  ni  wetu  wasifu ,ni  mfano  kila  kona ,
          leo  siku  jumuiya ,tulonge  na  Kiswahili.

8.     ukumbuke  moja  jambo ,toka  enzi  za  mababu ,
          SAUT  toka  kitambo  ,watekereza  wajibu,
          Vijana  tufanye  mambo,mnayo  kila  sababu,
          leo  siku  jumuiya ,tulonge  na  Kiswahili.

9.     kila  alofanya  jema , yapasa  kumsifia,
          pongezi  baba  kitima ,heshima  twakuekea,
          ulo  yafanya  ni  mema ,SAUT  imetulia,
          leo  siku  jumuiya ,tulonge  na  Kiswahili.

10.                        Sasa  lako gurudumu ,heshima  baba  mkamwa,
          kuendeleza  elimu ,kazi  ya  mungu  kutumwa,
          mishahara  ya  walimu ,izidi  kuwa  muluwa,
          leo  siku  jumuiya ,tulonge  na  Kiswahili.

11.                        Tumejipanga  vizuri ,SAUT  kutumikia,
          Hii  ni  yetu  fahari ,popote  kusimulia,
          SAUT  mambo  mazuri, ,kuku  ,bata  twajilia,
          leo  siku  jumuiya  ,tulonge  na  Kiswahili.

12.                        Kwanza  mwanza  ni  upepo ,ziwani  na  zile kingo,
          Malimbe  hapa  tulipo ,tunafaidi  matango,
          Wadau  wengi  walipo ,luchelele  nyamalango
          Leo  siku  jumuiya ,tulonge  na  Kiswahili.

13.                        Sisi  watu  wa  ukweli ,malezi  bora  kwa  mama,
          Twakipenda  Kiswahili,tumetoka  chawakama,
          Tupo  nchi  mbalimbali ,chama  twakipa  heshima
          Leo  siku  jumuiya ,tulonge  na  Kiswahili.

14.                        Kiswahili  twakikuza  kwa  uwezo  wa  jalari
          Wazawa  acha  puuza ,hili  si  jambo  la  kheri,
          Wageni  wanajifunza  ,kwao  ni  kubwa  fahari,
          Urithi  wetu  pekee ,ni  lugha  ya  Kiswahili

15.                        Kasumba  ndio  kikwaza ,watu  wakiwa  membari,
          Juhudi  za  kudumaza , na  kufifisha  kandiri,
          Lugha  wanaipwekeza ,kunyima  yake  nambari,
          Urithi  wetu  pekee ,ni  lugha  ya  Kiswahili

16.                        Baba  kavoi  heshima,   ,na  mbilinyi  kadharika,
          Na  malenya  wetu  mama, nadharia  muafaka,
          Mama  zena  yu   salama , pongezi  baba  mashaka,
          Urithi  wetu  pekee ,ni  lugha  ya  Kiswahili

17.                        Na  wageni  mbalimbali  ,mlo  huko  mabandani,
          Mno  penda  Kiswahili  , chawakama  jiungeni,
          Mje  faidi  asali, tuwe  nanyi  shairini,
          Urithi  wetu  pekee ,ni  lugha  ya  Kiswahili

18.                        Peni  chini  nailaza ,kwa  heshima  si  kejeri,
          Lugha  kuiendeleza , duniani  ishamiri ,
          Na  wazawa  kuhimiza , kwa  msingi ,sekondari
          Urithi  wetu  pekee ,ni  lugha  ya  Kiswahili.

19.                        Naacha  kiti  na  meza , nazima  na  kibatari,
          Ni  usiku  wenye  kiza  ,kwa  lugha  ya  kishairi,
          Ni  mengi  nimewajuza ,majibu  nayasubiri,
          Urithi  wetu  pekee ,ni  lugha  ya  Kiswahili.


……………………….Mtila  b  mtillah………………………………
………….0689 358 544……………0657 965 867…………………..


























28 Jun 2014



                                                         

                   MAAJABU  YA  LUGHA  YA  KISWAHILI

          Lugha  ya  Kiswahili ni  lugha  ya  kibantu  yenye  asili  ya  mwambao  wa  pwani  ya  afrika  mashariki  yenye lahaja  mbalimbali na  ambayo  hutumiwa  na  watu  wengi  wa  afrika  mashariki na kati  mfano  Kenya ,Rwanda,Burundi,Congo na  hususani  Tanzania. Maajabu  ni  mambo  ya  kushangaza ,yasiyokuwa  ya  kawaida na  yenye  upekee  mkubwa  ukilinganisha  na  hali  ya  kawaida.


Maajabu  ya  lugha  ya  Kiswahili  ni upekee , hali  isiyokuwa  ya  kawaida ,ubunifu  na  umahili  ndani  ya  lugha  ya  Kiswahili  jinsi  inavyopendeza ,inavyovutia  na inavyotumika  ndani  ya  jamii  mbalimbali .Kuna  maajabu  mbalimbali  ndani  ya  lugha  ya  Kiswahili  lakini  yafuatayo ni maajabu  saba  ya  lugha  ya  Kiswahili :-
            Asili  ya  lugha  ya Kiswahili; lugha  ya  Kiswahili  asili  yake  ni  mwambao  wa  pwani  ya  afrika  mashariki  ambao  huhusisha  nchi  kama  Kenya  na  Tanzania .Asili  hii  ya  lugha  ya  Kiswahili  tunaweza  kusibitisha  kwa  sababu  mbalimbali  kwa  mfano  lahaja  nyingi  za  Kiswahili  zinapatikana  ndani  ya  afrika  mashariki, waongeaji  wazuri  wa  lugha  ya  Kiswahili  wanapatikana ndani  ya  afrika  mashariki na waandishi  wengi  wa  vitabu  vya  Kiswahili  bado  wanapatikana  ndani  ya  afrika  mashariki. Hivyo basi  hii  inathibitisha  kuwa  Kiswahili  kina maajabu  makubwa.
            Fasihi  ya  lugha  ya  lugha  ya  Kiswahili, fasihi ya  lugha  hii  ni  ya  pekee  sana  ukilinganisha  lugha  zingine  mfano katika  tanzu  kama  vile  Liwaya ,Tamthilia  na   Ushairi, kwa  kiasi  kikubwa  tanzu  hizi  zinaingiliana  na  kutofautana  mfana  tamthilia  ya  Nguzo  Mama  ya  Penina  Muhando  tunaona  anajaribu  kutumia  nyimbo  katika  kuisana  kazi  yake ambao  ni  kipera  cha  ushairi. Hivyo  basi  haya  ni  maajabu  ndani  ya  lugha  Kiswahili  katika  fasihi  ya  Kiswahili.
           Ukuaji  na  ueneaji  wa  lugha  ya  Kiswahili, hapa  tunaangalia  njia  mbalimbali  zinazotumika  kukuza  na  kueneza  lugha  hii  ya  Kiswahili  mfano  vyombo  vya  habari  kama  vile  Lungoya  (redio  japan  idhaa ya  Kiswahili) ,sauti  ya  amerika  kwa  lugha  ya  Kiswahili hii ni kwa  upande  wa  nje  ya  afrika  mashariki.pia  kuna  taasisi  pamoja  na  vyama  mbalimbali vinavyoshughulikia  na ukuzaji  na  uenezaji  wa  lugha  hii ndani  ya  afrika  mashariki  mfano  TUKI ,TAKILUKI ,CHAWAKAMA,BAKITA,UKUTA nakadhalika. Hivyo  basi  hii  inapelekea  idadi  ya  watumiaji  kuongezeka  na  kukifanya  Kiswahili  kuendelea  kuwa  na  maajabu  makubwa.
           Matumizi  ya  lugha  ya  Kiswahili  katika  muktadha  mbalimbali, mfano  elimu,siasa, uchumi, michezo,mikutano ,sherehe  na  mahubiri.kwa  kuanza  na  muktadha wa elimu Kiswahili  kimepandishwa  hadhi  mpaka  kufundishwa  ngazi  ya  chuo  kikuu, sekondari  kama somo  na  shule  za  msingi  kama  lugha  ya  kufundishia masomo  yote  isipokuwa  kiingereza tu ndani  ya  Tanzania pia  Kiswahili  kutumika  kwenye  mikutano  mikubwa  ndani  ya  afrika mfano  ya  jumuiya  wanachama  wa  afrika mashariki. hivyo  basi  hayo  ni  maajabu  makubwa  ndani  ya  lugha  hii.
           Uundaji  wa  msamiati  wa  lugha  ya  Kiswahili.  msamiati ni  maneno  yanayopatikana  katika  lugha  Fulani  hivyo  basi  msamiati  katika  lugha  ya  Kiswahili  ni maneno  yanayopatikana  ndani  ya  lugha  ya  Kiswahili. Lugha  hii  ina njia  nyingi  sana  zinazotumika  katika  kukuza  msamiati  wake  kama  vile  kutohoa  toka  lugha  za  kigeni, miambatano, kufananisha  umbo  sura  na  sauti, na  kubadilisha  mpangilio  wa  herufi.hizi  njia  zinazotumika  katika  kuundia  msamiati  wa  lugha  ya  Kiswahili.
           Utafutaji  na  upataji  wa  visawe  vipya  vya  lugha  ya  kiswahli. Visawe  ni  maneno  ndani  ya  lugha  mbalimbali  yanayofafanua kitu  au  jambo  moja  kwa  matamshi  ya  lugha  hizo. Katika  lugha  ya  Kiswahili  kuna  uhaba wa  visawe  vinavyotokana  na  maendeleo  ya  sayansi  na  teknolojia lakini  jitihada  zimefanyika  na  zinaendelea  kufanyika katika  kuhakikisha  visawe  vinapatikana  mfano  wa  visawe vipya ni  mnyange, nywila, kinuruweo, sasisha, talakilishi, talakilishi mpakato pamoja  na  kinyoni. Hivyo  basi  haya ni  maajabu  makubwa  sana yanayopatikana  ndani  ya  lugha  hii  ya  Kiswahili.
            Kasumba  na  uhaba  wa  wataalamu  wa  lugha  ya  Kiswahili. Kasumba  ni  hali  ya  kutothamini  kitu  chako  kwa  kung’ang’ania vitu  vya  kigeni.hili  ni  moja  ya  ajabu  katika  lugha  ya  Kiswahili  kwa   sababu  wazawa  wengi hususani  wasomi  wanakidharau  kiswahli japo  kuwa  ndio  lugha  yao  pia  licha  ya  kuwa  Kiswahili   asili   yake  ni  afrika  mashariki  ajabu  bado  kuna  uhaba  wa  wataalamu  wa  lugha  hii. Hivyo basi  hayo  yote  yanabaki  kama  maajabu  katika  mlongo  hasi.
         Hivyo basi  hayo  ndio  maaajabu  ya  lugha  ya  Kiswahili. Ili  kiswahili  kiweze  kuendelea  zaidi  na  zaidi  ni  lazima  elimu  itolewe  juu  ya  umuhimu  wa lugha  hii.pia  serikali  ni  lazima  itambue  kuwa  hii  ni  lasilimali hivyo  basi  ni  lazima iwekeze  vya  kutosha kwa  kushilikiana  na  vyombo  vyombo  vya  habari, wadau mbalimbali, mashirika  mbalimbali  , pamoja  na  taasisi na  vyama  mbalimbali  vya  kukuza  na  kuendelza  Kiswahili  ndani  na  nje   ya  nchi.




…>>>>>>>>>>>>>????MTILA BAHATI?????>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Powered by Blogger.

Wasiliana nami papo kwa papo

Name

Email *

Message *

Ads 468x60px

Breaking News

Top Featured

Featured Posts

Sample text

Sample Text

Recomended

Facebook

Advertise

Most Popular

Connect With Us

Followers

Social Icons

Pages

Pages

BTricks

Pages

Popular posts

Tafuta chochote ukiwa hapahapa

Kategori

Recent Comments

You can replace this text by going to "Layout" and then "Page Elements" section. Edit " About "

recent posts

Video Of Day

TRANSLATE

Instructions

Video

Flickr Images

FURAHIA UWEPO WAKO HAPA

Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

Imetembelewa mara

TAKWIMU ZA WATEMBELEAJI

Popular Posts

SAJIRI

Definition List

premium-wordpress-themes.org