Radio
japan ni moja
kati ya radio
kubwa kabisa duniani
na ambayo hurusha
matangazo yake kila
pande ya dunia. Radio
japan idhaa ya
Kiswahili ni sehemu
ndani ya radio
japan ambayo hurusha
matangazo yake kwa
lugha ya Kiswahili , idhaa hii
ilianzishwa mnamo mwaka
1964.
Radio japan
ni radio ambayo
ina maajabu makubwa, upekee na
ubunifu wa hali
ya juu. Yafuatayo ni
maajabu ambayo nimeshuhudia
ndani ya radio Japan :-
Kuendelea na kuenea kwa mitambo ya FM na Satelaiti ya radio Japan kila pande ya dunia, radio japan imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuweza kurusha matangazo yake katika nchi mbalimbali kwa lugha tofautitofauti mfano kifaransa , kihindi , kithai, Kiswahili, kiindonasia, kiarabu na nyingine nyingi. Hivyo basi hili ni moja kati ya maajabu ya radio ya Japan.
Kuendelea na kuenea kwa mitambo ya FM na Satelaiti ya radio Japan kila pande ya dunia, radio japan imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuweza kurusha matangazo yake katika nchi mbalimbali kwa lugha tofautitofauti mfano kifaransa , kihindi , kithai, Kiswahili, kiindonasia, kiarabu na nyingine nyingi. Hivyo basi hili ni moja kati ya maajabu ya radio ya Japan.
Maajabu mengine ni jinsi radio japan inavyofungamana na mitandao ya kijamii katika kurusha matangazo yake, mfano facebook na barua pepe. Hii ina maana kwamba unaweza kupata matangazo ya mbalimbali ya radio japan kupitia mitandao ya kijamii mfano kusikiliza taarifa ya habari pia habari mbalimbali ndani ya ukurasa wa barua pepe. Hivyo basi haya ni moja kati ya maajabu ndani ya radio japan.
Mpangilio mzuri wa ratiba ya vipindi vya radio japan idhaa ya Kiswahili, mfano jumatatu 5,2014 malimba ya kijapani , ijumaa mai 9,2014 karibu japan iliyostaajabisha yanagawa, miji wa mifereji,mai 10,2014 utamaduni mpya wa kijapani kisambaza filamu mpya za kijapani, jumapili mei 11, 2014 ukumbi wa jumapili. Hivyo baadhi ya vipindi na ratiba zake kila inapoisha ratiba moja ndio mwanzo wa ratiba nyingine. Hivyo basi hili ni moja ya upekee wa radio japan.
Vipindi motomoto na matangazo ya radio Japani mfano jifunze kijapan , darasa la kujifunza kijapani kwa mtandao kwa Kiswahili ni kipindi cha dakika 10 kinachotangazwa na radio ya NHK ya dunia kila wiki, katika matangaazo utapata taarifa ya habari idhaa ya Kiswahili.pia taarifa mbalimbali ndani ya mabara mbalimbali mfano Asia na duniani kwa ujumla.
Matumizi ya njia mbalimbali katika urushaji wake matangazo , mfano FM kipitia radio washiriki, TBC FM , RADIO KWA NEEMA FM 98.2 MHz (Mwanza) pia radio mbalimbali sehemu kama Bujumbula, Nairobi na maeneo mbalimbali duniani. pia kwa njia ya setelaiti nayo pia hurusha matangazo yake kwa urahisi kila kona ya dunia. hivyo basi radio japan ina maajabu makubwa sana ndani ya huu ulimwengu.
Ajabu la mwisho ambalo sito kuja kulisahau na ambalo limenifurahisha sana ni juu ya taarifa ya vyoo vya kisasa vilivyogunduliwa na kuanza kutumika nchini Japan. Hivi ni vyoo vya kisasa kabisa ambavyo vimetengenezwa nchini Japan na vimeanza kutumika hii ni taarifa ambayo niliipata kupitia njiia ya mtandao. Haya ni maendeleo makubwa sana.
Mwisho radio Japani ni ya pekee sana kwa sababu hutoa fursa kwa wadau kutoa maoni juu ya maendeleo na maboresho ndani ya radio japani mfano radio Japan idhaa ya Kiswahili.hivyo basi radio japan ni radio iliyojikamilisha katika kufanikisha yale waliyoyaadhimisha.