Lugha
na Utamaduni
Dhana
ya Lugha
Binadamu
huwasiliana kwa kutumia lugha. Lugha ndicho chombo kikuu cha mawasiliano ya
binadamu. Lugha ni miongoni mwa vitambulisho vya utamaduni wa jamii fulani.
Jamii hutumia lugha kusalimiana, kupashana habari na kubadilisha mawazo.
Ushirikiano baina ya mtu na mtu hutokana na matumizi ya lugha
Kwa ujumla tunaweza kufasili lugha kwa kusema Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu za kusemwa zenye maana zilizokubaliwa na jamii
ya watu ili ziweze kutumika katika mawasiliano yao.
Ni
muhimu kutambua kuwa lugha ni kwa ajili ya binadamu na wala si kwa wanyama.
Wanyama, wadudu na ndege huweza kuwasiliana miongoni mwao lakini hawana lugha.
Maana(fasili) ya lugha inapotajwa mambo yafuatayo
huzingatiwa;
(i)
Mfumo maalumu (mpangilio)
Lugha lazima iwe na mpangilio maalumu ambao huanzia katika kiwango kidogo
kabisa hadi kufikia kiwango cha juu.
(ii)
Sauti za
nasibu (sauti za bahati tu), Mara nyingi hakuna uhusiano
wa moja kwa moja baina ya jina la kitu na kile kinachotajwa (kitu)pia hakuna
kikao maalum kilichokaa ili kuchagua maneno ya lugha husika na maana zake.
(iii)
Maana-
Lugha lazima iwe na maana kwa jamii inayoitumia
(iv)
Binadamu
(jamii) – Lugha ni mali ya binadamu, binadamu pekee ndiye hutumia lugha.
(v)
Mawasiliano
– Lugha ni chombo cha kupashana habari
Vipashio
vya lugha
Vipashio
vya lugha ni vipengele ambavyo kwa pamoja huijenga lugha. Lugha huundwa na
vipashio vikuu vinne ambavyo ni sauti, silabi, neno na sentensi.
(a)Sauti
Sauti
ni sehemu ndogo sana ya neno ambayo
haiwezi kugawanyika zaidi. Kila lugha ina vitamkwa (sauti) vyake. Sauti
zinazotumika katika lugha ya Kichina zinatofautiana na sauti zinazotumika
katika lugha nyingine kama vile Kiingereza, Kijerumani, Kiswahili na kadhalika.
Mfano a, b, c,d,e,f,gh,h,I,j,k,l,m,n,nk.
Sauti za lugha ya Kiswahili hugawanyika katika aina
mbili ambazo ni irabu na konsonanti.
(i)Irabu/vokali(I)
Irabu ni sauti ambazo wakati wa utamkaji wake huwa hakuna kizuizi katika
mkondo wa hewa utokao mapafuni na kupitia mdomoni. Kuna irabu tano za Kiswahili
ambazo ni a, e, i, o, u
(ii)Konsonanti(k)
Konsonanti ni sauti ambazo wakati wa utamkaji wake huwa na kizuizi katika
mkondo wa hewa utokao mapafuni na kupitia mdomoni.Kuna konsonanti kumi na
tisa(19) katika lugha ya kiswahili ambazo ni
b,ch,d,f,g,h,j,k,l,m,n,p,r,s,t,v,w,y na z
Katika lugha ya Kiswahili kwa mfano neno
“anacheza” limejengwa kwa vitamkwa a/n/a/ch/e/z/a. Vitamkwa au vipande- sauti
hivyo ndivyo vinavyounda maneno.
Kumbuka kwamba mawasiliano ya kutumia ishara
si lugha. Vilevile mawasiliano baina ya wanyama, ndege na wadudu hayawezi
kuitwa lugha kwa sababu vitamkwa vyake haviwezi kujulikana wala kuleta maana.
(b)Silabi
Silabi ni kipashio kidogo kinachojenga lugha
ambacho hutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Silabi
inapoungana na silabi nyingine huunda neno.
Miundo ya silabi
Silabi huweza kujitokeza katika miundo ifuatayo;
·
Irabu pekee(I)
Mfano; Oa, Ua.Hapa kuna silabi mbili kwa kila neno yaani o-a,u-a
·
Konsonanti
pekee(K)
Mfano;M-toto,M-kungu
·
Konsonanti na
irabu (KI)
Mfano; Baba, Karatasi.Hapa kuna
ba-ba,ka-ra-ta-si
·
Konsonanti,
konsonanti na irabu (KKI)
Mfano; Mwezi, Chafya.Hapa kuna
mwe-zi,cha-fya.
·
Konsonanti,
konsonanti, konsonanti na irabu (KKKI)
Mfano; mkwe, pendwa, Mchwa.Hapa
kuna m-kwe,pe-ndwa,m-chwa
Kumbuka kuwa silabi ni kipashio cha kimatamshi na hivyo hudhihirika katika
matamshi tu.Hivyo basi ili kujua neno lina silabi ngapi unapaswa kulitamka
kwanza;kila pigo(fungu) moja la sauti ni silabi moja.
(c)Neno
Neno ni kipashio kidogo kinachojenga lugha ambacho
hutokana na muunganiko wa silabi mbili au zaidi na unaoleta maana kamili.
Mfano; Mama, Lima, Cheza, Cheka.
(d)Sentensi.
Sentensi ni kipashio kikubwa kabisa kinachojenga
lugha ambacho kina muundo wa kiima na kiarifu na chenye kutoa taarifa kamili.
Sentensi huweza kuwa na neno moja au kikundi cha maneno kinachotoa taarifa
kamili.
Mfano;
Ninakuja.
Mama anapika.
Shangazi anashona kitenge.
Tafakuri
1. Kwa
nini mawasiliano ya wanyama, ndege na wadudu siyo lugha?
Jibu lako linaweza kuwa kama
ifuatavyo:
i)
Wanyama, ndege
na wadudu hawana lugha.
ii)
Lugha ni mali
ya binadamu kutokana na sauti zinavyopangiliwa vizuri hata kuleta maana
inayojitosheleza.
iii)
Kwa kuzingatia
sauti za wanyama tunaona kwamba ni sauti tu zinazoashiria kitu fulani.
iv)
Mnyama
anasikia sauti, anaweza pia akaelewa inaashiria nini.
Kazi 1.1
1. Soma
kifungu cha habari kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Maalufu
nchini mwandishi Tanzania Emmanuel Mihambo amejikita katika utunzi wa vitabu
vya mapenzi, vitabu ambavyo wanawake wengi Tanzania wa huvisoma muda yote.
Wengi hujikutaga wamerara usingizi wakivisoma. Ni kweri hivi vitabu ni motomoto
kwani ndani zake zina ujumbe mzito wenye wito wa kujenga hamani na umoja
nchini.
Umaalufu
wake mwandishi huyu umevuka mpaka badara ya kuandika kitabu chake cha “nani
nimuoe” na ile cha “Nauzika moyo wangu” kinachothimulia namna alivyowahi
kukutana na mlembo wa kitanga Tanzania huko.
Maswali
i)
Bainisha
maneno yenye makosa na uyaandika kwa usahihi
ii)
Kwa nini
mwandishi ametumia maneno maalufu, kweri, kurara, badara na thimulia?
iii)
Andika
sentensi tatu zenye makosa ya kisarufi yanayotokana na athari za mazingira.
2. Fafanua
tofauti ya irabu na konsonanti kwa mifano
3. Baada
ya Tobi kuzaliwa na mama yake alitupwa katika msitu mnene ambako kulikuwa na
sauti za ndege pamoja na wanyama wa mwituni. Akalelewa na nyani mpaka
alipofikisha miaka kumi na mitano. Unafikiri Tobi alikuwa akitumia lugha gani
baada ya kurejea nyumbani kwao?
Sifa za Lugha/nduni
za lugha
Lugha ina sifa mbalimbali ambazo huitofautisha na njia nyingine za mawasiliano.
(i)Lugha huzaliwa,hukua na hufa.
Lugha ina tabia ya uhai kwani huzaliwa kwa kuanza kutumi
wa na kikundi kidogo cha watu baadae hukua kwa
kupata
mashiko na kuenea kwenye eneo pana
zaidi na baadaye ina
weza kufa kwa kukosa watumiaji.
Dhima
za lugha katika mawasiliano
Lugha ina dhima(kazi) nyingi katika jamii. Baadhi
ya dhima hizi ni kama ifuatavyo:
(i)
Lugha
ni chombo cha mawasiliano
Lugha kama
chombo cha mawasiliano humwezesha binadamu kumpatia mwenzake mawazo mbalimbali.
Mawazo hayo humfikia binadamu kwa njia ya lugha. Lugha huwawezesha binadamu
kufahamiana na kuelewana. Kutokana na kuwasiliana huko umoja na ushirikiano
baina ya wazungumzaji huimarika sana. Watu wanaotumia lugha moja hujisikia kuwa
ni wamoja ukilinganisha na watu wanaotumia lugha tofauti.
(ii)
Lugha
ni chombo cha kuelimisha
Sehemu kubwa
ya maarifa anayoyapata binadamu hupitia katika lugha. Lugha inatumika kuelezea
mambo yanayofaa kufanywa na yale ambayo hayafai kufanywa katika jamii zetu.
Watoto wanaozaliwa hujifunza kwa kuyasikiliza yale yanayosemwa.
(iii) Lugha ni
kielelezo cha utamaduni wetu
Mila na
desturi na mienendo ya matukio mbalimbali katika jamii yanaenezwa na lugha. Kwa
mfano, Kisukuma kinasambaza utamaduni wa wasukuma yaani mila na destri na
mienendo yao katika matukio mbalimbali. Mfano wanawake kupiga magoti wakati wa
kusalimia au kuweka chakula watu wale. Hivyo hivyo Kiswahili hueneza utamaduni
wa watanzania.
(iv) Lugha husaidia
kuhifadhi ujuzi wa ulimwengu na kurithisha ujuzi huo kutoka kizazi hadi kizazi.
Hii ni
kutokana na Kiswahili kuenea katika mataifa mbalimbali duniani pamoja na nchi
zinazotumia lugha ya Kiswahili zikiwemo Kenya, Uganda, Kongo na Msumbiji.Hivyo
kupitia Kiswahili jamii inaweza kuhifadhi maarifa mbalimbali na kuyaeneza
kwenye vizazi vijavyo.
(v)
Lugha
ni chombo kinachoathiri mawazo
Mpangilio wa
mawazo hutegemea lugha. Mtu anayefahamu lugha fulani ana nafasi kubwa ya
kujieleza au kutoa mawazo yake popote akaeleweka kuliko yule asiyefahamu lugha
hiyo.
(vi) Lugha
hupatanisha au kufarakanisha
Lugha
hupatanisha kwani husaidia katika kutatua matatizo mbalimbali yaliyomo katika
jamii. Hata hivyo lugha inaweza kufarakanisha watu hasa pale unapotokea mgogoro
katika jamii na lugha ikashindwa kuutatua mgogoro huo.
(vii) Lugha
hutambulisha matabaka katika jamii
Katika
jamii moja unaweza kutofautisha wasomi na wasiosoma kupitia lugha.
Tanzu za Lugha
Tunaweza
kupanga tanzu za lugha katika tanzu mbili, nazo ni lugha ya mazungumzo na lugha
ya maandishi.
Lugha
ya mazungumzo ni lugha inayotolewa(kuwasilishwa) kwa njia ya mazungumzo ya
mdomo, ni sehemu ya mawasiliano ambayo hujumuisha mzungumzaji na msikilizaji
ambapo mzungumzaji huzungumza na msikilizaji husikiliza
Lugha
ya maandishi ni ile inayomwezesha mzungumzaji ajieleze kwa njia ya maandishi.
Hivyo, lugha ya maandishi humhusisha mwandishi na msomaji (fanani na hadhira).
Umuhimu wa lugha ya kiswahili
l
Lughga ya
kiswaili utumik kufundishia masomo yote katik shule ya msingi na vyuo vya kati.
Hii husaidia wanafunzi kuelewa zaidi kutokana na kujifunza kwa lugha rafiki.
l
Lugha ya
kiswahili huwaunganisha watu.Mfano Tanzania inazaidi ya makabila 120 lakini
makabila yote hunganishwa na lugha moja ya kiswhili katika mawasiliano yao.
l
Lugha ya
kiswahili ni lugha rasmi ambayo hutumika katika shughuli rasmi na muhimu katika
serikali.
l
Lugha ya
kiswahili ni nyenzo ya kutolea maarifa, ujuzi na taaluma mbalimbali
l
Lugha ya kiswahili hutoa fursa za ajira
kutokana na kiswahili kutumika nje ya nchi yetu, watanzania hupata fursa za
ajira mfano; kwenda kufundisha.
Hadhi ya lugha ya kiswahili kimataifa
l
Lugha ya kiswahili imepewa hadhi ya kutumika katika shughuli rasmi za
kimataifa
l
Lugha ya
kiswahili imeafanikiwa kwa kiwango kikubwa kuleta umoja katika bara la Afrika.
l
Kiswahili
kinatumika kama lugha rasmi katika jumuiya
ya maendeleo kusini mwa Afrika ( SADC )
na jumuiya ya Afrika mashariki
l
Lugha ya
kiswahili hutoa fursa za ajira kimataifa, mfano baadi ya
watannzania wenye taaluma ya kiswahili wanapopata ajira nje ya nchi
l
Lugha ya
kiswahili ndio lugha pekee inayotumika katika umoja wa Afrika Sanjari na lugha zingine za kimataifa
Zoezi
la kikundi
1. Lugha
hujengwa kwa vitamkwa, vifafanue vitamkwa hivyo kwa mifano.
Kazi
ya nyumbani
Binadamu wangeishi bila lugha nini kingetokea?
Orodhesha mambo matano ambayo yangetokea.
Nyanja
za Lugha
Lugha ya Kiswahili ina nyanja kuu mbili ambazo ni
sarufi na fasihi.
Fasihi
ni nyanja ya lugha ambayo hutumia maneno kwa njia ya kiufundi (kisanaa) ili
kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa.
Sarufi
ni kanuni na taratibu za lugha zinazofuatwa na wazungumzaji katika mawasiliano.
Hivyo sarufi ni kanuni au taratibu zinazotawala matumizi ya lugha.
Kwa hiyo sarufi ya lugha inaweza kugawanyika
katika sehemu zifuatazo:
(i)
Sarufi
matamshi (fonolojia) vitamkwa vya msingi
(ii)
Sarufi maumbo
(mofolojia) mpangilio wa vitamkwa
(iii)
Sarufi muundo
(sintaksia) mpangilio wa maneno
(iv)
Sarufi maana
(semantiki) upatikanaji wa maana.
Sarufi
matamshi (fonolojia)
Sarufi matamshi ni aina ya sarufi inayochunguza
namna neno linavyotamkwa. Matamshi ya binadamu yanakumbwa na matatizo kutokana
na sababu kuu mbili ambazo ni:
(i)
Athari ya
lugha mama
(ii)
Matatizo
katika mfumo sauti
Kuathirika huku husababisha kukosekana kwa baadhi
ya herufi.
Matatizo haya husababisha kukosekana kwa baadhi ya
maana ya moja kwa moja.
Utaratibu wa mpangilio wa vitamkwa vya msingi
vinavyojenga maneno hujitokeza katika lugha zote. Tawi hili la sarufi
hushughulikia vipande sauti vijengavyo maneno. Vipande sauti hivi ni vidogo
vidogo, hivyo haviwezekani kugawanywa zaidi vikaleta maana. Vipande sauti hivyo
vinaweza vikaleta tofauti katika maana ya maneno hasa vinapoathiriwa na lugha
nyingine.
Kwa mfano;
(i)
Niletee fiatu
fyangu – badala ya Niletee viatu vyangu.
(ii)
Wewe metenda
zambi – badala ya wewe umetenda dhambi
(iii)
Watoto
wamerara kitandani- badala ya Watoto wamelala kitandani
(iv)
Abbas Ibrahim
amenunua thamani za ndani – badala ya Abbas Ibrahim amenunua samani za ndani.
Sarufi
maumbo (mofolojia)
Ni sarufi inayohusika na namna maneno
yanavyoumbika. Huzingatia vipande sauti (vitamkwa) au vipashio vinavyounda
neno. Kila kipashio kina kazi yake katika neno.
Kwa mfano,
(i)
Mama atapika
(ii)
Humphrey Lema
anafundisha wenzake darasani.
Vipashio na
na ta vinatoa maana tofauti ya
sentensi, ta inaashiria wakati ujao
na na inaashiria wakati uliopo.
Sarufi
muundo (sintaksia)
Ni sarufi inayoshughulikia namna maneno
yanavyopangwa ili kujenga sentensi. Mpangilio wa maneno katika tungo unaweza
kufanya tungo itoe taarifa iliyokusudiwa, au ipotoshe taartifa, au itoe taarifa
zaidi ya moja na kumchanganya msikilizaji.
Kwa mfano;
(i)
Kiti mimi nina
(ii)
Mimi nina kiti
Sentensi ya kwanza haieleweki kwa sababu maneno
yake hayakupangwa kwa muundo sahihi wa sentensi za Kiswahili.
Sarufi
maana (semantiki)
Ni sarufi inayofafanua maana za maneno ya lugha
fulani. Pia huzingatia muktadha wa neno linalotumiwa.
Kwa mfano
(i)
Niletee kanga
haraka
(ii)
Ukifuata barabara
utakuwa salama
(i)
Msikilizaji
anayejua ya kuwa kanga ni ndege tu anaweza kumleta ndege huyo, kumbe
mzungumzaji amekusudia kuletewa nguo.
(ii)
Mtu asiyejua
kuwa barabara ina maana ya sawasawa anaweza kufuata njia anayoiona kuelekea
sehemu fulani.
Dhana
ya Utamaduni
Utamaduni
ni mfumo wea maisha ya watu jinsi wanavyoishi na maandeleo yao kijamiii,
kiuchumi, kisiasa, n.k . Tanzania ni moja kati ya nchi zinazosifika duniani kwa
kulinda maadili yao
Kuna
makabila kama yasiyopungua 120 amabayo yote hutunza mila na desturi zao kwa
kiasi tofauti tofauti. Mavazi, salamu na vyakula ni miongoni mwa mambo yanayobainisha
utamadumi wa mtanzania
Lugha
ya kiswahili kama kielelezo cha utamaduni wa mtanzania
Matumizi
ya lugha ya kiswahili kama kielelezo cha utamaduni wa mtanzania huweza ujizidhilisha katika misingi ifuatayo;
a)
Lugha
nji njia kuu ya mawasiliano na hubadilika kadri jamii inavyobadilika. Ni sehemu
ya utamaduni, ni amali ya jamii
ianyoizungumza na ina alama ya
umoja wa taifa. Pia lugha ni utambuylisho wa jamii na kwa kutumia lugha watu hupashana habari,
hujenga uhusiano wa kufahamiana, kuelimishana n kupatana au kufarakana. Bila
lugha ingekuwa vigumu kuurithisha
utamaduni wa kizazi kimoja hadi kizazi kingin. Kama lugha itaendele kuwa
kielelezo cha utamaduni wa watanzania, basi kiswahili kitaendelea kuwa njia kuu
ya mawasilianao ya wanajamii wa watanzania
na hata nje
b)
Matumizi ya
kiswahili katika shughuli za utamaduni yamechochea maendeleo ya jamii ya
tanzania kwa namna nyingi.Lugha ya kiswahili hutumiwa na vikundi vya sanaa au
vyama mbalimbali vya utamaduni kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa.Sanaa za
kuchonga kama vinyago pamoja na kwamba zinahitaji kujieleza kwa kuzitazama tu.
Lugha ya kiswahili hutumika kutolea ufafanuzi wa fikra mficho katika sanaa hizo
c)
Matumizi ya
kiswahili hudhihirika katika nyimbo ambazo huwa na mafunzo na maadili fulani
kwa jamii kwa mfano; maadili ya kuwaelimisha wanajamii kuhusu mambo mbalimbali
d)
Katika
magazeti na vyombo vingine vya habari,Lugha ya kiswahili ni mojawapo ya lugha
zinazotumika kuelezea, kuelimisha na nakuburudisha wanajamii kuhusu mambo
kadhaa wa kadhaa yakiwemo ya utamaduni.Michoro ya vikatuni kuambana na
maelezo yaliyoandikwa kwa lugha ya
kiswahili ili kutoa mafunzo mbalimbali ya kitanzania kwa walengwa
e)
Viongozi wa dini hutumia lugha ya kiswahili
katika kutunga sheria na kanuni pamoja na kuandika vitabu vyenye mambo bora ya kuelimisha jamii
Umuhimu
wa kulinda na kuhifadhi utamaduni wa kitanzania
a)
Kutambua na
kulinda rasilimali , mazingira na urithi wa utamaduni
b)
Kuhakikisha na
kuhimiza usawa katika matumizi bora ya
mgawanyo wa haki na rasilimali na miliki
c)
Utamaduni
husaidia kuenzi na kutunza tabia njema
na kukemea vitendo viovu kama
vile matumizi matumizi ya dawa za kulevya , ulevi , wivu, uzembe n.k
d)
Utamaduni
husaidia kutambua na kuthamini kazi halali
kuwa ni msingi wa maisha na maendeleo ya binadamu
e)
Utamaduni
husaidia kuiandaa jamii kutambua kwamba, elimu, mafunzo na ubunifu ni muhimu katika kuzalisha mali nna kuendesha
mambo ili kuongeza tija na kuleta ufanisi
f)
Utamaduni
husaidia kuinua hali ya maisha ya jamii
kupitia nguzo zake kuu mfano sanaa za ufundi na sanaa za maonyesho
g)
Utamanuni au
jamii kuthamini na kutumia ujuzi,
taaluma na teknolojia ya kisasa na ya jadi kuimarisha afya, matumizi bora ya
mazingira, rasilimali na kuendeleza jamii
h)
Uta,maduni
hujenga tabia ya ushirikiano, mshikamano, udugu, uzalendo, upemdo na moyo wa
kuvumiliana wakati wa shida na raha
i)
Utamaduni hulitambulisha na kulingaza taifa nje ya
mipaka yake na kuimarisha uhusiano wa kitaifa.