6 May 2016



UTANGULIZI
Vitamkwa, ni neno linalotokana na kitenzi ‘Tamka’ ambalo lina maana ya kitendo cha kutoa nje ye kinywa au pua ya mwanadamu sauti ambazo hutumika katika mazungumzo au usemi wowote uwao. (Kihole, Masamba na Hokororo, 2003).
Hivyo basi, vitamkwa ni sauti ambazo hutolewa na binadamu kupitia katika chemba ya kinywa na chemba za pua  kwa kufuata utaratibu maalumu. Utaratibu huu huhusu namna au jinsi ya kuzitoa sauti hizo na mahali pa kutolea sauti hizo.
Mfano:  [ p ] + midomo – mahali
               [ p ] + midomo ishikane na kuachana
Lakini pia sauti hizi zitamkwazo zaweza  kuwa ni konsonanti  na irabu (vokali).
Mfano:  [ b ], [ d ] kama konsonanti na [ e ],[ u ],[ i ] kama vokali au irabu.  
Vitamkwa, ni sauti zitumikazo katika lugha fulanina hujumuishwa kwa jina la Alfabeti ambazo ndani yake kuna konsonanti na irabu.  Mfano: a, b, c, d, e, f.
Kuna baadhi ya wataalamu mbalimbali ambao wameelezea sifa za vitamkwa na baadhi ya wataalamu hao ni pamoja na Romani Jackobson na Nikolaji Trubertzkoy.
Roman Jakobson,Ni raia wa Urusi(Russia) alizaliwa October 11,1896,Moscow na alifariki July18,1982.Cambrige alikuwa mwalimu wa Linguistic na ni mmoja wa waanzilishi wa Prague kwa kushirikiana na Halle walibainisha sifa Kinzani za lugha katika makund imawili ,Konsonanti na vokali na baadae makundi madogo manne Konsonanti halisi,Vokali,Vitambaza naViyeyusho kwa kutumia Nadharia ya Sifa Pambanuzi
Nikolaj Trubertzkoy,huyu nae ni raia wa Urusi(Russia)  Alizaliwa April,16,1890 mjini Moscow na kufariki  June,25,1938 alikuwa mwalimu wa masomo ya Historian a Kiingereza katika vyuo vikuu vya Moscow,Vienna na Sofia nchini urusi pia alikuwa mwanzilishi wa mawazo ya Prague.Mwaka 1969 alibainisha sifa za vitamkwa kwa kutumia Nadharia ya Upambanuzi au Nadharia ya Ukinzani Pambanuzi .zifuatazo ni tofauti za sifa za vitamkwa zilizoelezwa na Nikolaj Trubertzkoy na Roman Jakobson.
Trubertzkoy, alizibainisha sifa za vitamkwa kifonetiki na kifonolojia lakini alijikita zaidi katika Fonetiki kwani katika upambanuzi wake ametumia lugha mbalimbalikama; Kiingereza,Kijerumani na Kiswahili.Ilhali Jakobson alipendekeza sifa za vitamkwa  kifonetiki na kifonolojia lakini alielemea zaidi katika sifa za vitamkwa kifonolojia katika lugha ya Kiswahili.Ambapo alielezea Konsonanti na Vokali za Kiswahili.
Nikolaj Trubertzkoy,ametumia Nadharia ya upambanuzi Wakati Jakobson alitumia Nadharia ya Sifa Pambanuzi.
 Katika Nadharia ya Upambanuzi, Trubertzkoy madai yake ya msingi ya Nadhari yake ni kwamba pakiwa na Upambanuzi basi lazima patakuwepo na ukinzani.kwa mfano Ukinzani wa kiuwili ambapo jumla ya sifa bainifu zinazochangiwa na sauti mbili kinzani hupatikana katika sauti hizo mbili peke yake na si kwingineko.Mfano Vipasuo vya mdomo [P] na [b] katika Kiswahili ambavyo vinachangia sifa ya Vipasuo vya midomo, hakuna vipasuo vingine vinavyochangiansifa hiyo.Lakini Katika Nadharia ya Sifa Pambanuzi yake Roman Jakobson, anabainisha sifa za Kimatamshi dhidi ya Sifa Kiaukustika.Kwa mfano katika sifa za Kiaukustika anabainisha sifa ambazo ni;
Sifa ya Usononanti.
Hii ni sifa ambayo hujitokeza katika kutamka irabu na huwa na mguno mkubwa (vokali). Sifa hii ilitumiwa kubainisha sauti za konsonati na irabu. Katika ubainishaji wake, irabu ingeoneshwa kuwa na sifa ya usonoranti [ +usonoranti], lakini konsonanti ingeoneshwa kuwa si ya usonoranti [-usonoranti]. Mfano, kimadende na kitambaza /r/ na /l/ ni konsonanti lakini huwa na usonoranti [+usonoranti]. Nazali hupewa sifa ya usonoranti, /m/ na /n/ [+usonoranti], viyeyusho navyo pia hupewa sifa ya usonoranti, /w/ na /y/.  
 Sifa ya Uprotensi.
Sifa hii hutumiwa kutofautisha zile fonimu ambazo ni kaze. Sauti kaze, ni zile ambazo hutamkwa kwa kutumia nguvu nyingi na zinakaa muda mrefu zinapotamkwa. Mfano, sauti si ghuna huwa ni kaze (+kaze) Ilihali sauti si ghuna ni sauti si kaze (-kaze).
Mfano: sauti /t/ si ghuna kwa hivyo ni kaze (+kaze), fonimu /d/ ni ghuna kwa hivyo ni sauti si kaze (-kaze).
 Sifa ya Utoni
Hii ni dhana ambayo hutumiwa kuelezea uhusiano baina ya sauti mbili au zaidi za fonimu moja ambazo haziwezi kutokea katika mazingira sawa. Mfano, fonimu /k/ na /v/.
                        [k]                                     [v]
                       +Konsonanti                    +Konsonanti     
                       +Kizuiwa                         +Kikwamizwa   
                       +Kaka laini                      +Midomo meno
                       -Nazali                              -Nazali
                       -Ghuna                             +Ghuna
Katika kuzieleza sifa za Vitamkwa ,Trubertzkoy alielezea kwa kuzigawa sifa hizo katika Seti tatu za Ukinzani Pambanuzi ,seti hizo ni kama zifuatazo;
Seti ya kwanza,katika seti hii alizipambanua katika vipengele vinneambavyo ni; Ukinzani kiuwili,Ukinzani kiwingi, Ukinzani  kiwiani na Ukinzani kipeke.
        i.            Ukinzani kiuwili, huu ni ukinzani ambao anaeleza kuwa Sifa mbili kinzani hupatikana katika sauti hizo mbili peke yake na si kwingineko.Mfano,vipasuo vya midomo  [P] na [b] katika Kiswahili ambavyo vinachangia sifa ya kuwa vipasuo vya kinywa vya midomo .ukinzani wake unajidhilisha katika kielelezo
            [p]                                                        [b]
+Kipasuo                                               +kipasuo
-ghuna                                                  +ghuna
      ii.            Ukinzani uwingi , ni ukinzani ambao unaeleza jumla ya sifa bainifu zinazochangiwa na sauti hizo huweza kupatikana katika seti ya sauti nyingine pia mfano herufi P na R ambazo zote zinachangia mkunjo wa upinda wa kuelekea kulia ,lakini sihizo tu balizipo na herufi nyingine kama herufi B na D ,hvyo ukinzani huo uhuhusicha herufi nyingi .
    iii.            Ukinzani kiwiani , ukinzani huu huelezae Sauti mbili zinazowiana na kukinzana na suti nyingine mbili zinazouwiana .mfano sauti [F] na [v], na ukinzana na [s] na [z] katika Kiswahili . tazama kielelezo hiki.
[f]           na         [v]                      [s]      na   [z]
        [+midomomeno ] [+midomomeno] [+ufizi]   [+ufizi].
ivUkinzani kipeke, ni ukinzani ambao ni wa kipekee kabisa. Mfano [r] na [l] kaika lugha ya kiingereza hakuna memba wengine wanaohusiana na uhusiano na wanamna hiyo . na katika lugha ya Kiswahili ukeli ni kwamba sauti [r] ni kimadende ambacho kipo peke yake pia sauti [l] ni kitambaza ambacho kipo peke yake pia .
Seti ya pili  ,katika seti hii Trubertzkoy ameigawa katika seti ndogo ndogo tatu ambazo ni seti ya kuzinzani kibinafsi, ukinzani kimwachano taratibu na ukinzani kisawa .
                    i.            Ukinzani kibinafsi , ni ukinzani ambao sauti moja inakuwa na alama ya ziada (sifa ya ziada) na suti nyingine inakuwa haina .mfano sauti moja inakuwa ghuna na nyingine inakuwa sighuna kama vile sauti [p] na sauti [b], pia sauti moja yaweza kuwa nazali na nyingine ikose sifa hiyo , kama vile sauti  [m] na [k] .
                  ii.            Ukinzani kimwachano taratibu ,ukinzani huu unaeleza kuwa memba wa seti wanapishana kwa viwango tofauti vya sauti ile ile, mfano sauti ya vokali [o] na [u] .  Tazama kielezo kifuatacho
              [o]                                      [u]
         +vokali                                +Vokali
        +Nyuma                               +Nyuma
        +Mviringo                            +Mviringo
        +Nusu juu                             +Juu 
iii Ukinzani wa kisawa, ukinzani wa memba wa kundi moja ni sawa na ukinzani baina ya kundi jingine.Kwa maana kwamba ukinzani wao si wa kupishana kwa viwango vya sifa ile ile.Mfano sauti [p]na [t],[f] na [k] katika lugha ya Kijerumani.



Seti ya tatu, hii ni seti  ambayo inaelezea  ukinzani imara  na ukinzani usio imara.Ukinzani imara ni ule ambao Usio badilifu,Mfano ni ukinzani baina ya sauti [t,d na l] ambazo zote  ni sauti za ufizi. Na  ukinzani usoimara ni ule ukinzani ulobadilifu yaani hubadilika . mfano katika mazingira ya sauti [l] hubadilika na kuwa sauti [d] katika mazingira ya kutanguliwa na Vokali [i] ,mfano  Ulimi-Ndimi.Hivyo sauti [l] si imara na sauti [d] ni imara.
Ilhali, Roman Jakobson   amependekeza sifa za vitamkwa katika makundi makuu mawili ambayo ni Kundi la sauti za Konsonanti na Kundi la sauti za vokali. Ambayo pia aliyagawa katika ,makundi madogo madogo manne.ambayo ni Konsonanti halisi,Vokali,Vitambaza na Viyeyusho.Mfano Konsonanti halisi huwa na sifa ya ukonsonanti pekee na hukosa sifa ya vokali.Kama vile fonimu /p/ .Vokali ni vokali peke yake bila kuwa na sifa ya konsonanti ,kama fonimu /a/, vitambaza ni muunganiko wa konsonanti na vokali, viyeyusho,hivi viko pekee havihusishi konsonanti wala vokali,kama /y/. Uainishaji huu una maana kwamba kuna sauti zinazochangia sifa kama inavyodhihirika katika mfano ufuatao.
 Konsonanti+Vitambaza       [+konsonanti]
 Konsonanti+Viyeyusho       [-Vokali]
 Vokali+Vitambaza               [+Vokali]
 Vokali+Viyeyusho               [-Konsonanti]
Hitimisho.
Kutokana na tofauti za sifa za vitamkwa zilizoelezwa na wataalamu hawa,pia kuna uhusiano wa sifa za vitamkwa kwa kigezo cha uwili.
                                 
   
 MAREJELEO.
Massamba,D.P.(2011).Maendeleo ya Sarufi ya Kiswahili.Nairobi: Phoenix Publishers
Matinde,R.S.(2012).Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia.Mwanza: Serengeti Educational  
        Publishers
Mgullu,R.S.(2010).Mtalaa wa Isimu:Fonetiki,Fonolojia,na Mofolojia ya Kiswahili.Dar-es-
         salaam :Longhorn Publishers.
Hokororo J.I, Kihore Y.M, & Masamba D.P.B, (2003). Sarufi Miundo ya Kiswahili
         Sanifu.SAMIKISA.Dar-es Salaam: TUKI Publisher. 

0 maoni:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Wasiliana nami papo kwa papo

Name

Email *

Message *

Ads 468x60px

Breaking News

Top Featured

Featured Posts

Sample text

Sample Text

Recomended

Facebook

Advertise

Most Popular

Connect With Us

Followers

Social Icons

Pages

Pages

BTricks

Pages

Popular posts

Tafuta chochote ukiwa hapahapa

Kategori

Recent Comments

You can replace this text by going to "Layout" and then "Page Elements" section. Edit " About "

recent posts

Video Of Day

TRANSLATE

Instructions

Video

Flickr Images

FURAHIA UWEPO WAKO HAPA

Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

Imetembelewa mara

TAKWIMU ZA WATEMBELEAJI

Popular Posts

SAJIRI

Definition List

premium-wordpress-themes.org