14 Jul 2025

 

Kusikiliza mazungumzo

Dhana ya mazungumzo.

Mazungumzo ni utaratibu ni maelezoya mdomo kwa lugha ya kawaida kuhusu suala lolote mbili au zaidi ambapo kwa kawaida kwa kawaida wahusikawa mazungumzo hayo huwa ni watu .Mazungumzo yanapofanyika huwakutanisha mzungumzaji na msikilizaji ,msikilizaji huelewa vizuri mazungumzo kutokana na kusikilizakwa makini. Mazungumzoau habari anayosomewa au kusimuliwa msikilizaji huhitaji umakini .Habari inaweza kusimuliwa ana kwa ana au kutoka kwenye televisheni ,redio ,komyuta au simu ya mkononi.

Mambo ya kuzingatia katika kusikiliza mazungumzo

Ili kuelewa vizuri mazungumzoau habari anayosikiliza,msikilizaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo,

·        Awe makini kusikiliza kinachosimuliwa au kusomwa

·        Abainishe mambo muhimu yanayoelezwa katika mazungumzo anayosikiliza.

·        Msikilizaji amtazame usoni mzungumzaji iliaweze kupata taarifa za ziada ambazo mzungumzaji anawe za kuzitoa kwa kutumia ishara za mwili.

·        Msikilizaji awe makini na sarufi ya lugha inayozungumzwa na lafudhi ya mzungumzajia anaweza kuzitoa kwa kutumia ishara za mwili

·        Msikilizaji awe makini na sarufi ya lugha inayozungumzwa na lafudhi ya mzungumzaji

·        Msikilizaji awe katika eneo lenye utulivu kuepuka kelele zinazoweza kufanya asisikie vyema .

 

 

Sifa za lugha ya mazungumzo.

Lugha ya mazungumzo huwa na sifa kadhaa kama ifuatavyo;

·        Mzungumzaji na msikilizaji kupeana nafasi wakati wa mazungumzo ili wweze kuelewana

·        Kutumia lugha ya mkato kwalengo la kurahisisha mawasiliano na kuokoa muda

·        Huwa na utaratibu wa kurudiana kwa maneno au sentensi kwa lengo la kusisitiza au kufafanua  jambo zaidi

·        Huwa na matumizi ya lugha ya vionjo kwalengo la kupamba lugha . mfano, matumizi ya semi.

·        Huhusiha stadi kuu mbili  za lugha ambazo ni kuzungumza na kusikiliza kwa wakati mmoja.

·        Hutumia lugha ya ishara na mijongeo ya viungo ya mwili .Mtu anapomzungumza huwezakucheka kutikisa mabega ,kuguna,kuweka mkono usoni,kutikisa kichwa kuashiria kukubali au kukataa jambo.

·        Mzungumzaji au msemaji au msikilizaji wote kwa pamoja hutakiwa kuzingatia ufasaha wa maneno yanayotolewa

Kusikiliza mazungumzo changamani.

Mazungumzochangamani ni mazungumzo yale yanayohusu masuala muhimu yanayozungumziwa katika mazungumzo.katika kusikiliza mazungumzo changamani, msikiliza anatakiwa awe na kalamu na karatasi,kompyuta,simu au tablet kwa ajili ya kuandika mambo hayo muhimu kutoka kwenye habari anayoisikiliza.ikumbukwe kuwa mazungumzo changamani ni yale mazungumzo marefu ambayo yanahitaji msikilizaji awe makini kuchambua ni kusikiliza mambo muhimu. Mfano wa mazungumzo changamani ni hotuba za viongozi , kampeni za siasa, risala na mazungumzo mengine yenye mada mchanganyiko,

 

Kufupisha mazungumzo changamani.

Ufupisho ni taaluma inayohusu upunguaji wa maneno katika habari au mazungumzo kwa kuzingatia maudhui ya habari au mazungumzo husika . upunguzaji huo huyaondoa au kuyajumuisha maneneo yenye dhana moja bila kuathiri ujumbe uliokusudiwa katika kufupisha mazungumzo changamani ,unapaswa kuzingatia yafuatayo ;

·        Kufupisha mazungumzo yawe mafupi kuliko ya mwanzo

·        Kubakiza maana ileile katika mazungumzo uliyofupisha,usiondoe maneno ya msingi

·        Kuwa na mtiririko mzuri wa mazungumzo yako nay awe na mantiki

·        Tumia maneno yako mwenyewe

·        Zingatia kutokpunguza ujumbe wa mazungumzo

·        Tafuta maneno mengine yanayoweza kutumika badala ya fungu Fulani la maneno. Kwa mfano “kaka wa mama yangu ni mgonjwa” inaweza kuwa mjomba ni mgonjwa.

Hatua za kufuata katika kufupisha mazungumzo changamani

l   Sikiliza mazungumzo au habari yote kwa makini

l   Bainisha mawazo makuu kutoka kwenye habari au mazungumzo uliyoyasikiliza

l   Mazungumzo au habari uliyoisikiliza ina lugha fasaha na mtiririko mzuri wa mawazo

l   Hakikisha hujapunguza ujumbe wa mazungumzo

l   Husianisha mazungumzo muhimu na mazungumzo ya awali kama yanaendana.

 

 

 

Kushiriki katika majadiliano ya muktadha mbalimbali.

Majadiliano ni kitendo cha kupeana mawazo chanya baina ya watu au pande mbili au zaidi ili kufikia muafaka wenye manufaa kuhusu suala au jambo fulani.

Mara nyingi majadiliano hufanywa kwenye kikundi cha watu wawili au zaidi ili kutatua jambo au kuonngeza ujuzi wa jambo Fulani. Kwa mfano:majadiliano kuhusu umuhimu wa elimu .

Majadiliano huwa na mada moja au zaidi . Aidha, majadiliano yanaweza kuwa rasmi au yasiyo rasmi . majadiliano rasmi huzingatia mazingira rasmi na majadiliano yasiyo rasmi hufanyika katika mazingira yasiyo rasmi mfano kijiweni,nyumbani au barabarani

Taratibu na sifa za majadiliano

·        Huhusisha pande mbili yaani wazungumzaji na wasikilizaji kwa wakati mmoja

·        Huwa  na washiriki wawili au zaidi

·        Huwa  na hoja au mada imayojadiliwa

·        Huandaliwa katika mazingira rasmi au yasiyo rasmi

·        Huhusisha utamkaji sahihi na matumizi ya Kiswahili fasaha

·        Huhitaji utamkaji sahihi na matumizi ya Kiswahili fasaha

·        Huhitaji usikivu mkubwa ili kuweza kuchangia hoja.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Zoezi la Marudio

 

1.  Chagua jibu sahihi katika maswali yafuatayo

i)   Malezo ya mdomo  kwa lugha ya kawaida kuhusu jambo lolote huitwaje?

A.Majadiliano 

B.Mazungumzo  

C.Mawasiliano   

D.Ushirikiano

E.Makubaliano

 

ii)  Ipi kati ya seti zifuatazo si sifa ya mazungumzo?

A.  Haifanyiki bila kuzingatia aina za maneno

B.  Kupeana nafasi wakati wa mazungumzo

C.  Kuna matumizi ya vionjo vya mwili

D. Hutumia lugha ya mkato ili kurahisisha mawasiliano

E.  Hawana urudiaji wa maneno au sentensi ili kusisitiza

 

iii)  Zipi ni pande mbili zinazohusisha mazungumzo?

A.  Mzungumzaji ma msemaji

B.  Msemaji na msikilizaji

C.  Msilikilizaji na msemaji

D. Mzungumzaji na msikilizaji

E.  Msikilizaji na Msomaji

iv)  Unaelewa nini kuhusu mazungumzo changamani?

A.  Mazungumzo ya watu wakubwa

B.  Mazungumzo yahusuyo masuala muhimu

C.  Mazungumzo yahusuyo familia tu

D. Mazungumzo yaliyopitwa na wakati

E.  Mazungumzo yanayotumia lugha ya ishara.

v)    Taaluma inayohusu upunguzaji wa maneno katika habari au mazungumzo kwa kuzingatia maudhui ya habari au mazungumzo husika huitwaje?

A.  Mazungumzo changamani

B.  Ufupisho

C.  Majadiliano

D. Mkazo

E.  Ufahamu

 

2.  Oanisha maana ya dhana katika Orodha A na dhana zinahusika kutoka Orodha B kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.

ORODHA A

ORODHA B

    i.        Redio,televisheni,kompyuta,simu ya mkononi na kinasa sauti

A.  Kupunga,kukunja uso, kucheka

  ii.        Kueleza jambo kwa maneno machache

B.  Vifaa vinavyoweza kutumika katika maasiliano ya mzangumzo

iii.        Ishara zitumikazo katika mazungumzo

C.  Mzungumzaji na msikilizaji

 iv.        Mazungumzo huhusisha pande mbili

D. Ufupisho

   v.        Hutambulisha jamii Fulani

E.  Lafudhi

 

F.  Mkazo

 

G. Lugha ya mazungumzo

 

3.  Eleza mambo matano (5) yanayoweza kukusaidia kuelewa unaposikiliza mazungumzo

4.  Fanya majadiliano na wenzako darasani kuhusu chanzo cha mmomonyoko wa maadili kwa vijana na kupendekeza nini kifanyike ili kuondoa hali hiyo . Kisha, andika ufupisho na mjadala huo kwenye daftari lako kwa maneno yasiyozidi 150

5.  Sikiliza kifungu cha habari kifuatacho kinachosomwa na mwenzako, kisha kifupishe kwa sentensi zisizozidi tano(5)

Maendeleo ya Kiswahili nchini ni ya kutia moyo Lugha hii sasa imeingia katika uwanja wa sayansi na teknolojia . Huu ni wakati muhimu sana katika maendeleo ya lugha hii . kwanza ni wakati ambapo kunahitajika kuwapo na mikakati kabambe yenye upeo wa mbali ya kuendeleza lugha hii kitaaluma. Sayansi na teknolojia ni uwanja wa taaluma . Pili, tunahitajika kutumia utaalamu wa hali ya juu katika kuijenga lugha hii ili iweze kubeba mahitaji katika mazingira hayo. Bila hiyo hatuwezi kusonga mbele.

6.  Fafanua sifa za lugha ya mazungumzo na taratibu za majadiliano

7.  Unapata ujumbe gani unaposikiliza wimbo wa Taifa la Tanzania unakimbwa

8.  Fafanua sifa tano za majadiliano

9.  Andika tofauti tano kati ya mazungumzo na majadiliano

10.Fafanua mambo matano(5) yanayoweza kusababish msikilizaji asiweze kuelewa anachosikiliza.

 

0 maoni:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Wasiliana nami papo kwa papo

Name

Email *

Message *

Ads 468x60px

Breaking News

Top Featured

Featured Posts

Sample text

Sample Text

Recomended

Facebook

Advertise

Most Popular

Connect With Us

Followers

Social Icons

Pages

Pages

BTricks

Pages

Popular posts

Tafuta chochote ukiwa hapahapa

Kategori

Recent Comments

You can replace this text by going to "Layout" and then "Page Elements" section. Edit " About "

recent posts

Video Of Day

TRANSLATE

Instructions

Video

Flickr Images

FURAHIA UWEPO WAKO HAPA

Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

Imetembelewa mara

NUMBER OF VIEWERS

Popular Posts

SAJIRI

Definition List

premium-wordpress-themes.org