21 May 2016







TANZU ZA FASIHI SIMULIZI.

Utangulizi.
Fasihi Simulizi imefasiliwa na wataalamu mbalimbali miongoni mwa waalamu hao ni M.M.Mulokozi (1996) anasema Fasihi Simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi.
TUKI (2004) Fasihi Simulizi ni kazi ya fasihi inayohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo kama vile; hadithi, ngoma na vitendawili.
Balisidya (1983) anasema fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake.
Wanjara (2011) anasema fasihi simulizi ni sanaa ambayo vyezo kuu ya utunzi, uwasilishaji na usambazaji wake ni sauti pamoja na vitendo. Fasihi simulizi ni sanaa inayotumia mazunguzo na vitendo kisanii ili kuwasilisha maarifa au ujumbe Fulani kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Kwa ujumla, fasihi simulizi nisanaainayobuniwa ikiwasilishwa na kusambazwa kwa (lugha ya) mdomo, na vyombo vyake vikubwa ni mdomo na sauti ya binadamu katika hali ya kuimba, kusimulia, kuiga ,kughani, kutamba na kutenga. Kama vile vitendawili vinavyotegwa kwa hadhira.

Tanzu za fasihi simulizi
Tanzu ni istilahi inayotumiwa kuelezea au kurejelea aina ya kazi mbalimbali za kifasihi, inawezekana utanzu mkuu kuwa na vitanzu vingine mbalimbali.
Tanzu za fasihi simulizi ni nyingi na si rahisi kuzianisha zote. Waandishi wafuatao wamejadili tanzu kadhaa za fasihi simulizi kama ifuatavyo:-
M.M.Mulokozi katika makala yake ya tanzu za Fasihi Simulizi iliyo katika jarida la Muulika namba 21(1989) amezigawa tanzu na vipera vya Fasihi Simulizi kwa kutumia vigezo viwili ambavyo ni,kigezo cha kwanza ni umbile na tabia ya kazi inayohusika na kigezo cha pili ni muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira. Umbile na tabia ya kazi inayohusika: katika kigezo hiki Mulokozi ameangalia vipengele vya ndani vinavyoiumba sanaa hiyo na kuipa muelekeo au mwenendo. Baadhi ya vipengele hivyo vya ndani ni namna lugha inavyotumika (kishahiri, kinathari, kimafumbo, kiwimbo na kighani), muundo wa fani hiyo na wahusika. Kwa upande wa muktadha na namna ya uwasilishaji amezingatia kuwa, Fasihi Simulizi ni tukio hivyo huambatana na muingiliano wa mambo matatu ambayo ni muktadha, watu na mahali. Mwingiliano huu ndio unaotupa muktadha na muktadha ndio unaoamua fani fulani ya Fasihi Simulizi ichukue umbo lipi, iwasilishwe vipi kwa hadhira, kwenye wakati na mahali hapo. Hivyo hadithi inaweza kugeuzwa wimbo, utendi unaweza kuwa hadithi na wimbo unaweza kugeuzwa ghani au usemi kutegemea muktadha unaohusika.
Mulokozi ameanisha tanzu sita za fasihi simulizi kama ifuatavyo :-
         i.            Mazungumzo
       ii.            Masimulizi
      iii.            Maigizo (drama)
     iv.            Ushairi
       v.            Semi
     vi.            Ngomezi (ngoma)
Mazungumzo ni maongezi au maelezo yam domo katika lugha ya kawaida juu ya jambo lolote ile. Si kila mazungumzo ni fasihi mazungumzo ili yawe fasihi lazima yawe na usanii wa aina Fulani na uhalisia baada ya kuunakili.mfano tanzu zinazoingia katika fungu la mazungumzo ni kama hotuba, malumbano ya watani, ulumbu,soga na mawaidha.
Masimulizi ni fasihi yenye kusimulia habari Fulani Mulokozi (1989) anasema kuwa masimulizi ni fasihi ya kihadithi na fani zake huwa na sifa kama kuelezea tukio katika mpangilio Fulani mahususi, huwa na wahusika yani watendaji.Katika Mulika 21 Mulokozi amegawanya fasihi simulizi katika tanzu zifuatazo za kihadithi ambazo ni ;ngano,visakale,tarihi, istiara,mbazi na kisa.
Semi ni tungo au kauli fupifupi zenye kubeba maana Fulani au mafunzo muhumu katika jamii, Mulokozi ameanisha tanzu semi kama ifuatavyo; methali,mafumbo,vitendawili.
Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi ya kuwa na vina ushairi una ufasaha wa maneno au muktasari wa mawazo na maono ya ushairi huvuta moyo kwa namna ya ajabu. Ushairi hupambanuliwa na lugha ya kawaida kwa kutumia lugha na mbinu za kimuktadha. Mulukozi (1989) amegawa ushairi katika mafungu mawili ambayo ni nyimbo na uwasilishaji.
Maigizo (drama) ni sanaa inayotumia watendaji kuiga tabia au matendo ya watu na viumbe wengine ili kuburudisha na kutoa ujumbe Fulani. Maigizo ni sanaa inayopatikana katika makabila mengi. Mulokozi anasema drama (maigizo) ya kiafrika huambatana na ngoma mtambaji wa hadithi au matendo ya kimila.
Ngomezi ni midundo Fulani wa ngoma kuwakilisha kauli Fulani katika lugha ya kabila hilo mara nyingi kauli hizo huwa ni za kishairi au kimafumbo.

Nae Wanjara (2011) anaainisha tanzu mbalimbali za fasihi simulizi ambazo ni zifuatazo :-
         i.            Hadithi za kihistoria
       ii.            Hadithi za kubuni
      iii.            Ushairi (nyimbo)
     iv.            Semi
       v.            Maigizo
     vi.            Mazungumzo
    vii.            Ngomezi.
Ndungo na wangali, wao wanaziainisha tanzu tano za fasihi simulizi wanaanza na :-
         i.            Hadithi
       ii.            Ushairi na nyimbo
      iii.            Sanaa za maonyesho
     iv.            Methali
       v.            Vitendawili.

Njogu na Chimera (1999) anaanisha tanzu zifuatazo za fasihi zifuatazo za fasihi simulizi:-
         i.            Hadithi
       ii.            Nyimbo
      iii.            Methali
     iv.            Vitendawili
Nyambari  na Masebo (2007) wanaainisha tanzu zifuatazo za fasihi simulizi  ambazo ni hadithi, semi, ushairi na sanaa za maonesho.





Wataalamu wote wana mitazamo inayoendana katika kuainisha tanzu za fasihi simulizi, baada ya kutambua mawazo yao sasa ni vyema kutumia nafasi hii kuziweza tanzu hizi katika makundi jumuishi manne (4) ambayo ni `:-
                                     FASIHI SIMULIZI
HADITHI
SEMI
USHAIRI
SANAA ZA MAONYESHO
Ngano
Methali
Nyimbo
Majigambo
Tarihi/visakale
Vitendawile
Maghani
Tambiko
Visasili
Misimu
Ngonjera
Miviga
Soga
Mafumbo

Michezo ya watoto
Visoga
Lakabu

Ngoma

Misemo
Mizungu

Utani
Ngonjera
Vichekesho
Jukwaani



Hadithi
Ni tungo za fasihi simulizi zitumiazo lugha ya nathari (lugha ya ujazo ya maongezi ya kila siku). Mtiririko wa matukio ndio unaotawala masimulizi. Hadidhi hizozaweza kuwa ngano zitumiazo wahusika kama wanyama,miti na watu kueleza au kuonya kuhusu maisha, tarihi ni hadithi zinazohusu matukio yaliyotendeka zamani; visasili ni hadithi ambazo huwa na wahusika wa aina tofautitofauti ambao ni bapa hasa miungu na binadamu husimulia uu ya matukio ya kiada, vigano ni hadithi fupi zinazoeleza makosa au uovu wa watu Fulani na kueleza maadili Fulani; soga huumuisha hadithi ndogondogo ambazo huteta utani vilevile huwa na ucheshi.
Hivyo tunaona kuwa hadithi huumuisha tungo yeyote ya kubuni inayosimuliwa kwa lugha ya nathari.
Mfano,mfano katika fasihi simulizi ni za aina nyingi lakini zote huanza kwa njia moja inayofuata mtindo huu.
Msimulizi : paukwa!
Wasikilizaji : pakawa!
Msimulizi : paukwa!
Wasikilizai : pakawa!
Msimulizi : hapo zamani za kale…………..

Semi
Ni tungi au kauli fupifupi za kisanaa zenye kubeba maana au mafunzo . kigezo kilichotumika kugawa utanzu huu ni kigezo cha lugha ambacho ni lugha ya mkato na kigezo cha kidhima ambacho hufunza mfano methali, vitendawili, misimu, mafumbo, lakabu, missemo na nahau.
Ushairi
Ni utungo unaojumuisha tungo zote zenye kutumia mapigo kwa utaratibu maalumu. Mapigo ya kimziki, mathalani mapigo hayo yanaweza kupangwa kwa muala wa urari. Hivyo basi ushairi huweza kuwa wa namna tofautitofauti kama vile nyimbo, maghani na ngonjera. Katika vipera hivi zinakusudiwa ni zile zinazotungwa kwa mdomo( bila maandishi) na kusambazwa kwa mdomo.

Sanaa za maonyesho
Katika kudadavua zana ya sanaa ya maonyesho ni vema kujua dhana ya sanaa ya yenyewe. Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa; umbo ambalo mtu hulitimia kuelezea hisia zinazo mgusa kwa kutolea kielelezo/vielezo vyenye dhana maalumu. sana  za maonyesho ni sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza katika umbo ambalo linaweza kuifadhiwa na uzuri wake huonyeshwa wakati wote. Sanaa hizo ni kama vile uchorai, utalizi, ufinyanzi na uchongaji.
Hivyo basi sanaa za maonyesho  hujumuisha vipera kama vile majigambo, tambiko, miviga, ngoma, utani, ngonjera, vichekesho, michezo ya jukwaani ya watoto.


MAREJELEO
Mulokozi, M.M. (1996). Utangulizi wa Fasihi Simulizi ya Kiswahili. TUKI. Dar es Salaam.
Mulokozi,M.M. (1989).Tanzu za fasihi simulizi.Mulika.21:1-24.Dar-es-salaam.
TUKI, (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. (Toleo la Pili). East Africa: Oxford University Press  
       na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI).
 Wamitila, K.W. (2003). Kamusi ya Fasihi, Istilahi na Nadharia. Focus Publications Ltd.  

            Nairobi.
Wamitila,K W (2003) Kichocheo cha fasihi simulizi: Focus Publications Ltd.  

            Nairobi

10 comments:

  1. asante sana nimeelwa sana ndugu

    ReplyDelete
  2. Aina mbili za masimulizi ni zipi katika fasihi simulizi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aina za masimulizi ni
      1.Masimulizi ya kihistoria
      2.Masimulizi ya kubuni

      Delete
  3. Nimependa Sana hii mmefafanua Vizur

    ReplyDelete
  4. Unaweza kulinganisha na kulinganua kazi zozote mbili za kifasihi za tanzu tofauti kwa kumulika vipengele viwili vya fani.Pengine unaweza kunisaidia kuelewa zaidi

    ReplyDelete

Powered by Blogger.

Wasiliana nami papo kwa papo

Name

Email *

Message *

Ads 468x60px

Breaking News

Top Featured

Featured Posts

Sample text

Sample Text

Recomended

Facebook

Advertise

Most Popular

Connect With Us

Followers

Social Icons

Pages

Pages

BTricks

Pages

Popular posts

Tafuta chochote ukiwa hapahapa

Kategori

Recent Comments

You can replace this text by going to "Layout" and then "Page Elements" section. Edit " About "

recent posts

Video Of Day

TRANSLATE

Instructions

Video

Flickr Images

FURAHIA UWEPO WAKO HAPA

Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

Imetembelewa mara

TAKWIMU ZA WATEMBELEAJI

Popular Posts

SAJIRI

Definition List

premium-wordpress-themes.org