18 Apr 2016

Swali: Sarufi miundo virai inatofautianaje na sarufi geuzi?

DHANA YA SARUFI
Sarufi ni taaluma ya lugha inayochunguza na kuchanganua vipashio na kanuni mbalimbali zinazotawala muundo wa lugha, (Matinde, 2012.
Sarufi ni utaratibu wa kanuni ambazo humwezesha mtumiaji wa lugha kutunga tungo sahihi zinazoeleweka mara zinapotamkwa. (Kapinga, 1983).
Dhana ya sarufi inatafsiriwa katika mitazamo tofauti lakini yenye kuhusiana. Mtazamo wa kwanza tunaweza kusema Sarufi ni taaluma ya uchambuzi walugha inayojumuisha viwango vyote vya uchambnuzi yaani kiwango cha umbo sauti (fonolojia), kiwango cha umbo neno (fonolojia), kiwango cha miundo maneno (sintaksia) na kiwango cha umbo maana(semantiki), (Massamba, 1999).
DHANA YA SARUFI MUUNDO VIRAI
Sarufi muundo virai ni mkabala wa kimapokeo ambao haujihusishi na sarufi miundo katika marefu na mapana yake, ambapo zilijihusisha sana na sentensi sahili, (Massamba 1999).
Sarufi muundo virai ni kitengo cha sarufi geuza maumbo zalishi, ambacho hujikita katika matumizi ya sheria chache kuzalisha sentensi nyingi zisizo na kikomo, ambazo zina usarufi na hata zile ambazo hazijawahi kutungwa, ( Matinde, 2012).
Sarufi muundo virai ni mpangilio wa vitu vidogo vilivyowekwa pamoja na kujenga kitu kikubwa zaidi. Sarufi miundo virai ni mkabala wa kuchambua lugha kwa kuigawa sentensi katika virai vinayoiunda na kasha kuvichanganua zaidi hadi kufikia neno mojamoja lililokiunda kirai, (Massamba, 2001).
DHANA YA SARUFI GEUZI
Ugeuzi ni utaratibu unaotumiwa kubadili umbo la tungo kuwa umbo jingine kwa kutumia kanuni maalumu. Kwa hiyo ugeuzaji ni mbinu ya kisarufi ambayo hutumiwa katika sarufi geuza maumbo zalishi kuzalisha sentensi lukuki kwa kufuata sheria mahususi, (Matinde, 2012).
Sarufi geuzi hueleza ujuzi wa lugha ambao msemaji mzawa anao ujuzi anaomwezesha kutumia lugha (Habwe na Karanja,2007).
Sarufi geuzi maumbo ni utaratibu wa kubadili maumbo kuwa maumbo meng kwa kufuata kanuni maalumu (Matinde,2012).
Zifuatazo ni tofauti kati ya sarufi miundo virai na sarufi geuzi:
Hutofautiana katika lengo. Lengo la sarufi muundo lilikuwa halifahamiki zaidi ya kutumia taratibu za kijarabati zinazohusu ukusanyaji wa data na kuzichambua pamoja na kuunda kanuni kwa kutumia data hizo. Lakini,
Lengo la sarufi geuzi liko bayana, hujitokeza dhahiri. Lengo la sarufi hii ni kufafanua umilisi wa ujuzilugha ambao huwa mwanalugha anao. Umilisi huo humfanya mwanalugha kutambua viambajengo kati ka tungo, katika mtazamo wa ndani yaani muundo wa ndani.
Hutofautiana katika miundo. Sarufi miundo virai, hii huwa inajikita katika miundo ya nje, ambayo huchunguza na kuchambua sentensi katika umbo la nje.
Mfano; Mama anakula ugali
Hivyo huonyesha tu aina ya maneno husika katika sentensi au tungo kama vile: Mama- Nomino, Anakula- Kitenzi, na Ugali- Nomino. Ilihali,
Sarufi geuzi, hii huwa imejikita katika kuchungaza sentensi kama umbo la ndani na umbo la nje. Muundo wa ndani ni uchopekwaji katika miundo hiyo ambapo muundo wan je lazima upitie katika muundo wa mofofonemiki na kuweka katika kitengo cha fonolojia.
Hutofautiana katika vitengo. Sarufi geuzi ni sarufi ambayo inafumbata vitengo vyote vya lugha ambavyo ni fonolojia, sintaksia, semantiki, na mofofonemiki ambapo kitengo cha fonolojia hushughulikia sauti za lugha, kitengo cha kisintaksia hushughulika na uundaji wa sentensi, kitengo cha semantiki hushughulika na ufasili wa maana, na kitengo cha mofofonemiki huwa na kazi ya kuibadili njeo za wakati. Ilihali
Sarufi miundo virai hufumbata kitengo cha mofolojia ambapo sentensi iligawanywa katika kiunzi cha aina za maneno kama Nomino, Kitenzi, Kivumishi, Kielezi na kihunzi hicho kilijulikana kama utaratibu wa uchanganuzi wa viambajengo.
Hutofautiana katika uhusiano wa sentensi. Sarufi geuzi ilipiga hatua kubwa, kwanza huonyesha uhusiano uliopo kati ya maumbo mbalimbli ya sentensi au tungo. Na pia kuonyesha uhusiano unaoweza kuwepo baina ya sentensi moja na sentensi nyingine.
Mfano: (1) Mtoto mrefu anacheza, na si kusema kuwa Mtoto anacheza mrefu
Huu ni uhusianao kati ya maumbo.
Mfano: (2) Juma alipiga mpira
Mpira ulipigwa na Juma
Huu ni uhusiano wa sentensi moja na sentensi nyingine. Ilihali
Sarufi miundo virai haionyeshi uhusiano kati ya sentensi moja na sentensi nyingine.
Hutofautiana katika uwazi. Sarufi geuzi huonesha sentensi sahihi na ambazo sio sahihi pia huonesha sentensi ambazo zinakubalika na sentensi zisizokubalika kwa msemaji mzawa. Ilihali
Sarufi miundo virai yenyewe haina uwazi huo.
Hitimisho ni kwamba, Sarufi geuzi ilianzishwa kutokana na mapungufu katika sarufi muundo virai. Sarufi iliyokuwepo, sarufi miundo virai, ilishindwa kuonyesha mahusiano yaliyokuwepo baina ya sentinsi zinazo husiana kimaana. Hivyo kutokana na upungufu huo kulikuwa na haja ya kuonyesha uhusiano huo.

MAREJELEO
Kapinga,M.C.(1983). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA). Dar-es-Salaam:
TUKI.
Massamba, D.T., Kihore,M.Y.& Hokororo.(1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu
(SAMIKISA). Dar-es-Salaam: TUKI.
Matinde,S.R.(2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia. Mwanza: Serengeti Educational
Publishers (T) LTD.







14 Apr 2016


Swali :
Linganisha na linganua riwaya pendwa na riwaya pevu kwa kurejelea Riwaya ya Nyota ya Rehema na Kufa na Kupona . 


UTANGULIZI
Masebo (2008) anasema riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni yenye mawanda mapana ,lugha ya kinathari ,mchanganyiko wa visa na dhamira ,wahusika kadhaa na matukio yaliyosukwa Kimantiki yenye kufungamana na wakati na kushabihiana na maisha halisi.

Msokile (1992) ,anasema kuwa riwaya ni kazi ya sanaa ya kubuni yanye maandishi ya kinathari yanayosimulia hadithi ambayo ina uzito ,upana, na urefu wa kutosha ina wahusika mbalimbali wenye tabia za aina nyingi vilevile huwa na migogoro mingi ,mikubwa na midogo ndani yake.

Madumulla (2009) ,riwaya pendwa ni riwaya ambayo inajihusisha na masuala ya mapenzi ,upelelezi, na ujasusi ambapo mara nyingine katika ufuatiliaji wake kuna mapigano makali ya kimwili au kiakili kati ya mtu mmoja au wachache na watu wengi.

Masebo (2008) ; riwaya pevu ni riwaya yenye kuchimbua matatizo au masuala mazito ya kijamii ,kutafuta sababu zake ,athali zake na ikiwezekana ufumbuzi wake. Ni riwaya inayokusudiwa kumkera na kumfikirisha msomaji,sio kumstarehesha tu.

Riwaya pendwa ni kufa na kupona iliyoandikwa na E. musiba na Riwaya pevu ni Nyota ya Rehema iliyoandikwa na iliyoandikwa na M.S Mohammed.

Riwaya pendwa na riwaya pevu hufanana na hutofautiana.Kwa kutumia kitabu cha riwaya ya “ Nyota ya Rehema” iliyoandikwa na M.S Mohammed na riwaya ya “Kufa na Kupona” iliyoandikwa na E .Musiba .

Ufuatao ni ufanano uliopo kati ya riwaya pendwa na riwaya pevu kwa kutumia riwaya ya “Nyota ya Rehema” na riwaya ya “Kufa na Kupona.”

Riwaya hizi zimetumia mandhari halisi ,mandhari kama eneo ambalo tukio la kifasihi kutendeka .riwaya pevu na riwaya pendwa waandishi wake mara nyingi hutumia mandhari ambazo ni halisi na zidhihilikazo katika mazingira halisi. Kwa mfano katika riwaya ya “Nyota ya Rehema “ mwandishi ametumia mandhari kama vile Mwembeshomari (uk 31)

Unakwenda mwempeshomari? Rehema aliulizwa.

Mwembeshomari’ aliitika upesi upesi.”

Vilevile katika riwaya ya “kufa na Kupona” mwandishi mandhari kama vile

Nairobi-kenya . uk 18 ,

upanga –Dar –es –salaam.

nikaingia kwenye gari langu huyoo upanga” uk 12

Riwaya hizi zinaelimisha jamii ;riwaya pevu na pendwa zote zinaelimisha jamii katika mambo mbalimbali kwa mfano riwaya ya “Nyota ya rehema “ mwandishi amewatumia Rehema na Sulubu kuelimisha jamii suala la kutokata tamaa, baada ya wahusika hawa kufukuzwa katika shamba la Ramwe wakapata kijieneo kidogo huko pakani ambapo hapakuwa na rutuba lakini hawakukata tamaa na jitihada za kilifanya shamba kuwa na rutuba kwa kulitilia moto na kuanza kulima kwa juhudi (uk -155 -159 ).

Pia katika riwaya ya Kufa na Kupona mwandishi amewatumia wahusika Sammy na Joe Masanja konesha suala la kutokata tama ambapo wapelelezi wenzao wanauwawa mmoja mmoja kwa vifo vya kutisha na kikatili lakini wao wanaendelea na upelelezi wa nyaraka za siri pasi kuto kukata tamaa mfano Wiilly Gamba anasema

lazima mumkamate na kumuua mimi mwenyewe kama nitakuwa mzima wakati wote wa madhira kama yao………… (uk 24)

Zote zinaonyesha uhalisia wa matukio katika jamii, riwaya pendwa na riwaya pevu zote huonyesha uhalisia wa matukio yaliyo katika jamii . mfano katika riwaya ya “ kufa na kupona” mwandishi anaonyesha matukio ya rushwa,usaliti ,mauaji ya kiharifu na upelelezi ambapo mwandishi anamtimia mhusika piter mpigania uhuru aliyewasaliti wenzake kwa kuiba “nyaraka za siri “ Uk 91.

Pia DR Dikson Njoroge aliyeahidiwa kupewa rushwa na wareno ili kufanikisha wizi wa karatasi za siri (uk 99 ). Pia Benny anayefanya mauwaji ya kiharifu ili kulinda “nyaraka za siri walizoziiba (uk 53). Hivyo hivyo katika riwaya ya “Nyota ya Rehema” mwandishi anaonyesha matukio kama vile Dhuruma ambapo mwandishi anaonyesha rehema anadhurumiwa shamba la Ramwe aliyopewa na Baba yake (Fuad ) enzi za uhai wake na akina salma na karim (uk -150).

.Zifuatazo ni tofauti kati ya riwaya pevu ya “Nyota ya Rehema “ na ile ya “Kufa na Kupona” unadhihirika katika mambo yafuatayo ;-

Mtindo ,huu ni upekee wa mwandishi ambao hutofautisha kazi ya mwandishi mmoja na mwingine katika riwaya ya “Nyota ya Rehema” mwandishi ametumia mtindo wa wimbo. Kwa mfano pale Rehema alipoanza kukalili nyimbo za kubembelezea wototo.

ukimpenda mwanao

Na wa mwenzio mpende,

Wako ukimpa chenga

Wamwezio chenjegere

Humjui akufaaye

Akupaye maji mbele……………”



Nyamaa mama nyamaa

Nyamaa usilie ,

Ukilia waniliza

Wanikumbusha ukiwa

Ukiwa wa baba na mama” (uk 49 na 50)

Vilevile mwandishi ametumia mtindo wa nafsi ya tatu umoja na pia nafsi ya kwanza umoja, mfano “Mansuri alimtazama Rehema aliyekuwa akingojea jawabu kwa hamu “ (nafsi ya tatu umoja ) (UK 43). Na matumizi madogo ya nafsi ya nafsi ya kwanza mfano “ningependa kwenda huko rakwe nikakuona kulivyo “ alisema Rehema (uk 86). Na katika riwaya ya “Kufa na kupona” mwandishi ametumia matumizi ya simu.mfano ni pale polisi walipompigia willy kumjulisha Benny aliwasiliana na nani. Kama vile :

Hello ,Joe huyu “ “polisi stesheni hapa”

Basi hii simu ilikuwa inapigwa huko laving green ,kwenye nyumba ya Dr. Dickson Njoroge “ . uk 80.

Vilevile kuna matumizi ya nafsi ya kwanza umoja “nilipiga simu kwa chifu saa hiyohiyo nikimweleza kuwa awashauri maofisa polisi wasishugulike sana na mauaji mengi yatakayotokea “.

Katika riwaya pendwa mhusika mkuu ni mkwezwa ilhali katika riwaya pevu mhusika mkuu ni wakimapinduzi. Mfano katika riwaya ya Kufa na kupona mhusika Willy Gamba amekwezwa na mwandishi kwa kumpalia sifa kama ,mwenye nguvu ,jasiri na mwenye uwezo mkubwa wa kupambana ,mfano mwandishi anamwinyesha mhusika Gamba akipambana na kundi la watu kumi na tatu na bado akawashinda anasema …

..walipotaka kuanza kunifyatulia risasi haraka nikawafyatulia mfululizo.sita tayari chini nilipiga risasi mkono wa pita risasi ikaanguka chini bila ya kuwa nayo bastolla,ksha nikawamalizia wale wane waliobaki”………(uk 93). Pia katika riwaya ya “Nyota ya Rehema” mwandishi anamwonyesha mhusika mkuu Rehema kama mwanamapinduzi pale ambapo moja alipotoroka nyumbani kukataa mateso ya mama yake wa kambo (uk 22) pia kujiepusha kuingiliwa kimwili na mansuri kwa kumuuma meno na kupata nafasi ya kujiokoa (uk 65) tatu ,kupitia jitihada ya kufanya kazi kama ufugaji na kilimo ili kupambana na maisha yake na mmewe aliyemchagua kuishi naye (uk 104)

Riwaya imetumia lugha rahisi na inayoeleweka ilihali riwaya pevu imetumia lygha ngumu. Kwa mfano katika riwaya ya nyota ya rehema mwandishi ametumia misamiati ambayo si rahisi kuelewa maana yake mfano bigija,dhiyaa,ghila (uk 170) pia mwandishi ametumia mafumbo kama ubwebwe wa shingo haujamtoka………(uk 45) lakini, katika riwaya Kufa na kupona mwandishi ametumia lugha rahisi na inayoeleweka na iliyo na methali mfano mtaka cha sharti ainamen (uk 44).

Matumizi ya taharuki taharuki kama hamu ya msomaji kujua matokeo ya kitu Fulani katika riwaya pevu matumizi ya taharuki hutumika kwa kiasi kidogo mfano katika riwaya ya Nyota ya Rehema,taharuki imejitokeza ktika (uk 12) mwandishi anasema

jina lako nani ? Faud alijisikia akiuliza kwa sauti iliyokuwa si yake

Adili ; alisikia jawabu akija

Aligeuka kumtazama na macho yao yakakutana ,roho zao zikaumana …………milele. Baada ya hapo hakuna chochote kilichoendelea baada ya hapo mwandishi ametuacha kwenye taharuki. Ilhali katika riwaya pendwa taharuki hujitikeza kiasi kikubwa mfano katika riwaya ya kufa na kupona wandiishi anathibitsha katika ukurasa wa 7 kama ifuatavyo “Amani lete madebe ya petrol na kiberiti”. Hii ni baada ya Sammy na willy kukamatwa na benny hivyo basi msomaji anapata hamu ya kujua nini kitatokea baadaa ya kuletwa petrol na kiberiti.

Pia katika ukurasa 45 taharuki imejitokeza pale willy aliposema “alinivuta akaanza kufungua tai yangu,kasha shati langu , halafu suruali yangu……….. tukajilaza . pia hapa msomaji atataka kuelewa kitu gani kiliendelea baada ya hapo.

Pia katika ( uk 67 ) ni pale ambapo willy anamkuta lina amechomwa kisu na mtu aliyemfahamu na anataka kumuuliza bila mafanikio. Hivyo msomaji Napata maswali je? Lina atakufa au atapona baada ya kujeruhiwa vibaya na mtu asiyefahamika

Vilevile taharuki nyingine imejitokeza pale ambapo willy Gamba alivyokamatwa na benny na akaambiwa asali sala yake ya mwisho kabla sijammiminia risasi kama mwenzake (uk 89 ).hivyo msomaji anapata taharuki kuwa je? Anaweza kufa au kunusulika? Lakini hata Gamba mwenyewe anakuwa yuko kwenye taharuki je? Anaweza kunusulika.

Wahusika katika riwaya pevu huakisi hali halisi ya maisha ilhali wahusika katika riwaya pendwa hupewa uwezo mkubwa usio wa kawaida wa kutenda matukio yanayosawiriwa Wahusika katika riwaya pevu huakisi hali halisi katika jamii riwaya hizi waandishi wametumia wahusika wao ambao ni tofauti dhidi ya uwakilishaji wao wa uhalisia wa mambo. Riwaya ya “Nyota ya Rehema” kama Rehema alipokuwa akipambana kupata mali yake ya urithi wa mali ya baba yake Faud, ambaye alifariki.hali hii ya urithi wa mali kwa mtu aliyefariki ni hali halisi kwa sababu yanatokea. katika jamii . mwandishi anathibitisha katika (uk 143) “ konde zilizomo na shamba lenyewe ni mali ya yangu bwana muridi na mimi ndiye motto wa maarehemu bwana Faud………………….. . Na katika riwaya ya “KUFA NA KUPONA “ mwandishi ameonyesha hali isiyo halisi kwa kumtumia mhusika Gamba aliyepewa uwezo mkubwa pale anapopambana na watu kumi na watatu na kuwashinda . hali hii si ya kawaida katika jamii.Katika (uk 93) walipotaka kuanza kunifyatulia risasi haraka nikawafyatulia mfululizo.sita tayari chini nilipiga risasi mkono wa pita risasi ikaanguka chini bila ya kuwa nayo bastola ,kasha nikawamalizia wale wakiobaki”

Katika riwaya pendwa mwanamke amechorwa kama chombo cha anasa na katika riwaya pevu mwanamke amechorwa kama mlezi na mzazi. Mwandishi wa riwaya ya kufa na kupona anaonyesha ambavyo lina na lulu wanavyojidhihirisha na masuala ya anasa kama kuwa na mahusiano wa kimapenzi na mhusika Benny aliyekuwa mharifu katika wizi wa nyaraka za siri (uk 3) lakini mwandishi wa riwaya ya “Nyota ya Rehema “ anamwonyesha Bii kiza katika nafasi ya mlezi kwa kumlea Rehema baada ya kifo cha mama yake (Aziza) pia Rehema anachorwa kama mzazi na mlezi wa mwanae aliyeitwa Faud baada na kuonana na sulubu mume aliyemchagua mwenyewe (uk 44)

Suluhu ya matatizo katka Riwaya pevu hutolewa hali ambayo ni tofauti na riwaya pendwa . suluhu ya matatizo katika riwaya ya “Nyota ya Rehema “ imedhihirika pale ambapo mhusika Rehema baada ya kupiia mikasa mingi katika maisha ambayo ilimfedhehesha, mfano kufa kwa mama yake (Aziza ) safari yake ya kutoroka nyumbani kwao ,maisha magumu aliyokuwa nayo mjini ,kudhurumiwa haki ya urithi lakini badi hakukata tama,hatimaye akampata sulubu ambaye kwake alimuona ni mume mchapakazi na chaguo lake katika maisha. Ilhali katika riwaya pendwa, suluhisho la matatizo haijaonyeshwa , kwani mwandishi wa riwaya ya kufa na kupona anaonyesha mwisho wa riwaya kuwa Lulu anawapigia simu

Tofauti nyingine ni riwaya pevu imejikita katika mkondo wa kihalisia ilihali riwaya pendwa imejikita katika mkondo wa kipelelezi, mkondo wa kiuhalisia ni aina ya mkondo ambao hueleza jambo katika uhalisia wake. Katika riwaya ya nyota ya rehema mwandishi amejaribu kueleza matatizo mbalimbali yanayoakisi jamii zetu. Mfano; ugumu wa maisha ,watu kunyimwa haki zao mwandishi katika (uk 143) anathibitisha

Konde zilizomo na shamba lenyewe ni mali yangu bwana Mudiri na mimi ndiye mototo wa marehemu bwana Faud……………” . Hapa mhusika Rehema alikuwa akijitetea pindi alipokuwa anataka kudhurumiwa shamba wakati ni haki yake kabisa. Hivyo basi haya ni masuala ya kihalisia kabisa katika jamii zetu. Lakini mkondo wa kipelelezi ni aina ya mkondo ambao hujikita kuzungumzia masuala ya mapenzi, upelelezi na ujasusi katika riwaya ya Kufa na kupona tunaona mwandishi ameeleza na kuonyesha vya kutosha masuala ya upelelezi na mapenzi mfano katika (uk 66) mwandishi anasema

kwa hiyo kazi kubwa sasa ni kutafuta kwa kila njia tumjue huyo “ bosi mi nani. Na habari nilizozipata kwa James hizo karatasi zinabadilishwa kesho usiku………. .Hapa ni Willy alikuwa anazungumza na Sammy.hivyo basi hapa inasibitisha kuwa hawa wanajihusisha na vitendo vya upelelezi. Pia masuala ya mapenzi katika riwaya hii pia yapegusiwa kama sifa mojawapo mwandishi katika (uk 105)

Oh Willy,nilikuwa nakuota sasa hivi umenikumbatia ,kumbe ni kweli .Oh ,sasa nimepona kabisa ,nibusu Willy nirejewe na uhai”. Hapa ni lina baada ya kukutana na Willy.hivyo basi hii inathibtisha riwaya pendwa imejikita katika mkondo wa kipelelezi.

Kwa kumalizia riwaya pendwa na riwaya pevu zote kwa ujumla hubeba dhima za fasihi nia na madhumuni ni kufikisha ujumbe mzito uliokusudiwa kwa jamii lengwa ,mfano wa dhima hizo ni kuelimisha ,kukosoa ,kuburudisha kuonya ,kutunza historia ya jamii hivyi basi fasihi ya riwaya inamchango mkubwa katika jamii.




                                                             MAREJELEO
  1. Madumila, J.A. (2009),Riwaya ya Kiswahili,Nadharia Historia na Misingi ya Uchambuzi Dar-es-Salaam:Mture Education Publishers.
  1. Masebo, J.A.(2007), Nadharia ya Fasihi (Fasihi kwa Ujumla).Dar-es- Salaam: Nyambari Nyangwine Publishers.


8 Apr 2016


 NENDA KAFUNDISHE KISWAHILI NJE YA NCHI SASA

wadau wangu kamwe siwezi kuwatupa kama nyinyi msivyoweza kunitupa kwa jinsi mnavyotembelea blog yangu mara kwa mara basi hata mimi nafarijika sana. leo nimewaletea fursa adhimu sana kama wengi wenu mlivyoomba kwenye ukurasa wangu wa facebook, endapo itapatikana fursa ya kwenda kufundisha kiswahili nje ya nchi basi tujulishane .sasa ni wewe mwenyewe kuanza kufanya maombi hayo ili kuchangamkia fursa hii.fanya kwa uangalifu na ni mchakati mrefu kidogo, kwa yeyote atakaye tatizika au kukwama mahali tafadhari usisite kuwasiliana  nami kwa namba zilizopo hapo chini, kwani sisi wote ni Watanzania na mafanikio haya yote ni ya watanzania. Jaribu bahati yako. Changamkia fursa ndugu yangu.

Bm mtillah : 0717608230 WHATSAPP, 0683797770
EMAIL: bamtila@gmail.com

          Application cycle 2017 - 2018 is now open 
The Public Affairs Section of the United States Embassy in Dar es Salaam is seeking qualified candidates for the Fulbright Foreign Language Teaching Assistant (FLTA) program. Online applications are now available. The deadline for submitting applications is June 1, 2016. Only successful candidates will be called for interviews scheduled for mid-July, 2016.
The Foreign Language Teaching Assistant (FLTA) Program is funded by the U.S. Department of State. Teaching assistants are vetted through the J. William Fulbright Foreign Scholarship Board. The program aims to strengthen U.S. foreign language instruction and promote mutual understanding by establishing a foreign language native speaker expertise on U.S. campuses. The program enables the teaching assistants to complete their home country pre-service training by engaging in non-degree studies at accredited post-secondary U.S. educational institutions while teaching one or two language courses. Additionally they serve as resource persons in conversation groups, cultural representatives, attendants in language laboratories, coordinators of extracurricular activities or supervisors of clubs and language houses. Teaching assistants are expected to teach their language/culture for up to 20 hours per week while taking two courses per semester. All FLTAs receive room and board, a monthly stipend, and tuition waiver for the required coursework, in addition to Fulbright immigration services. The Fulbright grant is for one academic year and is non-renewable.  Tanzanian FLTA participants teach Swahili at Universities, colleges and occasionally secondary schools in the United States.

These teaching assistants are expected to teach Swahili language and Tanzania culture for up to 20 hours per week while taking two graduate-level courses per semester. The grant is for one academic year and is non-renewable. The program is designed to have native language and cultural informants who are close in age to undergraduate students in the USA. Normally, FLTAs would teach:
  • beginning level or conversation courses;
  • work in a language lab;
  • animate a language table; and
  • organize cultural activities or have similar duties.

The U.S. Government covers FLTAs’ costs related to travel, health insurance and subsistence expenses. Institutions where the FLTAs are placed provide tuition scholarships for the required coursework. The selection process for Tanzania is facilitated through the American Embassy in Dar es Salaam.

Applicants must be teachers of English or final year students studying English language learning, and at minimum must possess the equivalent of a U.S. bachelor's degree by June 1, 2016, to allow time to submit an official transcript prior to the start of the Fulbright FLTA Program and who are willing to travel for one academic year.

To apply, please refer to the online application.  You must submit the following documents to the U.S Embassy Dar Es Salaam;
  1. Signature page of your application;
  2. Three reference letters. (Filled out by teachers or other professionals with whom you have worked); and
  3. Copies of relevant certificates (degree, diploma).
 To submit your application, you can;
  • Hand-deliver to the address below;
  • Post to the address below; or
  • Email scanned copies to drs_exchanges@state.gov.
 Fulbright Program Coordinator
Office of Public Affairs
U.S Embassy Dar Es Salaam
686 Old Bagamoyo Rd. - Msasani
Box 9123, Dar Es Salaam.
Voice: 255 22 229 4186
Fax:    255 22 229 4722 
Please note that only a small number of applicants will be contacted for an interview. Also, only nominated candidates will be required to sit for the TOEFL exam and submit a medical report.

6 Apr 2016

UCHAGUZI WA VIONGOZI WAPYA NDANI YA
CHAWAKAMA SAUT-MWANZA
Chama Cha Wanafunzi Wanaosoma Kiswahili Vyuo Vikuu Afrika Mashariki(CHAWAKAMA) tawi la SAUT-MWANZA linatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wa chama hicho tarehe 16/04/2016 siku ya jumamosi hii ni katika kutekereza matakwa ya katiba ya chama hicho kama inavyosomeka  katika sura nne kifungu kidogo( muda wa uongozi 4.4. )“kamati tendaji itakuwa madarakani kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya hapo uongozi utaitisha uchaguzi tena………”. . Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi bwana Anodius Kakuba amesema maandilizi yapo vizuri na watu wameanza kuchukua fumu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuzingatia vigezo, sifa na masharti ya kuwa kiongozi ndani ya Chawakama kama katiba ya CHAWAKAMA-SAUT inavyojieleza.
Mwisho wa kuchukua na kurukua fomu ni ijumaa ya tarehe 8/04/2016 kutafuatiwa na usaili wa wagombea hao siku ya jumamosi ya tarehe 9/04/2016.
Siku ya tarehe 16/04/2016 ndio siku ya Uchaguzi wenyewe hapo ndipo uongozi mpya wa CHAWAKAMA – SAUT(MWANZA) utakabidhiwa madaraka .
Kama unajiona una sifa za kuwa kiongozi kama katiba inavyojieleza katika sura ya nne kifungu kidogo 4.5 (masharti ya uongozi) Unakaribishwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi unayoitaka. Fomu zinapatikana kwa mwenyekiti pamoja na katibu wake wa tume ya uchaguzi CHAWAKAMA SAUT.
Mawasiliano:
Mwenyekiti wa tume :0765 367 768
Katibu wa tume : 0764 832 106.


KUMBUKA
Taarifa zote kuhusu uchanguzi utaendelelea kuzipata kupitia blog hii

Powered by Blogger.

Wasiliana nami papo kwa papo

Name

Email *

Message *

Ads 468x60px

Breaking News

Top Featured

Featured Posts

Sample text

Sample Text

Recomended

Facebook

Advertise

Most Popular

Connect With Us

Followers

Social Icons

Pages

Pages

BTricks

Pages

Popular posts

Tafuta chochote ukiwa hapahapa

Kategori

Recent Comments

You can replace this text by going to "Layout" and then "Page Elements" section. Edit " About "

recent posts

Video Of Day

TRANSLATE

Instructions

Video

Flickr Images

FURAHIA UWEPO WAKO HAPA

Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

Imetembelewa mara

TAKWIMU ZA WATEMBELEAJI

Popular Posts

SAJIRI

Definition List

premium-wordpress-themes.org