14 Jul 2025

 

Kusikiliza mazungumzo

Dhana ya mazungumzo.

Mazungumzo ni utaratibu ni maelezoya mdomo kwa lugha ya kawaida kuhusu suala lolote mbili au zaidi ambapo kwa kawaida kwa kawaida wahusikawa mazungumzo hayo huwa ni watu .Mazungumzo yanapofanyika huwakutanisha mzungumzaji na msikilizaji ,msikilizaji huelewa vizuri mazungumzo kutokana na kusikilizakwa makini. Mazungumzoau habari anayosomewa au kusimuliwa msikilizaji huhitaji umakini .Habari inaweza kusimuliwa ana kwa ana au kutoka kwenye televisheni ,redio ,komyuta au simu ya mkononi.

Mambo ya kuzingatia katika kusikiliza mazungumzo

Ili kuelewa vizuri mazungumzoau habari anayosikiliza,msikilizaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo,

·        Awe makini kusikiliza kinachosimuliwa au kusomwa

·        Abainishe mambo muhimu yanayoelezwa katika mazungumzo anayosikiliza.

·        Msikilizaji amtazame usoni mzungumzaji iliaweze kupata taarifa za ziada ambazo mzungumzaji anawe za kuzitoa kwa kutumia ishara za mwili.

·        Msikilizaji awe makini na sarufi ya lugha inayozungumzwa na lafudhi ya mzungumzajia anaweza kuzitoa kwa kutumia ishara za mwili

·        Msikilizaji awe makini na sarufi ya lugha inayozungumzwa na lafudhi ya mzungumzaji

·        Msikilizaji awe katika eneo lenye utulivu kuepuka kelele zinazoweza kufanya asisikie vyema .

 

 

Sifa za lugha ya mazungumzo.

Lugha ya mazungumzo huwa na sifa kadhaa kama ifuatavyo;

·        Mzungumzaji na msikilizaji kupeana nafasi wakati wa mazungumzo ili wweze kuelewana

·        Kutumia lugha ya mkato kwalengo la kurahisisha mawasiliano na kuokoa muda

·        Huwa na utaratibu wa kurudiana kwa maneno au sentensi kwa lengo la kusisitiza au kufafanua  jambo zaidi

·        Huwa na matumizi ya lugha ya vionjo kwalengo la kupamba lugha . mfano, matumizi ya semi.

·        Huhusiha stadi kuu mbili  za lugha ambazo ni kuzungumza na kusikiliza kwa wakati mmoja.

·        Hutumia lugha ya ishara na mijongeo ya viungo ya mwili .Mtu anapomzungumza huwezakucheka kutikisa mabega ,kuguna,kuweka mkono usoni,kutikisa kichwa kuashiria kukubali au kukataa jambo.

·        Mzungumzaji au msemaji au msikilizaji wote kwa pamoja hutakiwa kuzingatia ufasaha wa maneno yanayotolewa

Kusikiliza mazungumzo changamani.

Mazungumzochangamani ni mazungumzo yale yanayohusu masuala muhimu yanayozungumziwa katika mazungumzo.katika kusikiliza mazungumzo changamani, msikiliza anatakiwa awe na kalamu na karatasi,kompyuta,simu au tablet kwa ajili ya kuandika mambo hayo muhimu kutoka kwenye habari anayoisikiliza.ikumbukwe kuwa mazungumzo changamani ni yale mazungumzo marefu ambayo yanahitaji msikilizaji awe makini kuchambua ni kusikiliza mambo muhimu. Mfano wa mazungumzo changamani ni hotuba za viongozi , kampeni za siasa, risala na mazungumzo mengine yenye mada mchanganyiko,

 

Kufupisha mazungumzo changamani.

Ufupisho ni taaluma inayohusu upunguaji wa maneno katika habari au mazungumzo kwa kuzingatia maudhui ya habari au mazungumzo husika . upunguzaji huo huyaondoa au kuyajumuisha maneneo yenye dhana moja bila kuathiri ujumbe uliokusudiwa katika kufupisha mazungumzo changamani ,unapaswa kuzingatia yafuatayo ;

·        Kufupisha mazungumzo yawe mafupi kuliko ya mwanzo

·        Kubakiza maana ileile katika mazungumzo uliyofupisha,usiondoe maneno ya msingi

·        Kuwa na mtiririko mzuri wa mazungumzo yako nay awe na mantiki

·        Tumia maneno yako mwenyewe

·        Zingatia kutokpunguza ujumbe wa mazungumzo

·        Tafuta maneno mengine yanayoweza kutumika badala ya fungu Fulani la maneno. Kwa mfano “kaka wa mama yangu ni mgonjwa” inaweza kuwa mjomba ni mgonjwa.

Hatua za kufuata katika kufupisha mazungumzo changamani

l   Sikiliza mazungumzo au habari yote kwa makini

l   Bainisha mawazo makuu kutoka kwenye habari au mazungumzo uliyoyasikiliza

l   Mazungumzo au habari uliyoisikiliza ina lugha fasaha na mtiririko mzuri wa mawazo

l   Hakikisha hujapunguza ujumbe wa mazungumzo

l   Husianisha mazungumzo muhimu na mazungumzo ya awali kama yanaendana.

 

 

 

Kushiriki katika majadiliano ya muktadha mbalimbali.

Majadiliano ni kitendo cha kupeana mawazo chanya baina ya watu au pande mbili au zaidi ili kufikia muafaka wenye manufaa kuhusu suala au jambo fulani.

Mara nyingi majadiliano hufanywa kwenye kikundi cha watu wawili au zaidi ili kutatua jambo au kuonngeza ujuzi wa jambo Fulani. Kwa mfano:majadiliano kuhusu umuhimu wa elimu .

Majadiliano huwa na mada moja au zaidi . Aidha, majadiliano yanaweza kuwa rasmi au yasiyo rasmi . majadiliano rasmi huzingatia mazingira rasmi na majadiliano yasiyo rasmi hufanyika katika mazingira yasiyo rasmi mfano kijiweni,nyumbani au barabarani

Taratibu na sifa za majadiliano

·        Huhusisha pande mbili yaani wazungumzaji na wasikilizaji kwa wakati mmoja

·        Huwa  na washiriki wawili au zaidi

·        Huwa  na hoja au mada imayojadiliwa

·        Huandaliwa katika mazingira rasmi au yasiyo rasmi

·        Huhusisha utamkaji sahihi na matumizi ya Kiswahili fasaha

·        Huhitaji utamkaji sahihi na matumizi ya Kiswahili fasaha

·        Huhitaji usikivu mkubwa ili kuweza kuchangia hoja.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Zoezi la Marudio

 

1.  Chagua jibu sahihi katika maswali yafuatayo

i)   Malezo ya mdomo  kwa lugha ya kawaida kuhusu jambo lolote huitwaje?

A.Majadiliano 

B.Mazungumzo  

C.Mawasiliano   

D.Ushirikiano

E.Makubaliano

 

ii)  Ipi kati ya seti zifuatazo si sifa ya mazungumzo?

A.  Haifanyiki bila kuzingatia aina za maneno

B.  Kupeana nafasi wakati wa mazungumzo

C.  Kuna matumizi ya vionjo vya mwili

D. Hutumia lugha ya mkato ili kurahisisha mawasiliano

E.  Hawana urudiaji wa maneno au sentensi ili kusisitiza

 

iii)  Zipi ni pande mbili zinazohusisha mazungumzo?

A.  Mzungumzaji ma msemaji

B.  Msemaji na msikilizaji

C.  Msilikilizaji na msemaji

D. Mzungumzaji na msikilizaji

E.  Msikilizaji na Msomaji

iv)  Unaelewa nini kuhusu mazungumzo changamani?

A.  Mazungumzo ya watu wakubwa

B.  Mazungumzo yahusuyo masuala muhimu

C.  Mazungumzo yahusuyo familia tu

D. Mazungumzo yaliyopitwa na wakati

E.  Mazungumzo yanayotumia lugha ya ishara.

v)    Taaluma inayohusu upunguzaji wa maneno katika habari au mazungumzo kwa kuzingatia maudhui ya habari au mazungumzo husika huitwaje?

A.  Mazungumzo changamani

B.  Ufupisho

C.  Majadiliano

D. Mkazo

E.  Ufahamu

 

2.  Oanisha maana ya dhana katika Orodha A na dhana zinahusika kutoka Orodha B kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.

ORODHA A

ORODHA B

    i.        Redio,televisheni,kompyuta,simu ya mkononi na kinasa sauti

A.  Kupunga,kukunja uso, kucheka

  ii.        Kueleza jambo kwa maneno machache

B.  Vifaa vinavyoweza kutumika katika maasiliano ya mzangumzo

iii.        Ishara zitumikazo katika mazungumzo

C.  Mzungumzaji na msikilizaji

 iv.        Mazungumzo huhusisha pande mbili

D. Ufupisho

   v.        Hutambulisha jamii Fulani

E.  Lafudhi

 

F.  Mkazo

 

G. Lugha ya mazungumzo

 

3.  Eleza mambo matano (5) yanayoweza kukusaidia kuelewa unaposikiliza mazungumzo

4.  Fanya majadiliano na wenzako darasani kuhusu chanzo cha mmomonyoko wa maadili kwa vijana na kupendekeza nini kifanyike ili kuondoa hali hiyo . Kisha, andika ufupisho na mjadala huo kwenye daftari lako kwa maneno yasiyozidi 150

5.  Sikiliza kifungu cha habari kifuatacho kinachosomwa na mwenzako, kisha kifupishe kwa sentensi zisizozidi tano(5)

Maendeleo ya Kiswahili nchini ni ya kutia moyo Lugha hii sasa imeingia katika uwanja wa sayansi na teknolojia . Huu ni wakati muhimu sana katika maendeleo ya lugha hii . kwanza ni wakati ambapo kunahitajika kuwapo na mikakati kabambe yenye upeo wa mbali ya kuendeleza lugha hii kitaaluma. Sayansi na teknolojia ni uwanja wa taaluma . Pili, tunahitajika kutumia utaalamu wa hali ya juu katika kuijenga lugha hii ili iweze kubeba mahitaji katika mazingira hayo. Bila hiyo hatuwezi kusonga mbele.

6.  Fafanua sifa za lugha ya mazungumzo na taratibu za majadiliano

7.  Unapata ujumbe gani unaposikiliza wimbo wa Taifa la Tanzania unakimbwa

8.  Fafanua sifa tano za majadiliano

9.  Andika tofauti tano kati ya mazungumzo na majadiliano

10.Fafanua mambo matano(5) yanayoweza kusababish msikilizaji asiweze kuelewa anachosikiliza.

 

 

Kusoma kwa Ufasaha na Ufahamu

Kusoma kwa ufasaha  ni kusoma matini kwa usahihi kwa kuzingatia taratibu za uandishi. Mambo ya kuzingatia  katika kusoma kwa ufasaha.

a)     Matamshi sahihi ya maneno.

b)     Alama za uandishi

c)     Kasi stahiki

d)     Mtiririko wa aya

e)     Utamkaji sahihi wa silabi zenye mkazo na kiimbo katika maneno ilikupata maana sahihi

Kusoma kwa Ufahamu

Kusoma kwa ufahamu ni uwezo wa kusoma na kuelewa jambo fulani liliandikwa. mtu anaweza kupata ufahamu kutokana na kusoma kifungu cha habari, makala, kitabu au gazeti.

Mambo ya kuzingatia katika kusoma kwa ufahamu

a)     Kusoma matini kwa sauti au kimya

b)     Kurudia kusoma matini  hiyo kwa makini na kubainisha mambo ya              msingi yaliyomo katika matini hayo.

c)     Kuwa makini katika kutafakari jambo alilolisoma ili aweze kutoa taarifa iliyo sahihi au kujibu maswali kwa usahihi.

d)     Msomaji anatakiwa kufahamu matini anayoisoma inahusu nini

e)     Msomaji anatakiwa  kubaini maneno mapya yaliyotumika katika matini aliyoisoma na namna yalivyotumika ili kutambua lengo  la mwandishi.

Umuhimu wa kusoma  kwa ufasaha  na ufahamu

a)     Huwezesha kukuza uelewa wa mambo mbalimbali na stadi za kuzungumza na kuandika

b)     Kukuza uwezo  wa kujenga hoja juu ya mambo mbalimbali na kujieleza  kwa ufasaha na kwa ufupi.

c)     Hukuza uwezo wa kuchambua mambo anuai na kuchochea ari ya kujisomea.

 

Dhana ya ufahamu.

Ufahamu ni neno linalotokana na neno kufahamu. Kufahamu ni kuwa na taarifa sahihi na za kutosha juu ya jambo au tukio fulani kiasi cha kuweza kulifafanua kwa mtu mwingine naye akaelewa. Ni ile hali ya kujua na kuelewa jambo kwa undani na kuweza kulifafanua au kulitolea taarifa.

Tunaweza kupima kuwa mtu fulani ana ufahamu kutokana na uwezo wake wa kufafanua jambo Fulani kwa undani Zaidi. Ufahamu hutokana na kuona au kusikiliza.

Umuhimu wa ufahamu

Ufahamu ni kipengele muhimu sana katika taaluma ya lugha kwa sababu zifuatazo;

a)    Huwezesha kukuza uelewa wa mambo mbalimbali

b)    Husaidia kukuza uwezo wa kujenga hoja

c)    Husaidia uwezo wa kuchambua mambo

d)    Huchochea hali ya kujifunza mambo mbalimbali

e)    Husaidia kuwa na uwezo wa kujieleza kwa ufupi na kwa ufasaha

 

Dhima ya ufahamu.

Ufahamu una dhima mbalimbali katika Maisha ya kila siku. Miongoni mwa dhima hizo ni Pamoja na hizi zifuatazo;

a)   Huokoa muda kwa kutoa taarifa mbalimbali kwa muhtasari.

Kufahamu jambo kwa undani kunasaidia mtu kulielezea jambo hilo kwa muhtasari ili kuokoa muda tofauti na asiyefahamu jambo hilo ambaye anaweza kuelezea jambo hilo kwa muda mrefu.

 

b)  Kuelimisha.

Mtu anaposoma habari fulani akaielewa bila shaka huelimika kutokana na alichokisoma. Hujipatia elimu na maarifa yaliyomo katika kifungu hicho. Kwa mfano kusimulia mwenzake hadithi aliyosoma au tukio aliloliona kunaweza kumfanya abadilike.

 

c)   Huokoa gharama

Mtu anayefahamu jambo lakini akaweza kulielezea jambo hilo kwa ufupi bila shaka huokoa gharama. Kwa mfano unaweza kuandika barua kwa kutumia karatasi moja tu badala ya kutoa maelezo mengi katika karatasi mbili au tatu.

 

d)  Hukuza lugha

Msomaji anaposoma habari humjenga na kujiongezea maneno au msamiati mpya wakati mwingine ambao hujawahi kuusikia au kuutumia.

 

e)   Huongeza maarifa

Kusoma vitabu ni Zaidi ya kusafiri na kwenda nchi ambayo hujawahi kufika. Ndani ya maandishi kuna ushauri, kuna Faraja na maarifa mbalimbali ambayo yanatokana na uzoefu wa Maisha ya mwandishi.

 

 

Aina za ufahamu

Kuna aina tatu za ufahamu, yaani ufahamu wa kuona, kusikiliza na kusoma. Aina y ufahamu hutegemea njia aitumiayo mtu kupata taarifa.

 

a)   Ufahamu wa kuona

Ni aina ya ufahamu unaohusu kutazama vitu au matukio na kuyatafakari kwa lengo la kupata ujumbe. Ufahamu huu huhusisha namna mtu anavyoweza kutazama matukio mbalimbali kisha kuweza kusimulia matukio hayo kwa wengine. Mfano, mtu aliyetazama mchezo wa mpira wa miguu uwanja wa Taifa kisha kuwasimulia wenzake.

 

b)    Ufahamu wa kusikiliza

Ni aina ya ufahamu ambao mtu anapaswa kupata taarifa kwa kusikiliza habari anayosomewa au anayosimoliwa kwa mdomo au kutoka kwenye kifaa cha kurekodia, redio, kompyuta, simu ya mkononi, televisheni au njia ya mtandao. Ni aina ya ufahamu ambao mtu husikiliza jambo linaloelezewa na mtu mwingine ana kwa ana au njia zilizotajwa hapo juu. Katika aina hii ya ufahamu kunahitajika uwepo wa fanani (msimuliaji au msomaji) na hadhira (msikilizaji)

Mambo ya kuzingatia katika ufahamu wa kusikiliza

a)     kuwa makini kwa kile kinachosimuliwa au kusomwa

b)    kuhusisha mambo muhimu na habari inayosimuliwa

c)     kujua matamshi ya mzungumzaji

d)    kubaini mawazo makuu

e)     kuelekeza mawazo kwenye kile kinachosikilizwa

f)      msikilizaji kuwa katika hali ya utulivu

g)     kuangalia ishara ya mzungumzaji au msikilizaji

h)    kumtazama usoni yule anayesimulia kama ni mtu

i)      kutambua matamshi ya mzungumzaji au msikilizaji.

 

a)     Ufahamu wa kusoma

Ufahamu wa kusoma ni uelewa unaopatikana kwa njia ya kusoma habari iliyo katika maadishi mfano magazeti, vitabu, majarida, vipeperushi, barua n.k.

Ufahamu wa kusoma hujitokeza katika aina tatu kama ifuatavyo;

(i)          Kusoma kwa sauti

(ii)        Kusoma kwa haraka na kimya

(iii)      Kusoma kwa makini

 

(i)          Kusoma kwa sauti

Kusoma kwa sauti ni aina ya usomaji ambao humwezesha msomaji kupata ujumbe na kuweza kutamka kwa  lafudhi ya Kiswahili sahihi. Kusoma kwa sauti humfanya msomaji ajisikilize na kujipima uwezo wake wa kutamka maneno kwa usahihi. Pia hupima kasi aliyonayo na uwezo wa kuelewa yale ayasomayo. Ni muhimu msomaji azingatie matamshi sahihi ya lugha ilia pate maana sahihi ya maandishi yenyewe. Kwa mfano msomaji akishindwa kutofautisha kati ya baada na badala, kuwakilisha na kuwasilisha huweza kuibua dhana tofauti na aliyokusudia mwanzo.

 

Mambo ya kuzingatia katika ufahamu wa kusoma kwa sauti

(a) Kutoa sauti ya kutosha wakati wa kusoma

(b)Kuzingatia alama za uandishi

(c) Kutamka maneno kwa usahihi

(d)Kusikiliza hoja kwa kutumia mkazo na kiimbo

(e) Kuzingatia kanuni za lugha husika kama vile matamshi

 

(ii)        Ufahamu wa kusoma kimya

Ufahamu wa kusoma kwa kimya ni ufahamu wa kusoma habari pasipo kutamka maneno kwa sauti inayosikika. Msomaji hupitisha macho kwa kwa haraka katika kila mstari wa maandishi akiwa amefumba kinywa chake. Usomaji wa aina hii hutumika sana maktaba sehemu ambako watu hawaruhusiwi kujadiliana wala kuongea. Ni aina ya usomaji Rafiki kwa watu wanaojiandaa kwa mitihani.

 

(iii)     Ufahamu wa kusoma kwa makini

Ufahamu wa kusoma kwa makini ni aina ya usomaji ambao msomaji huvuta fikra aina hii ya ufahamu.

 

Aina ya maswali ya ufahamu

Ili kujua kwamba kilichosomwa kimeeleweka msomaji hupewa maswali akijibu kwa urahisi huonesha kuwa ameelewa na akijibu vibaya huonesha kuwa hakuelewa.

Zipo aina mbili za maswali yanayoulizwa mara kwa mara kutokana na habari ya ufahamu. Aina hihi ni zifuatazo:

 

(a) Maswali mafupi

Ni aina ya maswali yanayohiaji majibu mafupi mafupi. Maswali hayo ni kama vile:

 

(i)          Maswali ya ndiyo kwa sentensi zilizo zilizo sahihi na hapana kwa sentensi zisizo sahihi. Wakati mwingine maswali haya huliza kama ni kweli kwa sentensi zilizo sahihi na si kweli kwa sentensi zisizo sahihi.

(ii)        Maswali ya kuchagua jibu lililo sahihi kutoka kwenye orodha ya majibu.

(iii)      Maswali ya kukamilisha majibu kwenye sehemu zilizoachwa wazi

(iv)       Maswali ya kuoainisha neno au kifungu kimoja na neno au kifungu kingine ili kuleta maana iliyo sahihi

 

(b) Maswali marefu

Ni aina ya maswali ambayo yanamhitaji msomaji afafanue jibu kwa kutumia busara yake. Maswali ya aina hii humtaka msomaji atoe Ushahidi au uthibitisho wa mawazo yake juu ya kile anachojibu.

Mbinu za kujibu maswali yatokanayo na habari.

a)  Kuvuta makini na kusikiliza bila kuruhusu kuingiliwa na mawazo mengine.

b)    Kusikiliza au kusoma habari yote kwa makini

c)    Kusikiliza au kusoma kila swali kwa makini

d)    Kutafakari kila swali, yaani kutafuta maana ya swali kwa kulihusisha na matini.

e)    Kujibu kila swali kwa kifupi na kwa usahihi.

Dhana ya ufupisho wa habari

Ufupisho wa habari ni kitendo au hali ya kupunguza maelezo ya habari ndefu uliyopewa na kuifanya kuwa fupi bila kupoteza maana yake ya msingi au maana ya awali. Jukumu la kubainisha mawazo makuu katika kifungu cha habari humwongoza msomaji katika kuandaa ufupisho wa habari aliyoisoma. Kwa kawaida maneno yakifupishwa hutakiwa kubaki theluthi moja (1/3) ya habari ya awali.

Hatua za kufuata katika ufupisho

(i)          Soma habari yote kwa makini mpaka uielewe.

(ii)        Chagua taarifa na maneno maalumu.

(iii)      Linganisha taarifa muhimu na habari ya awali.

(iv)       Andika muhtasari kama inavyotakiwa.

(v)         Linganisha usawa wa ufupisho na habari ya awali . kwa kawaida habari iliyofupishwa huwa ni theluthi moja (1/3) ya habari ya awali

(vi)       Andika idadi ya maneno unayotakiwa uandike iwapo utaelekezwa kufanya hivyo.

(vii)     Andika habari kwa lugha fasaha kwa mtiririko mzuri wa mawazo

(viii)   Zingatia taratibu za uandishi, mfano matumizi ya viafikishi na matumizi ya herufi kubwa na ndogo

Tanbihi  Ili kupata idadi ya maneno katika ufupisho, zipo njia mbili unaweza kuzitumia.

(a) Hesabu idadi ya maneno kwa kuhesabu neno au fungu moja moja mpaka mwisho.

(b)Hesabu idadi ya maneno kwenye mstari wa kwanza au mstari wowote uliokamilika kisha zidisha kwa idadi ya mistari iliyopo. Idadi ya maneno inaweza kuzidi maneno Matano au kupungua maneno kumi

Umuhimu wa ufupisho

(a) Hutumika katika kuandaa ripoti na kumbukumbu za vikao

(b)Husaidia wakati wa kuandaa shajala au kumbukumbu za kila siku

(c) Husaidia katika uhariri wa habari

(d)Husaidia kuokoa gharama hasa katika uandishi wa simu ya maandishi

(e) Husaidia kubainisha hoja kutokana na hadhara au hotuba.

Angalia mifano ya ufupisho

(i)          Kaka wa mama yangu amesafiri

Sentensi iliyofupishwa – mjomba wangu amesafiri

(ii)        Asha amekwenda sokoni kununua maembe, ndizi, machungwa, mananasi na mapapai.

Sentensi iliyofupishwa – Asha amekwenda sokoni kununua matunda

(iii)      Mama amenunua vijiko, sahani, vikombe, sufuria, sinia, ndoo, chujio na kisu

Sentensi iliyofupishwa – mama amenunua vyombo vya ndani.

 

 

 

Zoezi la marudio  la 5

1.  Chagua jibu sahihi katika maswali  yafuatayo :

i)            Dhana ya kusoma kwa ufahamu hufasiliwaje?

A.  Kusoma, kufikiri na kuelewa  jambo au vitu.

B.  Kuona, kusikiliza, na kutafakari

C.  Kuwa makini katika kutafakari

D. Kusoma, kusikiliza na kuona

E.  Kufikiri, kusoma na kuona

 

ii)          Alama za uandishi, matamshi sahihi ya maneno na kasi stahiki katika usomaji husaidia nini kwa msomaji?

A.  Kujenga hoja

B.  Kuchochea ari ya kusoma

C.  Kuelewa kile kinachozungumzwa

D. Kupenda kusoma

E.  Kujibu maswali

 

iii)        Adela anatikisa chupa ya dawa ya kikohozi kabla ya kunywa. Unafikiri kwa nini Adela  anafanya hivyo ?

A.   Alisoma ila hakuelwa  maelezo ya dawa

B.   Alisoma na alielewa maelezo ya dawa

C.   Hakusoma ila alielewa maelezo ya dawa

D.   Hakusoma wala kuelewa maelezo ya dawa

E.   Alisoma maelezo ya dawa.

 

iv)         Mambo yapi  kati ya yafuatayo  huzingatiwa katika kusoma kwa ufahamu na ufasaha?

A.   Kuzingatia matamshi sahihi,  alama za uandishi na kubainisha  mambo ya msingi.

B.   Kuchochea ari ya kujisomea, kubaini maneno mapya na kuchambua mambo ya msingi

C.   Kujenga hoja, kujieleza kwa ufasaha na kuchambua mambo anuai.

D.   Kukuza uelewa  wa mambo  mbalimbali , kubaini maneno mapya na kuchochea ari ya kujisomea.

E.   Kubaini Mawazo makuu, kuelewa maneno  anayoyasikia na viimbo na kujieleza kwa ufasaha.

 

v)           Ni kwa namna gani unaweza kuelewa lengo la mzungumzaji katika mazungumzo ?

A.   Kwa kuzingatia matamshi sahihi ya maneno

B.   Kwa kutumia alama sahihi za uandishi

C.   Kwa kusikiliza kiimbo cha mzungumzaji

D.   Kwa kutumia maneno maalum

E.   Kwa kuangalia msamiati .

 

2.  Oanisha maelezo yaliyopo katika Orodha A na dhana zilizopo katika Orodha B kwa  kuchagua herufi ya jibu sahihi .

 

Orodha  A

Orodha   B

i)            Kuzingatia habari na kubainisha Mawazo makuu na kuyaelewa.

ii)           

iii)        Nukta, mkato,  ritifaa,  mshangao, kiulizo, nukta pacha.

 

iv)         Msomaji hufumba kinywa na kupitisha  macho kwenye maandishi

 

v)           Kuimarisha ujuzi wa kutamka kwa kufuata kanuni na lafudhi ya Kiswahili.

 

vi)         Kuimarisha ujuzi wa kutamka kwa kufuata kanuni na lafudhi ya Kiswahili.

 

vii)       Kuandika kwa muhtasri kwa kuzingatia Mawazo makuu katika Habari. 

A.  Kusoma kwa sauti

 

B.  Kusoma kimyakimya

 

C.  Ufupisho

 

D. Alama za uandishi

 

E.  Mambo makuu ya kuzingatia katika ufahamu .

 

F.  Ufahamu

 

G. Kuchambua  maandishi

 

 


3.  Mtu anaweza kupata ufahamu kuhusu masuala mbalimbali kwa njia gani ?

 

4.  Bainisha ujanzo mbalimbali  wa taarifa na maarifa kuhusu masuala ya jamii kiuchumi, kiteknolojia na kidiplomasia.

 

5.  Kwa nini kusoma kwa ufahamu ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku ?

 

 

Powered by Blogger.

Wasiliana nami papo kwa papo

Name

Email *

Message *

Ads 468x60px

Breaking News

Top Featured

Featured Posts

Sample text

Sample Text

Recomended

Facebook

Advertise

Most Popular

Connect With Us

Followers

Social Icons

Pages

Pages

BTricks

Pages

Popular posts

Tafuta chochote ukiwa hapahapa

Kategori

Recent Comments

You can replace this text by going to "Layout" and then "Page Elements" section. Edit " About "

recent posts

Video Of Day

TRANSLATE

Instructions

Video

Flickr Images

FURAHIA UWEPO WAKO HAPA

Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

Imetembelewa mara

NUMBER OF VIEWERS

Popular Posts

SAJIRI

Definition List

premium-wordpress-themes.org