21 Sept 2019



SWALI:  
Neno na sentensi ni vipashio vikuu katika sarufi mapokeo. Eleza kinaganaga aina ya maneno na sentensi kwa mujibu wa sarufi hiyo.


Sarufi mapokeo
Kwa mujibu wa Khamisi na Kiango (2002), sarufi mapokeo ni sarufi ya kale, wataalamu wanaohusishwa na mkabala huu walijitokeza kuanzia karne ya 5 Kabla ya Kristo na katka karne ya 18 na 19 Baada ya Kristo, wataalamu hao ni kama Plato, Aristotle, Panin na Protagoras ambao walijihusisha na lugha kwa kutaka kujua asili yake ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa asili ya maumbo, hususani walitaka kujua asili yake ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa asili ya maumbo, hususani walitaka kujua kama lugha ni tukio la kimaumbile au tukio la unasibu.
Massamba na wenzake (2009) wanaeleza kwamba sarufi mapokeo zilikuwa ni sarufi elekezi ambazo zilisisitiza kanuni na nini cha kusema na wajua lugha. Watu wasiojua kanuni za lugha wanapaswa kujifunza kutoka kwa wanaojua sarufi ya lugha. Wanaendelea kusema kuwa wanaojua lugha hupaswa kutunga kanuni za sarufi.
Waasisi wa sarufi mapokeo walikuwa ni wanafalsafa wa Ugiriki. Katika kipindi hiki sarufiilshughulikiwa sambamba na falsafa, dini, fasihi, balagha na mantiki. Waasisi hao ni Plato na mwanfunzi wake Aristotle (Matinde, (2012).
Kwa mujibu wa sarufi mapokeo ni kweli kwamba neno na sentensi ndivyo vipashio vikuu katika sarufi mapokeo. Vipashio hivi (neno na sentensi) vimefafanuliwa kwa undani na wanasarufi mapokeo kama tutakavyoona hapa chini.
Aina ya sentensi kwa mujibu wa sarufi mapokeo
Sentensi ni fungu la maneno lenye uarifishaji mkamilifu. Sentensi huwa na muundo uliokamilika na hujitegemea kimaana (Matinde, 2012). Pia Massamba na wenzake (2009:136), wanasema sentensi ni kipashio kikubwa kabisa cha kimiundo chenye maana kamili. Miundo ya sentensi huhusisha vipashio vingine vidogo kimiundo.
Kwa mujibu wa Matinde (2012:211), tunaarifiwa kwamba Plato aligawa sentensi katika sehemu kuu mbili: Mtenda (Subject) na Kitendwa (Object). Pia Massamba na Wenzake (2009:52) katika SAMIKISA wanaongeza kwamba uchambuzi huo ulizingatia zaidi uamilifu (kazi) wa faridi au vipashio mbali mbali katika tungo au sentensi.
Kwa mfano, sentensi “Mama anapika chakula” aliigawa sentensi hii kama ifuatavyo:
Mama
anapika chakula
Mtenda (Subject)
Kitendwa (Object)

Kwa mujibu wa Habwe na Karanja (2004:142) wanasema wanasarufi mapokeo waliainisha sentensi kwa mujibu wa uamilifu wake. Na baadhi ya makundi ya uainishaji yaliyojitokeza ni kama yafuatayo:
Sentensi taarifa (arifu)
Matinde (2012:160), anafafanua kuwa “sentensi arifu ni sentensi ambazo hutoa taarifa au ujumbe fulani.” Sentensi za aina hii huishia kwa kituo kikuu/nukta. Mifano ya sentensi arifu:
v  Baba amenunua kitabu.
v  John anaimba vizuri.
Sentensi agizi (amrishi): Hizi ni sentensi ambazo huamrisha au humwagiza msikilizaji kutenda kitendo/jambo fulani. Sentensi hizi huundwa na kitenzi cha kuamuru. Aghalabu sentensi hizi huwa na sehemu ya kitendwa (kiarifu) tu. Sentensi hizi huishia na kituo kikuu au mshangao (Matinde, 2012:160). Kwa mfano:
v  Leta hiyo sahani.
v  Nenda kapige kelele huko nje.
Sentensi ulizi (swalifu): Sentensi hizi huwa zina pengo katika sehemu yake ya taarifa. Hivyo hutaka kupata taarifa Fulani. Hizi ni sentensi ambazo uamilifu wake ni kuuliza swali. Sentensi swalifu huishia kwa alama ya kuuliza (?). Kwa mfano:
v  Mwanao ana umri gani kwa sasa?
v  Ndama amepotea lini?

Matinde (2012:161) ameongeza aina za sentensi zifuatazo kwa kuzingatia kigezo cha uamilifu wake ambazo ni hizi zifuatazo:
Sentensi mshangao
Matinde (2012:161) anasema sentensi mshangao ni sentensi ambazo hudhihirisha mshangao wa msemaji kuhusu jambo au hali fulani. Sentensi hizi huishia kwa alama ya mshangao. Mifano:
v  Juma amefeli!
v  Chakula kimeshapikwa!
Sentensi shurutia
Kwa mujibu wa Matinde (2012:161) anaeleza kuwa sentensi shurutia ni sentensi za masharti ambazo huundwa na vitenzi viwili. Kitenzi cha kwanza hukamilishwa na kitenzi cha pili ili kuonesha uhusiano wa masharti. Vitenzi hivi huambikwa viambishi vya masharti mathalani: -nge, -ngali, -ngeli, na -ki. Viambishi hivi ni nguzo ya sentensi shurutia. Kwa mfano:
v  Juma angelisoma kwa bidii angelifaulu mtihani
v  Jane angaliimba angalipata zawadi
Aina za maneno kwa mujibu wa sarufi mapokeo
Baada ya kuwa tumeona namna sarufi mapokeo ilivyoshughulikia suala la sentensi kwa kuigawa katika sehemu kuu mbili yaani kiima (Mtenda) na kiarifu (Kitendwa) na sasa tuone namna wanasarufi mapokeo walivyojishughulisha na maneno na aina zake kama kipashio kingine cha msingi kwa mujibu wa kigezo hiki. Massamba na wenzake (2009:54) wanasema aina za maneno zilikuwa ni nomino, Kitendo (Kitenzi), sifa (kivumishi), advebo (kielezi) n.k. (maneno yaliyowekwa kwenye mabano ni istilahi za siku hizi).
Kwa mujibu wa Matinde (2012:211-212) anaeleza kuwa mara baada ya Plato kugawa sentensi kugawa sentensi katika sehemu kuu mbili mtenda (Subject) na kitendwa (Object), Aristotle aliweza kwenda mbali zaidi ya kazi ya mwalimu wake Plato kwa kugawa sentensi katika sehemu kuu tano, ambazo ni; Nomino, Kitenzi, Kivumishi, Kiunganishi, na Kielezi.
Matinde (2012:212) anaendelea kueleza kuwa miaka 100 Kabla ya Kristo mwanasarufi Myunani Dionysus Thrax aliandika kitabu cha sarufi cha awali kabisa ambacho kiliitwa Techne Grammatike (The art of Grammar). Dionysus Thrax aliainisha sehemu saba za sentensi ambazo ni; Nomino, Kitenzi, Kivumishi, Kiwakilishi, Kiunganishi, kielezi, na  Kiingizi.
Pia Habwe na Karanja (2004:131) wanasema wanasarufi mapokeo waliainisha maneno kutokana na kazi ambazo maneno hufanya katika uundaji wa sentensi. Maneno haya yameainishwa katika makundi tofauti kulingana na maana na utendaji kazi wake. Uainishji wa awali wa aina hii ulifanywa na wanasarufi mapokeo ambao walitambua aina mabalimbali za maneno walizoziita kategoria za maneno.
Baadhi ya kategoria walizotambua ni: Nomino, Vitenzi, Viwakilishi, Vivumishi, Vielezi, Vihusishi, Viunganishi, Vihisishi, Vionyeshi, Vibainishi na kadhalika.   
Nomino: Kwa mujibu wa sarufi mapokeo ni neno la kutaja vitu- yaani ni majina ya vitu. Hivyo majina nomino hutaja majina ya vitu, watu, hali, mahali, vyeo, na dhana. Baadhi ya wanasarufi huita nomino majina. Mifano ya nomino ni kama vile Tanzania, Utundu, Mtoto, Kisu, Malaika na nyinginezo.
Mfano: Baba analima
Viwakilishi: Ni maneno ambalo hutumiwa kusimama badala ya nomino katika sentensi. Viwakilishi pia hujulikana kwa jina la pronomino. Mifano ya viwakilishi; Wapi unaenda?  Neno wapi ni kiwakilishi kiulizi, aina nyingine ya viwakilishi ni viwakilishi nafsi, viwakilishi vimilikishi, viwakilishi vya idadi, viwakilishi vya jumla na kadhalika.
Vivumishi: Vivumishi hueleza habari ya kitu au mtu kikionyesha jinsi mtu au kitu kilivyo. Kisintaksia kivumishi ni neno linalotoa sifa ya neno au kifungu cha maneno, aghalabu nomino na viwakilishi vyake.
Mifano;  Mzee mrefu amewahi.
               Kitabu kizuri kimepotea.
Vitenzi: Ni maneno ambayo huwakilisha kitendo.Mbaadu (1985) anaeleza kuwa vitenzi kama maneno yoyote yanayoonyesha mambo yanayofanywa na watu, wanyama, au vitu katika wakati fulani. Pia vitenzi hueleza hali Fulani za watu, vitu, na matukio. Vitenzi ni kama vile imba, cheza, lima, sema, soma na kadhalika.
Mfano; Mama analima shamba.
              Watoto wanaimba nyimbo zao vizuri.
Vielezi: Ni maneno au fungu la maneno ambalo huongeza maana ya kitendo. Ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi, na vielezi vingine.  Mifano ya vielezi ni kama vile sasa hivi, ovyo ovyo, asubuhi na mapema.
Mfano; Mwanafunzi ameondoka sasa hivi.
             Jack anacheza vizuri.
Vihusishi: Ni neno aukundi la maneno yanayohusisha sehemu mbili au zaidi za sentensi. Huonesha uhusiano baina ya kitu na kingine au mtu na mwingine kama wahusika katika sentensi. Mifano ya vihusishi ni maneno kama vile katika, juu ya, kwa, hadi na kadhalika.
Mfano; Omari anacheza juu ya kitanda.
              Mtoto anakula kwa kijiko.
Viunganishi
Ni maneno ambayo huunganisha maneno au mafungu ya maneno. Viunganishi huweza kuunganisha maneno na maneno, au maneno na vikundi vya maneno na vikundi vingine vya maneno. Mifano ya maneno ambayo ni viunganishi ni kama vile na, kisha, na kadhalika.
Mfano; Juma na Ali wanasoma. (Neno kwa neno). 
             Ali alikwenda maktaba kisha akasoma jarida. (kishazi na kishazi)

Vionyeshi
Kwa mujibu wa Kapinga (1983) vionyeshi ni maneno yanayoonyesha ujirani wa kitu kwa kukihusisha na kitu kingine. Vionyeshi pia vimerejelewa kama viashiria. Mifano ya vionyeshi ni kama huyu, wale, hao na vinginevyo.
Mfano; Wale wanakuja.
              Hao ni wazuri.
Vihisishi: Ni aina ya maneno ambayo huonyesha hisia kama vile hali ya kufurahi, uchungu, kushangaa, kushtuka na kadhalika. Awali vilijulikana kama vishangao lakini hii haikutosheleza jukumu la vihisishi kwa sababu vishangao ni aina moja tu ya vihisishi yaani vile vinavyoonyesha mshangao tu. Mifano ya vihisishi ni kama alhamdulillahi!, Mungu wangu! Ebo! Simile! Lahaula! na vinginevyo.
Mfano wa kihisishi; Mungu wangu! Amepotea?
Vibainishi: Kategoria hii haipokatika lugha ya Kiswahili. Huweza kupatikana katika baadhi ya lugha ikiwemo lugha ya kiingereza. Vibainishi hutumiwa pamoja na nomino.
Kwa mfano: The student ate all the food,   An elephant is a wild animal.
                   A book is a good thing to have.
Hivyo ndivyo ambavyo wanasarufi mapokeo walivyoweza kuainisha maneno na sentensi ambavyo ndivyo vipashio vya msingi vya lugha kwa kuzingatia kigezo hiki cha sarufi mapokeo. Kikubwa ni kwamba wao katika uainishaji wao waliegemea zaidi uamilifu wa tungo hizo yaani kazi ambazo maneno na sentensi hufanya.




MAREJELEO
Habwe, J. & Karanja, P. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd
Khamis, A. M. & Kiango, J. G. (2002). Uchambuzi wa Sarufi ya Kiswahili. Dar es salaam:
                  TUKI.
 Massamba, D. P. B. na wenzake (2009). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA):
                   Sekondari na Vyuo. Dar es salaam: TUKI.
Matinde , R. S. (2012). Dafina ya lugha isimu na nadharia: Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na
                   Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti educational publishers

0 maoni:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Wasiliana nami papo kwa papo

Name

Email *

Message *

Ads 468x60px

Breaking News

Top Featured

Featured Posts

Sample text

Sample Text

Recomended

Facebook

Advertise

Most Popular

Connect With Us

Followers

Social Icons

Pages

Pages

BTricks

Pages

Popular posts

Tafuta chochote ukiwa hapahapa

Kategori

Recent Comments

You can replace this text by going to "Layout" and then "Page Elements" section. Edit " About "

recent posts

Video Of Day

TRANSLATE

Instructions

Video

Flickr Images

FURAHIA UWEPO WAKO HAPA

Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

Imetembelewa mara

TAKWIMU ZA WATEMBELEAJI

Popular Posts

SAJIRI

Definition List

premium-wordpress-themes.org