Kusoma kwa Ufasaha na Ufahamu
Kusoma kwa ufasaha ni kusoma matini kwa usahihi kwa kuzingatia
taratibu za uandishi. Mambo ya kuzingatia
katika kusoma kwa ufasaha.
a)
Matamshi sahihi ya maneno.
b)
Alama za uandishi
c)
Kasi stahiki
d)
Mtiririko wa aya
e)
Utamkaji sahihi wa silabi zenye
mkazo na kiimbo katika maneno ilikupata maana sahihi
Kusoma kwa Ufahamu
Kusoma kwa ufahamu ni uwezo wa kusoma
na kuelewa jambo fulani liliandikwa. mtu anaweza kupata ufahamu kutokana na
kusoma kifungu cha habari, makala, kitabu au gazeti.
Mambo ya kuzingatia katika kusoma kwa
ufahamu
a)
Kusoma matini kwa sauti au kimya
b)
Kurudia kusoma matini hiyo kwa makini na kubainisha mambo ya msingi yaliyomo katika matini hayo.
c)
Kuwa makini katika kutafakari jambo
alilolisoma ili aweze kutoa taarifa iliyo sahihi au kujibu maswali kwa usahihi.
d)
Msomaji anatakiwa kufahamu matini
anayoisoma inahusu nini
e)
Msomaji anatakiwa kubaini maneno mapya yaliyotumika katika
matini aliyoisoma na namna yalivyotumika ili kutambua lengo la mwandishi.
Umuhimu wa kusoma kwa ufasaha
na ufahamu
a)
Huwezesha kukuza uelewa wa mambo
mbalimbali na stadi za kuzungumza na kuandika
b)
Kukuza uwezo wa kujenga hoja juu ya mambo mbalimbali na
kujieleza kwa ufasaha na kwa ufupi.
c)
Hukuza uwezo wa kuchambua mambo anuai
na kuchochea ari ya kujisomea.
Dhana
ya ufahamu.
Ufahamu
ni neno linalotokana na neno kufahamu. Kufahamu ni kuwa na taarifa sahihi na za
kutosha juu ya jambo au tukio fulani kiasi cha kuweza kulifafanua kwa mtu
mwingine naye akaelewa. Ni ile hali ya kujua na kuelewa jambo kwa undani na
kuweza kulifafanua au kulitolea taarifa.
Tunaweza
kupima kuwa mtu fulani ana ufahamu kutokana na uwezo wake wa kufafanua jambo
Fulani kwa undani Zaidi. Ufahamu hutokana na kuona au kusikiliza.
Umuhimu
wa ufahamu
Ufahamu
ni kipengele muhimu sana katika taaluma ya lugha kwa sababu zifuatazo;
a)
Huwezesha kukuza uelewa wa mambo
mbalimbali
b)
Husaidia kukuza uwezo wa kujenga hoja
c)
Husaidia uwezo wa kuchambua mambo
d)
Huchochea hali ya kujifunza mambo
mbalimbali
e)
Husaidia kuwa na uwezo wa kujieleza
kwa ufupi na kwa ufasaha
Dhima
ya ufahamu.
Ufahamu
una dhima mbalimbali katika Maisha ya kila siku. Miongoni mwa dhima hizo ni
Pamoja na hizi zifuatazo;
a)
Huokoa muda kwa kutoa taarifa
mbalimbali kwa muhtasari.
Kufahamu jambo kwa undani kunasaidia mtu kulielezea jambo
hilo kwa muhtasari ili kuokoa muda tofauti na asiyefahamu jambo hilo ambaye
anaweza kuelezea jambo hilo kwa muda mrefu.
b) Kuelimisha.
Mtu anaposoma habari fulani akaielewa bila shaka huelimika
kutokana na alichokisoma. Hujipatia elimu na maarifa yaliyomo katika kifungu
hicho. Kwa mfano kusimulia mwenzake hadithi aliyosoma au tukio aliloliona
kunaweza kumfanya abadilike.
c)
Huokoa gharama
Mtu anayefahamu jambo lakini akaweza kulielezea jambo hilo
kwa ufupi bila shaka huokoa gharama. Kwa mfano unaweza kuandika barua kwa
kutumia karatasi moja tu badala ya kutoa maelezo mengi katika karatasi mbili au
tatu.
d) Hukuza
lugha
Msomaji anaposoma habari humjenga na kujiongezea maneno au
msamiati mpya wakati mwingine ambao hujawahi kuusikia au kuutumia.
e)
Huongeza maarifa
Kusoma vitabu ni Zaidi ya kusafiri na kwenda nchi ambayo
hujawahi kufika. Ndani ya maandishi kuna ushauri, kuna Faraja na maarifa
mbalimbali ambayo yanatokana na uzoefu wa Maisha ya mwandishi.
Aina za ufahamu
Kuna aina tatu za ufahamu, yaani ufahamu wa kuona,
kusikiliza na kusoma. Aina y ufahamu hutegemea njia aitumiayo mtu kupata
taarifa.
a)
Ufahamu wa kuona
Ni aina
ya ufahamu unaohusu kutazama vitu au matukio na kuyatafakari kwa lengo la
kupata ujumbe. Ufahamu huu huhusisha namna mtu anavyoweza kutazama matukio
mbalimbali kisha kuweza kusimulia matukio hayo kwa wengine. Mfano, mtu
aliyetazama mchezo wa mpira wa miguu uwanja wa Taifa kisha kuwasimulia wenzake.
b)
Ufahamu wa kusikiliza
Ni aina ya ufahamu ambao mtu anapaswa kupata taarifa kwa kusikiliza habari anayosomewa au anayosimoliwa kwa mdomo au kutoka kwenye kifaa cha kurekodia, redio, kompyuta, simu ya mkononi, televisheni au njia ya mtandao. Ni aina ya ufahamu ambao mtu husikiliza jambo linaloelezewa na mtu mwingine ana kwa ana au njia zilizotajwa hapo juu. Katika aina hii ya ufahamu kunahitajika uwepo wa fanani (msimuliaji au msomaji) na hadhira (msikilizaji)
Mambo ya
kuzingatia katika ufahamu wa kusikiliza
a)
kuwa makini kwa kile kinachosimuliwa
au kusomwa
b)
kuhusisha mambo muhimu na habari
inayosimuliwa
c)
kujua matamshi ya mzungumzaji
d)
kubaini mawazo makuu
e)
kuelekeza mawazo kwenye kile
kinachosikilizwa
f)
msikilizaji kuwa katika hali ya
utulivu
g)
kuangalia ishara ya mzungumzaji au
msikilizaji
h)
kumtazama usoni yule anayesimulia
kama ni mtu
i)
kutambua matamshi ya mzungumzaji au
msikilizaji.
a)
Ufahamu wa kusoma
Ufahamu
wa kusoma ni uelewa unaopatikana kwa njia ya kusoma habari iliyo katika
maadishi mfano magazeti, vitabu, majarida, vipeperushi, barua n.k.
Ufahamu
wa kusoma hujitokeza katika aina tatu kama ifuatavyo;
(i)
Kusoma kwa sauti
(ii)
Kusoma kwa haraka na kimya
(iii)
Kusoma kwa makini
(i)
Kusoma kwa sauti
Kusoma kwa sauti ni aina ya usomaji
ambao humwezesha msomaji kupata ujumbe na kuweza kutamka kwa lafudhi ya Kiswahili sahihi. Kusoma kwa sauti
humfanya msomaji ajisikilize na kujipima uwezo wake wa kutamka maneno kwa
usahihi. Pia hupima kasi aliyonayo na uwezo wa kuelewa yale ayasomayo. Ni
muhimu msomaji azingatie matamshi sahihi ya lugha ilia pate maana sahihi ya
maandishi yenyewe. Kwa mfano msomaji akishindwa kutofautisha kati ya baada na
badala, kuwakilisha na kuwasilisha huweza kuibua dhana tofauti na aliyokusudia
mwanzo.
Mambo
ya kuzingatia katika ufahamu wa kusoma kwa sauti
(a) Kutoa
sauti ya kutosha wakati wa kusoma
(b)Kuzingatia alama za uandishi
(c) Kutamka
maneno kwa usahihi
(d)Kusikiliza hoja kwa kutumia mkazo na
kiimbo
(e) Kuzingatia
kanuni za lugha husika kama vile matamshi
(ii)
Ufahamu wa kusoma kimya
Ufahamu
wa kusoma kwa kimya ni ufahamu wa kusoma habari pasipo kutamka maneno kwa sauti
inayosikika. Msomaji hupitisha macho kwa kwa haraka katika kila mstari wa
maandishi akiwa amefumba kinywa chake. Usomaji wa aina hii hutumika sana
maktaba sehemu ambako watu hawaruhusiwi kujadiliana wala kuongea. Ni aina ya
usomaji Rafiki kwa watu wanaojiandaa kwa mitihani.
(iii)
Ufahamu wa kusoma kwa makini
Ufahamu
wa kusoma kwa makini ni aina ya usomaji ambao msomaji huvuta fikra aina hii ya
ufahamu.
Aina ya
maswali ya ufahamu
Ili
kujua kwamba kilichosomwa kimeeleweka msomaji hupewa maswali akijibu kwa
urahisi huonesha kuwa ameelewa na akijibu vibaya huonesha kuwa hakuelewa.
Zipo
aina mbili za maswali yanayoulizwa mara kwa mara kutokana na habari ya ufahamu.
Aina hihi ni zifuatazo:
(a) Maswali
mafupi
Ni aina
ya maswali yanayohiaji majibu mafupi mafupi. Maswali hayo ni kama vile:
(i)
Maswali ya ndiyo kwa sentensi
zilizo zilizo sahihi na hapana kwa sentensi zisizo sahihi. Wakati
mwingine maswali haya huliza kama ni kweli kwa sentensi zilizo sahihi na
si kweli kwa sentensi zisizo sahihi.
(ii)
Maswali ya kuchagua jibu lililo
sahihi kutoka kwenye orodha ya majibu.
(iii)
Maswali ya kukamilisha majibu kwenye
sehemu zilizoachwa wazi
(iv)
Maswali ya kuoainisha neno au kifungu
kimoja na neno au kifungu kingine ili kuleta maana iliyo sahihi
(b) Maswali marefu
Ni aina ya maswali ambayo yanamhitaji
msomaji afafanue jibu kwa kutumia busara yake. Maswali ya aina hii humtaka
msomaji atoe Ushahidi au uthibitisho wa mawazo yake juu ya kile anachojibu.
Mbinu za kujibu maswali yatokanayo na
habari.
a) Kuvuta
makini na kusikiliza bila kuruhusu kuingiliwa na mawazo mengine.
b)
Kusikiliza au kusoma habari yote kwa
makini
c)
Kusikiliza au kusoma kila swali kwa
makini
d)
Kutafakari kila swali, yaani kutafuta
maana ya swali kwa kulihusisha na matini.
e)
Kujibu kila swali kwa kifupi na kwa
usahihi.
Dhana ya ufupisho wa habari
Ufupisho
wa habari ni kitendo au hali ya kupunguza maelezo ya habari ndefu uliyopewa na
kuifanya kuwa fupi bila kupoteza maana yake ya msingi au maana ya awali. Jukumu
la kubainisha mawazo makuu katika kifungu cha habari humwongoza msomaji katika
kuandaa ufupisho wa habari aliyoisoma. Kwa kawaida maneno yakifupishwa hutakiwa
kubaki theluthi moja (1/3) ya habari ya awali.
Hatua za kufuata katika ufupisho
(i)
Soma habari yote kwa makini mpaka uielewe.
(ii)
Chagua taarifa na maneno maalumu.
(iii)
Linganisha taarifa muhimu na habari
ya awali.
(iv)
Andika muhtasari kama inavyotakiwa.
(v)
Linganisha usawa wa ufupisho na
habari ya awali . kwa kawaida habari iliyofupishwa huwa ni theluthi moja (1/3)
ya habari ya awali
(vi)
Andika idadi ya maneno unayotakiwa
uandike iwapo utaelekezwa kufanya hivyo.
(vii)
Andika habari kwa lugha fasaha kwa
mtiririko mzuri wa mawazo
(viii)
Zingatia taratibu za uandishi,
mfano matumizi ya viafikishi na matumizi ya herufi kubwa na ndogo
Tanbihi Ili kupata idadi ya maneno katika ufupisho, zipo njia
mbili unaweza kuzitumia.
(a) Hesabu
idadi ya maneno kwa kuhesabu neno au fungu moja moja mpaka mwisho.
(b)Hesabu idadi ya maneno kwenye mstari
wa kwanza au mstari wowote uliokamilika kisha zidisha kwa idadi ya mistari
iliyopo. Idadi ya maneno inaweza kuzidi maneno Matano au kupungua maneno kumi
Umuhimu
wa ufupisho
(a) Hutumika
katika kuandaa ripoti na kumbukumbu za vikao
(b)Husaidia wakati wa kuandaa shajala au
kumbukumbu za kila siku
(c) Husaidia
katika uhariri wa habari
(d)Husaidia kuokoa gharama hasa katika
uandishi wa simu ya maandishi
(e) Husaidia
kubainisha hoja kutokana na hadhara au hotuba.
Angalia
mifano ya ufupisho
(i)
Kaka wa mama yangu amesafiri
Sentensi
iliyofupishwa – mjomba wangu amesafiri
(ii)
Asha amekwenda sokoni kununua maembe,
ndizi, machungwa, mananasi na mapapai.
Sentensi
iliyofupishwa
– Asha amekwenda sokoni kununua matunda
(iii)
Mama amenunua vijiko, sahani,
vikombe, sufuria, sinia, ndoo, chujio na kisu
Sentensi iliyofupishwa – mama amenunua vyombo vya ndani.
Zoezi la marudio la 5
1. Chagua
jibu sahihi katika maswali yafuatayo :
i)
Dhana ya kusoma kwa ufahamu
hufasiliwaje?
A. Kusoma,
kufikiri na kuelewa jambo au vitu.
B. Kuona,
kusikiliza, na kutafakari
C. Kuwa
makini katika kutafakari
D. Kusoma,
kusikiliza na kuona
E. Kufikiri,
kusoma na kuona
ii)
Alama za uandishi, matamshi sahihi ya
maneno na kasi stahiki katika usomaji husaidia nini kwa msomaji?
A. Kujenga
hoja
B. Kuchochea
ari ya kusoma
C. Kuelewa
kile kinachozungumzwa
D. Kupenda
kusoma
E. Kujibu
maswali
iii)
Adela anatikisa chupa ya dawa ya
kikohozi kabla ya kunywa. Unafikiri kwa nini Adela anafanya hivyo ?
A.
Alisoma ila hakuelwa maelezo ya dawa
B.
Alisoma na alielewa maelezo ya dawa
C.
Hakusoma ila alielewa maelezo ya dawa
D.
Hakusoma wala kuelewa maelezo ya dawa
E.
Alisoma maelezo ya dawa.
iv)
Mambo yapi kati ya yafuatayo huzingatiwa katika kusoma kwa ufahamu na
ufasaha?
A.
Kuzingatia matamshi sahihi, alama za uandishi na kubainisha mambo ya msingi.
B.
Kuchochea ari ya kujisomea, kubaini
maneno mapya na kuchambua mambo ya msingi
C.
Kujenga hoja, kujieleza kwa ufasaha
na kuchambua mambo anuai.
D.
Kukuza uelewa wa mambo
mbalimbali , kubaini maneno mapya na kuchochea ari ya kujisomea.
E.
Kubaini Mawazo makuu, kuelewa
maneno anayoyasikia na viimbo na
kujieleza kwa ufasaha.
v)
Ni kwa namna gani unaweza kuelewa
lengo la mzungumzaji katika mazungumzo ?
A.
Kwa kuzingatia matamshi sahihi ya
maneno
B.
Kwa kutumia alama sahihi za uandishi
C.
Kwa kusikiliza kiimbo cha mzungumzaji
D.
Kwa kutumia maneno maalum
E.
Kwa kuangalia msamiati .
2. Oanisha
maelezo yaliyopo katika Orodha A na dhana zilizopo katika Orodha B kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi .
Orodha A |
Orodha B |
i)
Kuzingatia habari na kubainisha Mawazo makuu na
kuyaelewa. ii)
iii)
Nukta, mkato,
ritifaa, mshangao, kiulizo,
nukta pacha. iv)
Msomaji hufumba kinywa na kupitisha macho kwenye maandishi v)
Kuimarisha ujuzi wa kutamka kwa kufuata kanuni na
lafudhi ya Kiswahili. vi)
Kuimarisha ujuzi wa kutamka kwa kufuata kanuni na
lafudhi ya Kiswahili. vii) Kuandika kwa muhtasri kwa
kuzingatia Mawazo makuu katika Habari.
|
A. Kusoma kwa sauti B. Kusoma kimyakimya C. Ufupisho D. Alama za uandishi E. Mambo makuu ya kuzingatia katika ufahamu
. F. Ufahamu G. Kuchambua maandishi |
3. Mtu
anaweza kupata ufahamu kuhusu masuala mbalimbali kwa njia gani ?
4. Bainisha
ujanzo mbalimbali wa taarifa na maarifa
kuhusu masuala ya jamii kiuchumi, kiteknolojia na kidiplomasia.
5. Kwa
nini kusoma kwa ufahamu ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku ?
0 maoni:
Post a Comment