Imeandaliwa na Mtila Mswahili
1.0 UTANGULIZI.
Kwa mujibu wa kamusi la Kiswahili Sanifu (TUKI).
(2004). Utamaduni ni mila, asili, jadi, na desturi za kundi Fulani.
Loliyong. (1972). Utamaduni ni jumla ya shughuli
kumbukumbu na mipango ya baadae ya jamii fulani zikiwemo pia ndoto na maono ya
jamii hizo.
Ibrahim, H. (2005). Jumla ya mambo yote yanayobuniwa
na jamii ili kukidhi utashi na maendeleo ya jamii.
Ni mwenendo wa maisha ya jamii na mtazamo wao, na
mambo na taratibu zao za kuendesha maisha ambazo huwatofautisha na jamii
nyingine. Kutokana na maelezo hayo ni wazi kuwa utamaduni huipa upekee na
kuifanya kutambuliwa kwa njia maalumu. Jamii yoyote inayotaka kuendelea
kutambulika na kuenziwa ni sharti iwe na upekee katika vipengele mbalimbali vya
kiutamaduni. Tunatambua kuwa, mila na desturi hujengwa kutokana na kurithishwa
kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Iwapo jambo hili halitotekelezwa kuna
uwezekano mkubwa wa kufifia kwa utamaduni uliopo katika jamii hiyo na hata
kupotea kabisa kwa wazanzibar.
Vipindi mbalimbali vilivyopitia utamaduni wa
Zanzibar. Baada ya mapinduzi ya Zanzibar 1964/01/12 utamaduni wa Zanzibar
ulianza kubadilika.
Kuanzia Mwaka 1964 mpaka 1979: Utamaduni wa Zanzibar
ulijionesha katika vipengele mbali mbali kama vinavoelzwa hapo chini.
1.1 MALENGO
1.1.1
Lengo kuu.
Ni kuonesha mabadiliko ya kiutamaduni katika vipindi
mbali mbali baada ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar hadi sasa.
1.1.2
Malengo madogo
- Kuonesha historia
ya utamaduni wa mswahili Zanzibar baada ya uhuru
- Kuonesha maendeleo
ya kiutamaduni wa mswahili hapa Zanzibar.
- Kuonesha
mabadiliko ya utamaduni wa mswahili hapa Zanzibar.
- Kuonesha ushahidi
kutokana na utamaduni wa mswahili halisi.
Zanzibar ni muunganiko wa visiwa viwili ambavyo ni
Unguja na Pemba, ambapo ndani yake muna visiwa vingine vidogo vidogo
vilivyozungukwa na bahari ya Hindi katika pande zake zote, Zanzibar pamoja na
visiwa hivyo vina historia ya kweli ya muda mrefu sana kutokana na matokeo na
mambo mbalimbali yaliyoijenga historia hiyo. Zanzibar ilikuwa imetawaliwa na
wakoloni mbalimbali wakiwemo Waengereza, Wajerumani, Waarabu, Wapashia, na
Wareno. Kila koloni lilikuwa na tamaduni zake walizotoka nazo kutoka katika
nchi zao na kuziendeleza katika visiwa vya Zanzibar kurithisha kizazi hadi
kizazi.
Wakoloni hawa waliitawala Zanzibar kwa muda mrefu na
kuanzisha mambo mbalimbali ya kiuchumi kwa manufaa yao. Wakati mapinduzi ya
Zanzibar 12/01/1964. Yaliyoongozwa na Muasisi wa mapinduzi hayo Shekhe Abed
Aman Karume.
Tayari tamaduni zote walizokuja nazo wakoloni
zilikuwa zilishaenea na kuendelezwa na
wazanzibar waliowengi.
Picha.na 1.0. inaonesha wanafunzi wa chuo kikuu SUZA
wakiongea na mwanahistoria wa mambo ya kale na utamaduni katika eneo la Dunga.
3.1
UTAMADUNI WA ZAMANI
Utamaduni wa mzanzibari kuanzia mapinduzi ya
Zanzibar 1964 ulidhihirika katika vipengele mbalimbali.
Ni sehemu muhimu ya utamaduni wa mswahili wa
Zanzibar, yalikuwepo mavazi maalumu ya kike na ya kiume, Wanaume walikua
wakivaa nguo tofauti na wanawake vile vile wanawake wakivaa nguo tofauti na
Wanaume, Pia watu wazima wakitifautiana mavazi yao na vijana. Kwa ujumla watu
wa Zanzibar baada ya mapinduzi walikua wanapenda kuvaa mavazi ya heshima
kulingana na jinsia zao na utamaduni wao.
Mavazi ni muhimu katika utamaduni, Mfano:-
Vazi la kanga: Vazi la kanga lilikua ni muhimu
katika kuonesha utamaduni wa Zanzibar. Kanga ilipendelewa zaidi kuvaliwa na
wanawake katika shughuli tofauti na kuzivaa hasa wanapokuwa majumbani mwao na
kutembelea sehemu za karibu na sio katika safari za mbali. Japokuwa Wanaume
walizitumia kujifunga wakiwa nyumbani lakini haikuwa mavazi yao rasmi.
Vazi la kanzu:
Kanzu ni miongoni mwa mavazi ambayo yalitumika katika kuonesha utamaduni wa kizanzibar. Vazi hili lilikua likivaliwa na Wanaume wakati walipokua wakienda misikitini au madrasa, maeneo mbali mbali ya visiwa vya Zanzibar. Pemba na Unguja walikua wakivaa vazi hili mfano: mjini Unguja kwa upande wa Unguja na Chake chake Kwa upande wa kisiwani Pemb
Baibui ni vazi ambalo lilikuwa likivaliwa na
Wanawake tangu hapo mwanzo kabla ya mapinduzi mpaka sasa. Vazi hili lilikuwa
likivaliwa na kila namna ya uvaaji wake basi lilikuwa likitoa maana yake.
Lakini baibui lilikuwa likivaliwa hapo mwanzo lilikuwa likiitwa baibui la
kamba(kizero) na maana hizo ni kama zifuatazo:-
a. mwanamke akivaa baibui kawaida, hivyo
inamaanisha kwamba anaenda dukani kutafuta vitu vya skukuu au vitambaa. Au
anavaa baibui akiwa amefunga kamba au hajafunga kizero katupia nyuma pia hiyo
maana yake anaenda dukani.
b. Mwanamke
akiwa amelivaa baibui akalishika kutoka chini mpaka kwenye mabega, kifua kikawa
wazi maana yake anaenda ugomvini kugombana na mtu mengine.
c. Ikiwa
mwanamke amelivaa baibui moja kwa moja na kizero akikifunika lakini unyuzi
hajaufunga maana yake huyo ni kizuka.
d. Ikiwa
kizero akikifunika usoni na akafunga na kamba maana yake huyo ni biharusi.
e. Mwanamke
akivaa baibui kifua wazi huku amelikamata maana yake huyo ni mjane.
f. Mwanamke
ikiwa amelivaa baibui na akalikamata kwa mkono basi maana ni anamgonjwa.
g. Mwanamke
ikiwa amevaa baibui, kizero amekipeleka nyuma nyuzi hajafunga na viatu mkononi
maana yake anaenda mazikoni.
h. Mwanamke
ikiwa amelivaa baibui na mkoba kavaa ndani ya baibui maane yake anaenda Kwa
bwana wake.
Picha na 1.2. inaonesha baibui la kizero
Vazi
la kofia
Ni vazi ambalo lilikuwa likivaliwa tangu mapinduzi
na hata sasa bado vazi hili limekiwa likivaliwa, pia vazi hili lilikuwa lina
namna mbalimbali ambazo pia zilikuwa zikitoa maana zake.kofia ambazo zilikuwa
zikivaliwa hapo tangu mwazo ni kama vile; tarbushi, kofia ya kiuwa
shumbulele(ilikuwa sana ikivaliwa na wavuvi).
Vazi
la kanga
Vazi hili lilikuwa sana likivaliwa na Wanawake na
ilikuwa ikipendelewa sana Kwa vijana na watu wazima kulivaa vazi hilo kama
sehemu mojawapo ya kujistiri.
Picha
.1.4. Vazi la heshima la kanga
Pia kuna mavazi mengine ambayo yalikuwa yakivaliwa
na waswahili wa hapa Zanzibar tangu mapinduzi kama njiani mojawapo ya kukuza na
kuuendeleza utamaduni wao. kama kikoi,shuka, kanzu na koti ,viatu vya
matarawanda na viatu vya biharusi.
4.1
VYAKULA
Wazanzibar pia walikuwa wakitumia vyakula vyao kama
kuuenzi na kuuendeleza utamaduni wao. Ambapo wanajamii wengi wamekuwa wakitumia
vyakula hivyo na hupendelea sana kutumia vyakula hivyo katika kukuza utamaduni
wao na kuvirithisha kizazi hadi kizazi. Vyakula hivyo ni kama vile; Manda,
bobwe, mseto, kipote, tapo, muhogo, makopa, tuwale, matonge, vwevwe, kirugu
(ugali wa muhogo), ndizi, uwele, mtama, ugali wa macho macho, vikuku, bokoboko
(uji wa nazi wa uwanga), zarubia, mabwabwata, pia katika mbogamboga kuna mnavu,
mungunye, na makunga.
Picha.2.0. vyakula vya alili.
5.1
VINYWAJI
Hivi pia ni vimiminika ambavyo vilikuwa vikitumiwa
na watu kama sehemu ya kiburudisho chao ama kinywaji chao cha asili ambavyo
hutumika katika kuuendeleza utamaduni wa kizanzibar mfano wa vinywaji hivyo ni
kama vile, potelo, togwa, uji wa mtama, uji wa mapunje, uji wa uwele.
6.1
SANAA
6.1.1
Sanaa ya muziki
Sanaa ya muziki nayo ni
miongoni mwa sanaa chachu ya utamaduni wa mswahili wa Zanzibar. Sanaa ya muziki
ni sanaa pendwa, pia ni kitambulisho cha utamaduni wa mswahili kwani walikuwa
wakitumia mambo ya asili katika muziki huo katika kuuenzi utamaduni wao. Miziki
ya kipindi hicho ilikuwa ni kama taarabu asilia, dumbaki, Ngoma ya msondo na
nyengine. Wanamuziki waliutangaza sana utamaduni wa mswahili wa Zanzibar
kupitia nyimbo zao ndani na nje ya nchi kama vile India na ulaya, ambapo
zilienea zaidi nyimbo za Bi Siti bint Saad na Bi Kidude bint Baraka, pamoja na
Mzee Makame Faki. Miongoni mwa nyimbo walizoimba ni kama vile, Nifanye nini,
Kijiti, Ahmada na Mpewa hapokonyeki.
Picha n.3.0.
inonesha wasanii wa zamani.
Katika mwaka 1990 sanaa ya muziki ilikuwa zaidi Hadi
kuchipukia kwa muziki wa zenji fleva. miongoni mwa wasanii hao na nyimbo zao ni
kama vile, AT na Berry Black, wimbo ni Kama Nimekosea.
Picha.3.1
Msanii wa zenji fleva
6.1.2
Sanaa ya maonesho
Hii ni sanaa inayooneshwa
katika kundi la watu kwa ajili ya kutoa ujumbe na kuelimisha jamii katika
nyanja nyingi. Sanaa hizi ziliweza kuibua hisia za watazamaji na wasikilizaji
pamoja na kuimarisha utamaduni. Sanaa hii ilihitaji upeo mkubwa wa kifikiri na
kuangalia yaliyomo katika jamii za waswahili. Miongoni mwa maonesho hayo ni
kama vile, maigizo, mashairi, ngonjera, Ngoma na maonesho mengine yenye kuibua
hisia. Wanamichezo hao wakongwe ni kama vile, Mzee Halikuniki, Mzee sekembuke,
walioogoza michezo kama vile, Kituko, Maraka tuu na Ugomvi wa mke.
Picha.3.2. Inaonesha
wanavichekeasho wa zamani wa Zanzibar
6..1.3
Michezo
Waswahili wa zanzibar pia walikuwa wakicheza michezo
mbalimbali katika kuuendeleza utamaduni na kuuendeleza hadi sasa mfano wa
michezo hiyo ni kama vile; mchezo wa ng'ombe, kurumbizi, Ngoma ya msewe,
kidumbaki, kuvuta kamba, mashindano ya vidau, mchezo wa kujisuka na charanga.
a.
Mchezo wa kamba: ni mchezo ambao ulikuwa ni wa
kushindana kuvuta kamba baina ya pande mbili ili kupimana nguvu. hususani
maeneo ya pujini.
Kurumbizi/ngwale: ni mchezo wa kuangushana hususani
maeneo ya pemba.
b.
Kidumbaki: hizi ni ngoma ambazo zilikuwa zikipigwa katika
sherehe za harusi.
Ngoma ya msewe: Ngoma hizi zilikuwa zikipigwa sana
kwenye sherehe za mavuno na sherehe za siasa.
c.Charanga:
ni Ngoma ambazo zilikuwa zikipigwa kwenye mikutano na hata katika mashindano ya
mpira kama kusherehekea. Ngoma hii sana ilikuwa ikipigwa maeneo ya kojani
Ngoma ya umundi: ni ngoma ambayo ilikuwa ikipigwa
katika sherehe za uganga hususani katika maeneo ya wingwi na kiuyu (pemba)
iii. Sherehe
Waswahili wa Zanzibar walikuwa wakifanya sherehe
katika kusherehekea, kufurahi na kujumuika kwa pamoja. Mfano wa sherehe hizo ni
kama vile:-
Sherehe za maulidi yaliyokuwa yakifanyika maeneo ya
Tumbatu (Gomani), Pemba (kojani), Fundo na Micheweni
a.
Sherehe za mavuno, hizi zilikuwa zikifanyika kila baada
ya mavuno na kusherehekea mavuno yao sehemu hizo ni kama vile Makunduchi
b.
Sherehe za harusi, ni sherehe zilizokuwa zikifanywa siku
za harusi katika jamii zao ambapo walikuwa wakipiga Dufu, Ngoma za vibati na
Kidumbaku. Watu walikuwa wakivaa mavazi yao mazuri. Kwa upande wa biharusi
alikuwa akichaguliwa mume na mzee wake pia alikuwa akiwekwa ndani mwezi kabla
ya harusi na kupewa mafunzo ya ndoa. Na baada ya ndoa wote mke na mume
hawaruhusiwi kutoka ndani mpaka wiki ifike huku wakihudumiwa.
Mavazi ya bibi harusi wa zamani alikuwa akivaa
buibui la nyuzi (kizoro) na kanga na mitarawanda. Na Kwa upande wa bwana harusi
alikuwa akivaa kanzu koti na kofia au kanzu kofia na joho na viatu vya
makubadhi.
c.
Sherehe za mwaka kogwa; ni sherehe ambazo zilikuwa
zikifanywa haswa baada ya mavuno ambapo paliandaliwa mapigano ya vigongo baina
ya makundi mawili kwa ajili ya kupimana nguvu zao na pamoja na kutumia mavuno
yao katika skukuu. Lakini baadae rais wa kwanza wa Zanzibar aliamrisha watu
kupigana kwa kutumia makoa (magomba). Sherehe hizo zilikuwa maarufu sana
Makunduchi na Kojani.
d.
Sherehe za skukuu ya Iddil fitri na Iddi lhaji.
Sherehe hizo zilikuwa maarufu sana Zanzibar, zilikuwa zikifanywa katika mfunguo
mosi na mfunguo tatu. Siku hizo watu walikuwa wakivaa vizuri na kunywa vizuri
pamoja na kutembeleana.
Skukuu ya Iddil fitri (mfunguo mosi) ilifanyika
baada ya waisilamu kumaliza kufunga Ramadhani
Skukuu ya Iddil hajji (mfunguo tatu). Hii hufanyika
baada ya waisilamu kumaliza kufanya hija huko Makka. Hapa waisilamu hufunga
siku Tisa kama kuwakilisha waliokwenda hijja
6.5
UONGOZI NA SIASA.
Zanzibar ni moja ya maeneo muhimu sana katika
historia ya Tanzania. Kuanzia mwaka 1964 hadi sasa, kumekuwa na viongozi kadhaa
walioongoza Zanzibar. Hapa nitataja baadhi ya viongozi muhimu wa Zanzibar tangu
mwaka 1964:
1. Shekh Abeid Amani Karume. (1964-1972) - Alikuwa
Rais wa kwanza wa Zanzibar baada ya muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Alikuwa
kiongozi wa Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 na alikuwa rais hadi kifo chake mwaka
1972.
2.Ali Hassan Mwinyi. (1972-1984) - Alichukua
madaraka baada ya kifo cha Abeid Amani Karume mwaka 1972 na akahudumu kama Rais
hadi mwaka 1984.
3.Idris Abdul Wakil.(1984-1988) - Alikuwa Makamu wa
Rais chini ya Ali Hassan Mwinyi, na aliteuliwa kuwa Rais wa Zanzibar baada ya
Mwinyi kuhamia Tanganyika kama Rais.
4. Aboud Jumbe. (1988-1990) - Alichukua madaraka
baada ya kujiuzulu kwa Idris Abdul Wakil mwaka 1988.
5. Salmin Amour. (1990-2000) - Alikuwa Rais wa
Zanzibar kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2000.
Baada ya mapinduzi, yaliongozwa na Mzee
KARUME."1964" Zanzibar ilianza kufuata sera za kiongozi mpya, ambaye
kwa muda mrefu alikuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za Wazanzibari na
kusukuma mbele malengo ya uhuru na maendeleo ya taifa.
Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, uchumi
wa Zanzibar ulibadilika sana. Mapinduzi hayo yalikuwa ya kisiasa na kijamii na
yalilenga kubadilisha mfumo wa serikali na uchumi wa Zanzibar. Baada ya
mapinduzi, sera za serikali ya Zanzibar zililenga kujenga uchumi wa kijamaa na
kufanya mageuzi katika mfumo wa umiliki wa mali na rasilimali za nchi.
Umiliki wa Ardhi na Viwanda; Baada ya mapinduzi,
ardhi na viwanda vilivyokuwa vikitawaliwa na wakoloni na wakulima wakubwa
vilinaswa na serikali au kugawiwa kwa wananchi. Hii ililenga kusambaza mali na
rasilimali kwa usawa miongoni mwa wananchi. Kwa mfano makunduchi serikali
ilipanga mkakati maalumu katika kukuza uzalishaji wa mazao. Wanajamii
walipatiwa mbegu kuziatika na kuangalia mbegu gani imeota vizuri na kuichagua
hiyo katika mwaka huo kama zao la kuotesha.
i.
Uchaguzi wa Taifa. Baada ya mapinduzi wazanzibari
walikuwa wanaendesha masuala ya siasa katika kuchagua kiongozi atakaewaongoza
wananchi kwa utaratibu maalumu. Ili
uwempiga kura halali lazima uwe
na meno kumi na nane (18). Yani (gego la mwisho liwe limeota). Serikali
ilioshika madaraka iliwafanya raia kuwa na mapenzi na viongozi wake na
kudhibiti machafuko kutotokezea. Hivyo, watu waliishi kwa amani na furaha na
viongozi wao.
Picha na .4.0. Picha
inaonesha uchaguzi wa taifa.
7.1
UCHUMI WA WAZANZIBARI BAADA YA MAPINDUZI.
7.1
Biashara.
Biashara baada ya mapinduzi ilikuwa ni wachache
wanaojihusisha na biashara, kwa sababu ilitangazwa rasmi kuwa kila mmoja afanye
biashara anayoitaka. Ispokuwa wale waliopewa mamlaka na serikali, mfano Pemba
watu walikuwa wanakwenda kupanga msongo maeneo ya wete kununua kilo ya Mchele,
na inawezekana asiupate kwa siku ile. Baada ya miaka michache ikatangazwa kuwa
kila mmoja afanye biashara anayoipenda mahali popote, watu wakafungua maduka ya
vyakula kama vile mchele, maharage, nguo, vyombo vya baskeli za rali
nakadhaalika.
Picha na 5.0. inaonesha biashara.
7.2
Kilimo
Baada ya Mapinduzi, serikali mpya ya Zanzibar
ilianzisha sera ambazo zililenga kuendeleza kilimo na kuinua hali ya maisha ya
wakulima. Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na:
Serikali ilichukua hatua ya kutaifisha mashamba
makubwa yaliyokuwa chini ya umiliki wa wakoloni au wenyeji matajiri na kugawa
ardhi hiyo kwa wakulima maskini. Hatua hii ililenga kuhakikisha usambazaji wa
ardhi kwa wakulima wengi ili waweze kufaidika moja kwa moja na kilimo.
Kuwepo kwa vyama vya Ushirika.Serikali ilianzisha
vyama vya ushirika ambavyo vilisaidia wakulima kuungana pamoja na kunufaika
kutokana na nguvu ya pamoja. Vyama hivi vilisaidia katika usambazaji wa
pembejeo za kilimo, mafunzo kuhusu mbinu bora za kilimo, pamoja na soko la
mazao yao.
Kilimo cha mazao ya biashara. Kuanzia 1964 biashara
ilikuwa na kusababisha waswahili kuwa na utamaduni wa kujipandia mazao ya
biashara kama vile karafuu. Minazi. miembe. Wakati wa karafuu watu wakiambizana
wote wenye uwezo wa kuchuma waende katika mashamba kwa ajili ya kuchuma zao
hilo.
Picha na.5.1 inaonesha mazao ya
biashara yanayolimwa Zanzibar.
Shuhuli za uvuvi. Uvuvi ilikuwa ni shuhuli maarufu
iliyo ikifanya na waswahili baada ya mapinduzi kwa ajili ya kupata kipato cha
kujikimu kimaisha. Waswahili walikwenda baharini kutafuta samaki, pweza, chaza,
kome, korong'onjo, choe, Tondo na kadhalika. Waliitumia bahari kupata kitoweo
na pia kupata kipato cha pesa. Vilevile walikamata samaki kutoka katika mito na
maziwa kama vile perege, kambare na aina nyengine za samaki.
7.3
MSIBA.
Misiba ya wazanzibari ilipo kuwa ikitokea,
walizingatia zaidi dini zao walizo kuwa nazo na hasa dini ya kiislamu na
wakiristo.
Katika msiba wa waislamu, ulipokuwa unatokea watu
wakikusanyika katika eneo la tukio na kushirikiana kwa hali na mali katika
kumstiri marehemu. Hutolewa watu katika kila Kona ya kijiji ili kila chochoro
angalau mtu mmoja aweze kushiriki katika uchimbaji wa kaburi. Watu wa karibu
walikuwa na utaratibu wa kuleta chakula ili wale na wafiwa kwa pamoja. Na
walikuwa na utaratibu wa kupeana mkono wa pole pia kulala matangani siku tatu.
Pia walisoma hitima ikifika siku ya tatu na siku ya
arobaini wakisoma halili.
Picha na 6.0. inaonesha misiba wa waswahili
Kwa upande wa wakiristo. Walikuwa anapokufa mtu
wanakusanyika na kumuombea kuuwaga mwili na baadae kwenda kumzika akiwa ndani
ya jeneza.
8.1
UONGOZI NA SIASA YA SASA.
Viongozi waliongoza kuanzia 2000 hadi 2024 nikama
wafuatao:
1.Amani Abeid Karume. (2000-2010) - Alikuwa rais wa
Zanzibar kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2010.
2. Ali Mohamed Shein. (2010-2020) - Alikuwa rais wa
Zanzibar kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2020.
3. Hussein Mwinyi. (2020-hadi sasa) - Alichaguliwa
kuwa rais wa Zanzibar.
Siasa za sasa zimekuwa za kiuhasama, kiuadui na
kujengeana chuki baina ya watu. Hii ni kutokana na kuwa viongozi wanaochaguliwa
hawana huruma na wafuasi wao, hujali kitu kuliko utu. Huwajaza Imani wafuasi
wao na matokezeo yake watu huanza kupigana, kudhulumiana, kutosalimiana,
kutohudhuria katika misiba ya kundi au watu wengine na hata kupoteza uhai wa
wengine. Utamaduni huu ulianza kukua kuanzia" 2000" Hadi sasa.
Mikutano
Siasa za sasa hufanyika kwa ushindano mkubwa baina
ya vyama tofauti. Kila kundi linajiona limekamilika kutokana na muamko wa watu
wanaohudhuria katika mikutano mbalimbali ya kisiasa. Watu hupiga ngoma na
matarumbeta pia husoma utenzi unaowapa moyo wafuasi, na kiongozi hupanda
jukwaani na kuhutubia hadhira iliomzunguka.
Uchaguzi
mkuu.
Siku ya uchaguzi Wazanzibar hujitokeza kwa wingi
katika vituo vilivyopangwa kwa ajili ya kupiga kura. Siku ya kura kila mmoja
huacha kila kitu ilimradi afike katika maeneo ya kupiga kura na kutekeleza
zoezi hilo. Utamaduni uliopo nikwamba , mpiga kura atakaefika mapema huanzisha
foleni bila kuzingatia vyeo vyao, vyama vyao , rangi zao , masikini wala tajiri
ispokuwa wote siku hiyo wanakuwa sawa , wala huwezi kumbagua mtu kutokana na
mavazi aliovaa ispokuwa viongozi katika chama fulani.
Picha na 6.1. inaonesha mahojiano juu ya chaguzi za
kisiasa
8.2 MILA.
Katika utamaduni wa mswahili wa Zanzibar pia
waswahili hawa walikuwa na mila zao ambazo walikuwa wakizifuata kutoka kwa
mabibi na mababu zao. Mila hizo walikuwa wakiziendeleza kwa kuzitekeleza kama
zinavyotakiwa..Mila hizo zilikuwa zikifanywa ima kwa siku kadhaa katika mwaka
na ni lazima zitekelezwe katika jamii husika.mfano wa mila hizo ni sherehe za
mwaka kogwa ( kutoka katika jamii ya makunduchi) , sherehe ya kuoga mwaka
(kutoka katika jamii ya pemba- kojani).
Picha n.6.2 inaonesha mila za waswahili katika eneo
la makunduchi
8.3
ITIKADI
Hii hufungamana sana na Imani ambapo wanajamii
huamini katika jambo fulani kwa kuomba shida na matatizo yao ili yaweze
kutatulika. Katika itikadi hizo waswahili wa zanzibar walikuwa wakiomba katika
mizimu ya mababu na mabibi zao, kuomba katika mapango na hata katika miti
mikubwa. lakini ingawa dini ilikuwa imeshaingia nchini lakini walikuwa
wakiabudu kwa misingi ya dini hizo na itikadi zao zilikuwa zikifuatwa vilevile
pasi na kuharibu au kuathiri utamaduni wao. Vilevile kutokana na itikadi hizo
nyengine zilikuwa zikiwekwa mipaka na kuwa jinsia hii itafanya na nyengine
isifanye juu ya kile wanachokiamini. Waswahili hawa huamini sana katika masuala
haya hata kama wakawa na mgonjwa au ugomvi katika familia zao basi hufuata
itikadi zao. mfano wa itikadi hizo ni;
wanawake pekee kuruhusiwa kuoga mwaka kogwa pasi na
kuonekana ama kushiriki na mwanaume yeyote na ikitokea mwanaume ataenda kuwaona
wanawake hao basi atahukumiwa kesi juu yake.
Wanawake wajawazito kutoruhusiwa kula yai kwa
kuhofia kuharibu ujauzito au kumuathiri mtoto wake. Mwanamke alie katika ada
yake haruhusiwi kuchuma mboga kwa kuamini kuwa ikiwa atachuma mboga hizo basi
zote hufa.
Kiti au kibanda kilichojengwa Kwa ajili ya kiongozi
au mkubwa wa kijiji basi katika sherehe zao za kiitikadi ilikuwa haruhusiwi
yeyote kukitumia kifaa hicho hata kama mwenyewe hayupo .ila katika siku za
kawaida basi huruhusiwa kutumia bila hata ya idhini ya mwenyewe na ikitokezea
mtu katika sherehe zao akatumia vifaa hivyo pasi na mwenyewe basi vilikuwa
vikimdhuru.
Picha na.6.3. inaonesha
herehe za mwakakogwa
8.4
JADI ILIVYOKUWA INATUMIKA
BAADA TU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 1964
Jadi ni miongoni mwa mila, maarifa pamoja na imani
ambayo hurithishwa kutoka kizazi hadi kizazi na ni sehemu ya utamaduni wa jamii
ya wanaadamu. Jadi huhusisha urithi wa kitamaduni unaotambulisha jamii fulani
na kuendeleza utambulisho wake kwa njia ya shughuli, fikra na maadili yaliyomo
katika utamaduni huo. Kwa kiasi fulani jadi ilivyokuwa ikitumika kabla ya
mapinduzi ya Zanzibar na baada ya mapinduzi mnamo miaka ya 1964 imegawika
katika vipengele.
I.Ngoma za jadi:
Ngoma za jadi zilizokuwa zinatumika
tangu enzi na enzi na mara tu baada ya mapinduzi ya Zanzibar ni kama vile Ngoma
ya Pungwa ambayo katika visiwa vya Zanzibar inafanyika Bumbwini Unguja na kwa
upande wa Pemba ngoma hii hujuilikana kama Umundi, pia ngoma ya Rubamba ambayo
hujumuisha mavazi meusi, Ngoma ya Somali au Ruhani, ngoma ya kibuki ambayo
asili yake ni Komoro. Ngoma hizi zimekuwa zikitumika sana tu katika kipindi cha
miaka ya nyuma na zilikuwa zikitiliwa maanani sana.
II.Vyakula vya jadi
Jadi ina muingiliano mkubwa na mila ambayo
imehusisha vyakula mbali mbali vya kijadi. Vyakula vya kijadi ni vyakula vya
asili lakini si kila vyakula vyote vya asili vinaweza kuingizwa katika jadi.
Mfano wa vyakula vya kijadi ni Bumbwi, Manda, Makopa yanayotengezwa kwa Muhogo,
Nyama ya kuchoma na venginevyo. Kimsingi vyakula hivi ndivyo vinavyotumika
katika jadi na vilikuwa vikipewa kipaombele sana katika ulaji wao. Vyakula
hivyo vya jadi vinatumika kuliwa katika sherehe za kijadi vilevile hutumika
kupikiwa mashetani pamoja na mizimu ili watu kuweza kuendeleza jadi yao ambayo
walirithi kutoka kwa mababu zao na mabibi zao na ndiyo maana ya kuwa jadi
hurithishwa kizazi hadi kizazi.
III.Matibabu ya jadi
Katika upande wa matibabu ya kijadi
hapo miaka ya nyuma kidogo baada ya mapinduzi ya Zanzibar miaka ya 1964 watu
walikuwa wakitumia sana dawa za mitishamba yaani dawa za asili pamoja na
kujitibu kupitia njia za kuomba mashetani. Matibabu haya yalikuwa na utaratibu
maalumu, Kwa upande wa matibabu ya kutumia dawa za asili yaani mitishamba watu
walikuwa wakiingia maporini na kujikatia miti inayofaa kwa kutibu maradhi yao.
Kwa upande wa matibabu kupitia njia za mashetani watu huenda kwa mafundi
(waganga wa kienyeji) ambao wao hutumia mashetani katika kutibu watu na
wagonjwa huambiwa wapeleke aidha kuku wa aina pamoja na rangi fulani, Ng'ombe,
Mbuzi, Kondoo pamoja na masharti mengine ili kuweza kupona maradhi waliokuwa
nayo. Pia kwa upande wa familia inakuwa na jadi yao ambayo wamerithi kutoka kwa
wazazi wao, kwahiyo mtu anapoumwa katika familia kiongoz ambae ameibeba jadi ya
familia hiyo ndiyo hutoa dawa. Na ikiwa familia hiyo kila mtu ana matatizo basi
hupewa kipaombele sana jadi kwa kuamua kuchicha mnyama yoyote ili familia hiyo
iweze kuepukwa na mikosi pamoja na nuksi. Matibabu mengine ya kijadi ni kuomba
kwenye mizimu au mashetani kwa ajili ya kutafuta tiba. Watu huenda sehemu za
mapango, kwenye mijiti mikubwa na sehemu maalumu zilizotengenezwa kwa ajili ya
kuomba mizimu pamoja na mashetani ili kuweza kupata tiba. Zifuatazo ni picha
zinazoonesha sehemu ambazo watu huenda kuomba ili kupata tiba na kutatuliwa
matatizo yao waliokuwa nayo.
Picha.na 7.2 inayonesha jadi za
waswahili.
Picha na.6.4 inaonesha wanafunzi wakifanya mahojiano
na Mzee Mwita wa Makunduchi katika eneo la mwaka kogwa.
8.5
MAADILI YA KALE
Maadili ni tabia ya mtu, watu au jamii Fulani.
maadili hayo yanaweza kuwa mabaya au mazuri. Baada ya uhuru yalikuwa katika
hali nzuri na ya kuridhisha kutokana na kushirikiana kwa wazee katika kulea
watoto waona kuwarithisha tabia njema ili kuwalindia utu na heshima za wazazi
wao, watoto walikuwa na adabu kwa wakubwa na wadogo zao, wakifuata mila na
itikadi zao kwa kufuatiwa na msemo usemao usiache mbachao kwa msala upitao. Kwa
wakati huon watoto walifundishwa mambo mengi kama kupata elimu, kujilinda na
vishawishi jambo ambalo limepelekea kutokuwepo kwa ukatili, ubakaji, na
udhalilishaji kwa vile jamii ilileana katika maadili mema mpaka kufikia kipindi
cha (1999). maadili yalipewa kipao mbele sana kwasababu kila mzazi alikuwa
hayupo tayari kumuona mtoto wake anapoteza na anaenda kinyume na maadili ya
utamaduni wa mswahili. Hivyo ikapelekea wazazi kujifunga kibwebwe kuepukana na
kwenda kinyume na na maadili kwasababu waliamini kwamba maadili ndio kitu
muhimu kwa mwanadamu katika harakati tofauti tofauti za kijamii na kimaisha.
Endapo mtu atakosa maadili alionekana kuwa haifai kuigwa katika jamii hiyo.
Mifano ya maadili ni kama vile watoto kuwasaidia wazee wanapokuwa na mizigo,
kuongea kauli nzuri unapoongea na watu wazima, kuwasalimia kwa kutumia
utamaduni wa mswahili, kuwa na mavazi yenye heshima na stara nakadhalika.
Vilevile maadili yaliongozwa na wanajamii wote na
ikafikia hatua kwamba mzazi yoyote anauwezo wa kumkanya na kumpa maadili mema
mtoto wa mzazi mwenzake. Na waliamini msemo wa wahenga waliosema " Samaki
akioza mmoja huoza wote" hivyo kutokana na msemo huo waliondoa tofauti zao
kama wazazi na waliona mtoto mmoja ni wa wanajamii mzima kwahio walikuwa hawako
tayari kuona mtoto mmoja katika jamii yao anaenda kinyume na maadili yao.
Pia waliamini kwamba "umoja ni nguvu utengano
ni udhaifu" jambo hilo liliwapelekea kuwa kitu kimoja na endapo mmoja
miongoni mwao katika jamii atapata matatizo wanaona kwamba tatizo hilo ni lao
wote hivyo watashirikiana kwa hali na mali kutafuta njia mbadala wa kulitatua
tatizo hilo kwa pamoja na kuendeleza maadili yao.
Vilevile waliamini kwamba maadili yanaleta faida
katika jamii miongoni mwa faida hizo ni kama zifuatazo:
a) Kuwepo kwa umoja na mashirikiano miongoni mwa
wanajamii: Hii ina maana kwamba
wanajamii wanapokuwa wameshikilia maadili yao fulani kutapelekea umoja na
mashirikiano katika harakati zao za maisha. Kwa mfano wakulima hupeana mijima
ya kusaidiana kulima kwa pamoja pindi wanapomuona mwenziwao akiwa katika
harakati hizo hivyo huungana kwa pamoja kulitekeleza jambo hilo.
b) Huzidisha mapenzi kwa wanajamii: Hali hii hutokea
pindi endapo wanajamii katika jamii fulani wanapoishi kwa kuzingatia maadili
yao hivyo hupelekea mapenzi na kuoneana huruma baina yao kutokana na maadili
yao ambayo wanayatumilia katika shughuli zao za Kila siku.
c) Huondosha migogoro katika jamii: Hii ni kwamba endapo jamii itaamua kuwa na
maadili fulani mazuri husaidia kwa kiwango kikubwa kuondosha migogoro katika
jamii hiyo kwa sababu wanajamii wote wanafuata maadili ambayo yamewekwa na
wanajamii wote katika jamii hizo.
Picha.na 7.0 inaonesha maadili ya watoto wa zamani.
Vile zamani ilikuwa kuna maadili ambayo bibi au babu
wanakaa na wajukuu zao na kuanza kuwatolea hadithi katika usiku wa mbalamwezi
mfano:
Picha.na7.1 inaonesha wazazi walivyo wakiwahadithia
watoto wao.
Maadili ni
kitu kizuri katika maisha ya mwanadamu katika jamii kwasababu husaidia
wanajamii kuishi na maadili mema na mchakato mzuri katika maisha.
10.1
ELIMU
Hiki ni kipengele muhimu sana
ambacho watu walikuwa wakipata ujuzi na maarifa hapo mwanzo waswahili wengi wa
Zanzibar walikuwa wakipatiwa elimu katika mfumo wa usemaji na utendaji jambo
ambalo limepelekea watu kuwa na weledi zaidi katika taaluma hizo, lakini
waswahili hao walikuwa wakipatiwa elimu kutokana na dini na jamii
inavyowazunguka mpaka tulivyotawaliwa na wakoloni ndipo elimu yetu ikaanza
kubadilika na kuwa na mfumo wa usemaji hadi tulipopata mapinduzi ukaendelea
kutumika mfumo huo huo.
Vilevile elimu ya hapo mwanzo
ilikuwa tofauti sana na hii ya sasa katika maeneo na mbinu za kujifunzia mfano;
vifaa au zana zilikuwa ni dhaifu, maeneo ya kujifunzia nk. Hapo mwanzo wanafunzi wengi walikuwa
wakijifunza chini ya miti.
Picha.8.0.inaonesha elimu ilivyo ikisomeshwa.
10.
2 UTAMADUNI WA WASWAHILI WA ZANZIBAR KUANZIA 2000 HADI SASA
Kuanzia
mwaka 2000 hadi kuendelea hivi sasa utamaduni wa mswahili umeweza kupokea
mabadiliko katika kila kiepengele cha utamaduni wa mzanzibar. Na mabadiliko
hayo ni kama vinavyoelezwa:-
11.1
UTAMADUNI WA SANAA
Utamaduni wa sanaa wa kipindi cha Mheshimiwa Rais
Amani Abeid Karume (2000) hadi sasa umezidi kuimarika bali pia kubadilika
kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na muingiliano wa watu na
mabadiliko ya tabia ya nchi. Hivi sasa sanaa imezidi kukua na kuendelea
kuchangia maendeleo hapa Zanzibar.
i.Sanaa
ya muziki ya sasa.
Katika kipindi hiki sanaa ya muziki wa Zanzibar ni
tofauti kabisa na wa kale kutokana na maendeleo ya sayansi na Teknolojia. Hivyo
muziki wa sasa ni mkubwa na umejigawa. Miziki hiyo ni zenji fleva na zile za
taarabu asilia ( rusha roho) beni na mengine. Kwa sasa taarabu ndiyo pekee
ambayo bado inaonesha utamaduni wa Zanzibar kwa kiwango cha juu ukilinganisha
na hii ya fleva ambayo kiuhalisia imebadilika haswa kimavazi, chakula, na hata
lugha inyotumika. Ambapo jambo hili linapelekea kuharibu na kudumaza utamaduni
wa mswahili wa Zanzibar.pamoja na kuibua migogoro mingi yenye kuhatarisha na
kupelekea mifarakano baina ya wanajamii.
Miongoni mwa wasanii hao ni kama vile Dogo fany
mwenye wimbo wa Naumwa.
Tamaduni huo wa sanaa katika kipindi hiki
unajionesha wazi kama vile ifuatavyo:-
Picha.8.1. ikimuonesha msanii Dogo fany: wimbo'
Naumwa'
ii.
Sanaa ya maonesho
Kwa sasa sanaa hii imekuwa sana. Sanaa hii
imebadilika sana na zamani na hata ubunifu wake umekuwa ni mkubwa na wenye
mawanda mapana. Sanaa hizi zinafanywa maeneo mengi sana kwa sasa. Pia wapo
wanaoendeleza na kukuza utamaduni kutokana na kuonesha ama kiwasilishabyale
mambo yanayofanywa juu ya utamaduni wetu. pia wanaudumaza kutokana na maonesho
ya tasnia zao zisizozingatia utamaduni wa waswahili kama vile; lugha, Mila,
mavazi wala vyakula vya kiutamaduni.
Picha.n.8.2
ikionesha Sanaa ya muziki.
iii.Sanaa
ya ususi
Katika sanaa hii watu wa Zanzibar husuka nywele na
vitu mbali mbali kwa umaridadi ambapo vitu hivyo vikiwa na asili ya utamaduni
wa mswahili hapa Zanzibar. Miongoni mwa misusi hiyo kwa upande wa wanawake ni
kama misuko ya nywele ya mitindo tofauti kama vile boga (rocket), jicho la mkwe
mwenza, usinionee wivu, ambapo misuko hii ilikuwa ikisukwa kwa muundo wa
mbinjuo ama mnyoosho. Pia katika utamaduni wa ususi umeelekea kubadilika kwa
watu kuanza kuweka madawa kichwani, kusuka rasta na pia kukata mikato kwa
wanawake hao wa Kiswahili. Na kwa namna hiyo hata watoto wa kiumbe hivi sasa
wameonekana wakisukana mikato yao ya ajabu kama kiduku. Jambo ambalo
linapelekea kuharibu na kupoteza utamaduni wa kwetu na kuendeleza utamaduni wa
wageni.
Pia kwa upande wa sanaa ya ususi wa vitu umeweza
kukua na kuendelea na kuchangia kiasi fulani kibiashara kutokana na bidhaa hizo
zenye asili na utamaduni wa Zanzibar. Baadhi ya bidhaa hizo ni kama vile
vipepeo vya makuti na ukindu, mokoba ya ukili, makuti ya kujengea ingawa
yamepungua kwa sasa kimatumizi, usukaji wa matenga, madema na masusu ya kubebea
vitu. Vitu hivi watu husuka kwa mitindo mbali mbali ili kupendezesha na kuvutia
wateja wake. Ingawa pia watu wanaojishugulisha na sanaa hii si wengi kutokana
na maendeleo ya sayansi na teknolojia ambayo inawaletea vitu mithili ya hivi
kutoka nje.
iv.Sanaa
ya ushoni
Katika utamaduni wa sanaa ya ushoni bado inaendelea
kuonesha utamaduni wa mswahili kwa kushona mishono tofauti ya kiasili kama vile
dira, suti, vitenge, shati, baibui na shungi ( abaya kwa sasa), mshazari, sketi
na panjabi. Lakini pia wakati huu mishono hio umeweza kubadilika sana. Wengi
wao kwa sasa wanashona mishono kwa kuiga mitindo ya watu wa nje yautamaduni wao
jambo linalopelekea vizazi hivi vya sasa kuvaa nguo zisizostara. Mfano wa
mishono hiyo ni kama vile sketi fupi suruali za kubana (pedo), kitentemente, madira
ya mpasuo, Modo, Nguva na mengineyo.
Picha.n.8.3. ikionesha Sanaa ya ushonaji.
v.
Sanaa ya uchongaji
Sanaa hii nayo imeweza kukua kwa ustadi mkubwa na
wenye faida kwa wakati huu kuliko zamani. Michongo ya kisasa inavutia sana na
inafanya kuvutia wateja kutokana na mapambo wanayoweka katika vitu hivyo. Kwa
kipindi hiki seremala wengi huchonga michongo mikubwa na mizuri mno, Vitu hivyo
vinavochongwa sana kwa wakati huu ni kama vile milango, kabati, meza na vitu,
vyetezo, henga za viatu na mapazia, dressing table, shokesti, vitanda, stuli na
vibao vya mikate na vya kukalia. Vitu hivyo ni bidhaa nzuri na pia hutokana na asili ya utamaduni wa mswahili
pia ni vyenye kuendana na wakati tulionao.
Picha n.8.4. uchongoji wa samani.
vi.
Sanaa ya uchoraji
Sanaa hii ya uchoraji imepamba moto kwa sasa na
kuwapa vijana ajira kwa kuchora michoro mbali mbali na Kuingiza kipato katika
kazi hizo, watu hao hujishughulisha na kuchora michoro tofauti kwa maandishi na
picha. Huchora katika maduka nguo hasa shati za skuli na mpirani na hata shati
za sherehe za serikalini, pia huchora katika mahoteli na mikoba.
Pia kuna uchoraji wa piko ambao huchorwa watu wenye
shughuli, maharusi na watoto katika kusherehekea skukuu za iddi. Ambapo michoro
hio ni tofauti na michoro ya zamani. Pià katika zama hizi watu huchora tatuu
katika mwili ambapo tatuu hizo hukaa kwa muda mrefu au hata maisha yote katika
ngozi bila kufutika ambapo suala hili ni tofauti na utamaduni wa Zanzibar.
Picha.n.8.5 mikoba iliyochorwa picha
vii.Sanaa
ya ufundi
Katika sanaa ya ufundi watu hutengeneza vitu vingi
sana vikiwemo ufundi wa umeme, ufundi wa simu, majiko ya umeme. taa na mafeni,
ufundi wa vyombo vya usafiri pamoja na ujenzi.
Picha.8.6.
inaonesha ufundi seremala
viii.
Sanaa ya upambaji
Upambaji ni nyenzo ya sanaa inayofanywa na jamii ya
watu wa Zanzibar. Upambaji hufanyika katika kupambamaharusi, kupamba nyumba,
maholi na masteji katika shughuli. Upambaji wa kipindi hiki ni tofauti na
upambaji wa miaka ya nyuma (1964-1999). Hivi sasa upambaji umetanuka sana
kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, ambapo hata dhana hizo za
kupambia zimebadilika.
Picha.n.9.0.inonesha mapambo ya harusi.
ix.Sanaa
ya ufinyanzi
Ni sanaa ambayo hutengeneza vitu kwa kutumia udongo.
Sanaa hii hadi leo bado inafanyika hasa katika vijiji kama Muyuni na Muungoni.
Watu hao hutengeneza vitu kama vile mikungu, vyetezo, mitungi, vyungu na hata
majiko ya mkaa yenye asili ya vyombo vya uswahilini. Ingawa kutokana na sayansi
na teknolojia sanaa hii imepungua kutokana na kuwepo kwa uingiaji wa vyombo vya
bati, kaure na vya kisasa.
Picha.n.9.1. vyombo
vya ufinyanzi.
x.
Sanaa ya udarizi
Pia katika kipindi hiki utamaduni wa mswahili wa
Zanzibar umeweza kuimarika kupitia udarizi wa vitu na mitindo tofauti ambayo
watu wakiibuni. Miongoni mwa udarizi huo ni mashuka, mapazia, kanzu, kofia na
mazulia.
Picha.9.2. inaonesha udarizi mashuka
12.1
MAVAZI YA SASA
Mavazi ni miongoni mwa stara ambazo waswahili wa
sasa wanayatumilia kuvaa kwa lengo la kujistiri milli yao. Mavazi hayo ni jambo
la kawaida sana kumkuta mwanamke na mwanamme wa zama hizi kuvaa ukilinganisha
zama zilizopita kwasababu mavazi hayo yanatofautiana sana katika mionekano yao
namna inavyoonekana. Japo kuwa mavazi ya
sasa ni yenye gharama sana lakini wanajamii wanayatafuta kwa hali na mali ili
kuyavaa katika harakati zao za kila siku. Hivyo na kupelekea mavazi hayo
kubadilika mionekano yake siku hadi siku zinavyoenda katika ulimwengu.
Pia mavazi
hayo kubadilika kulingana na wakati namna unavyokwenda na humpa taswira mtu
tofauti pindi anapoyavaa. Kwasababu kila
vazi linapovaliwa linaleta taswira yake na umuhimu wake katika jambo fulani
inaweza kuwa vazi hilo mtu akivaa ikawa naenda harusini, mazikoni hospitalini,
mashuleni, kondeni, kazini na kadhalika kulingana na mtu vazi alilovaa hivyo
humtambulisha namna kitu anachokifanya.
Vilevile mavazi ni moja ya njia wapo ambayo
humtambulisha mtu sehemu anayotoka kwasababu ya tofauti ya mavazi hayo. Kuna
aina mbali mbali za mavazi katika ulimwengu mavazi hayo ni kama vile mavazi ya
kihindi, mavazi ya kiarabu kama vile kanzu na kofia , mavazi ya kichina ,
mavazi ya kizungu ambao mara nyingi huvaa suruali na flana katika harakati zao
mbali mbali za kila siku pia kuna mavazi ambayo wanavaa waswahili ambayo
yameletwa na wageni mbalimbali ambao walikuja kitawala katika upwa wa Afrika
Mashariki ambapo walipoondoka wakatuachia mavazi hayo ambayo waswahili wa sasa
wanayatumilia kuvaa katika shuguli zao mbali mbali kama vile makazini ,
mashuleni , maharusini , mikutanoni katika mambo ya kisiasa , misikitini ambapo
mavazi yake ni kanzu na kofia ambazo zimeletwa na waarabu walipokuja katika
upwa wa Afrika Mashariki na mavazi hayo huvaliwa kwaajili ya kuabudu na
kujifunza elimu na pia hutumika katika shughuli za kindoa kwa waisalamu na
sherehe kama za kusherehekea Eid elfitr ambapo waislamu takribani wote huvaa
wakubwa kwa wadogo kwaajili ya sherehe hizo.
Kwa upande wa wakristo wao hupendelea kuvaa vazi la
suti ambalo limeletwa na Waengereza wakati walipokuja kutawala katika mwambao
wa Afrika Mashariki ambapo vazi hilo hutumika katika shughuli zao za kindoa na
sherehe mbali mbali kama vile krismasi , siku za kwenda kuabudu na kadhalika.
.
Picha.n.9.3.inaonesha mavazi ya sasa.
Huu ni mfano mmoja wapo ambao wanajamii wa wakati
huu wanavaa katika harakati zao za kila siku kabla ya hapo zamani kulikuwa
hakuna mavazi haya ispokuwa walikuwa wanavaa makaniki pamoja na mabaibui ya
nyuzi katika shughuli zao tofauti.
Picha.n.9.4.inaonesha baibui la sasa.
Kutokana utandawazi ulioingia ulimwenguni umepelekea
watu sasa hivi kutokuvaa mabaibui yao kiasili ya kiutamaduni waswahili na kuvaa
mabaibui ambayo yameletwa na wageni mbalibali kama vile waarabu, wazungu na
hata wachina.
Pia mavazi ya
sasa yako mengi sana ukilinganisha na ya zamani ambayo yapo ya kitoto na ya
kijitukizima mbali mbali kama vile:
Mfano wa mavazi wanayovaa wanaume wakati wa sherehe
kama vile harusi au sherehe za Eid ni kama yafuatayo:
Picha.n.9.5.mavazi ya ulimwengu mpya.
Pia Kuna mavazi tofauti tofauti ambayo sasa
yanavaliwa lakini zamani ilikuwa hayapo kutokana utandawazi ulioingia
ulimwenguni umepelekea watu sasa wanayatumilia kuvaa kwa ajili ya malengo yao
tofauti tofauti ambayo huvaliwa na wanawake wanapokwenda maharusini, makazini,
maofisini nakadhalika mfano wa mavazi hayo ni kama yafuatayo:
Picha.n.9.6.mavazi ya kizazi kipya.
Pia kuna mavazi ya kisasa mbayo huvaliwa na watoto
katika harakati tofauti tofauti za kijamii lakini zamani ilikuwa mavazi hayo
hayatumiki. Mfano wa mavazi hayo ni kama yafuatayo,
Picha.n.9.7. inaonesha mishono ya sasa.
Vile vile
watoto wa kiume wa sasa yapo mavazi ambayo wanayatumilia kuvaa lakini zamani
pia yalikuwa hayatumiki. Mfano wa mavazi hayo ni kama yafuatayo;
Picha.n.9.8.inaonesha mavazi ya kizazi cha sasa.
Kutokana
utandawazi uliyongia ulimwenguni sasa umepelekea wanajamii kuyaacha mavazi yao
ya kiasili na kufuata utamaduni wa kigeni na kuacha mavazi ya tamaduni zao za
kiswahili ambapo japo kuwa mavazi kuonekana kuwa na ubora zaidi kuliko na ya
kale lakini mavazi hayo ni ya gharama zaidi ukilinganisha na ya zamani ambayo
ndio ya kiasili zaidi.
Hivyo mavazi
pia yamepelekea kudumaza kwa kiwango kikubwa utamaduni wa mswahili baada ya
kuja utandawazi ambao umedhoofisha utamaduni wa mswahili hivyo hatuna budi
kuyaenzi mavazi ya zamani ili kuudimisha utamaduni wetu wa mswahili vijijini na
hata mijini
12.2 ELIMU
Elimu ni ujuzi fulani ambao mtu hupata ujuzi huo kwa
kusomea au kujifundishia. Utamaduni wa kupata elimu umekua ukitofautiana kwa
kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma iliopita. Elimu kwa sasa imekua
ikitolewa kwa njia moja tu ukilinganisha na utamaduni wa zamani ambao ulikua
ukitolewa kwa njia tofauti; mfano wa njia zilizozikitumika zamani ilikua ni
njia ilio rasmi na njia iliokua sio rasmi. Njia iliokua sio rasmi watoto
walikua wakikusanywa kwa ajili ya kupewa elimu kwa vikundi kama vile elimu ya
kijinsia, mila, utamaduni nakadhalika.
Njia ilyokua rasmi. Hii ni njia ambayo watoto
walikuwa wakipelekwa mashuleni kwa ajili ya kupatiwa elimu itakayoenda
kuwakomboa katika maisha yao ya kila siku. Idadi ndogo sana ya wanafunzi
ilonekana katika mashule hii ni kutokana na kukosa hadhi kwa wakati huo
kulingana na utamaduni wao.
Kwa sasa utamaduni wa kupatiwa elimu umekuwa
ukitumia njia moja tu ambayo ni njia rasmi. Utamduni wa kupata elimu kwa sasa
umekuwa suala la msingi kwa sasa ambapo watoto huanzia ngazi ya maandalizi
mpaka kufika kidato cha nne kama ni elimu ya lazima kwa zanzibar. Vile vile
ongezeko la wanafunzi limekua kwa sasa ukilinganisha na miaka iliopita nyuma;
hii ni kutokana kwa kuonekana elimu ni kitu muhimu katika maisha ya kila siku.
Pia katika elimu ya Zanzibar somo la kiswahili limekua kama ni somo moja wapo
ambalo ni la lazima katika masomo yake ili kuendeleza na kukuza utamaduni wa
Kiswahili.
Pia uboreshaji wa miundo mbinu ya kielimu imekua kwa
kiasi kikubwa kulinga na idadi ya wanafunzi maskulni, skuli tofauti kubwa za
ghorofa kama ni maskuli ya kisasa kumekuwa na ongezeko kubwa la madarasa ya
kujifunzia, vikalio, madaftari ya kujisomea, n.k
Pia idadi ya vyuo vikuu vimeongezeka kutoka idadi
chache na kufikia idadi kubwa ya vyuo hivo , jambo hili la kuenda vyuo vikuu
limefika idadi kubwa ya wanafunzi ambao wanajiunga na vyuo hivyo kama ni
utamaduni wao wa zanzibar. Vile vile idadi ya wafundishaji katika sehemu za
kutolea elimu ukilinganisha na hapo awali. Ubora wa elimu uinayopatika kwa sasa
imekua na hadhi kubwa na kuzalisha watu walio bora na ufanisi mkubwa wa
kazi.
Mfano wa wanafunzi wa sasa wanavopata elimu wakiwa
katika maeneo ya kujifunzia.
Picha.1.0.
inaonesha elimu ya sasa.
13.1 MILA NA ITIKADI
ZA SASA.
Waswahili wengi wa Zanzibar wamekuwa ni wenye
kuzitupa mkono mila na desturi zao walizokuwa nazo jambo ambalo limepelekea
kuharibu utamaduni wao. Mfano kuoga mwaka katika jamii nyingi za wazanzibari
mila hii wameziacha kabisa na kutokutekelezwa haswa na kupelekea kudhorota kwa
tamaduni zetu.
Vilevile kutokana na Zanzibari kuendelea kukua na
kuongezeka kwa idadi ya watu wake basi waswahili wa zanzibar wamekuwa si wenye
kuzifuata tena itikadi zao na zengine kupotea kabisa. Ingawa kabla na tangu
mapinduzi waswahili wa zanzibar walikuwa ni wenye kufuata itikadi za jamii zao
pamoja na zile za dini ya kiislamu na kikristo lakini kila miaka inavyozidi
kwenda ndipo mambo hubadilika na kwenda na wakati huo.
Tangu Karne ya 20 mpaka sasa waswahili wa zanzibar
wameziacha itikadi zao walizorithi kutoka kwa mababu zao na wengine ndio haswa
imani za kidini pia kuzipuuzia. Na sasa wengine wao wamekuwa ni wenye kuishi
kulingana na mfumo wa utandawazi na maendeleo ya sayansi
na teknolojia jambo ambalo limezidi sana kukandamiza
itikadi na utamaduni wa waswahili kwa ujumla, hivyo kufuata mfumo kutokana na
wakati na wageni katika nchi ya Zanzibar.
13.2
VYAKULA
Utamaduni wa
mswahili katika ulaji hapo awali kulikua na vykula vingi vya asili ambavyo
walikua wakitumia ikiwemo mabobwe, manda nk. Utamaduni huu wa ulaji wa vyakula
vya asili umekua tofauti na sasa kutokana na maendeleo na makuzi ya nchi na
kupelekea waswahili kula vykula vya kisasa ambavyo ni tofauti na vya zamani.
Mfano utamaduni wa sasa wa ulaji kwa waswahili umejikita zaidi katika vyakula
vya aina ya protini na mafuta ukilinganisha zamani ambapo wakitumia sana
nafaka, majani na kadhalika.
Katika utamaduni
wa mswahili umepekea madiliko makubwa katika upishi na ulaji wa vyakula na
kupelekea kuacha kutumia mbinu za upishi na ulaji wa vyakula ambavyo
huwatambulisha waswahili, hali hii hutokezea kutokana na maendeleo ya sayansi
na teknolojia. Mfano kutumia nyama za kutengeneza kama vile peduu badala ya
vitoweo vya baharini, kutumia mafuta kwa wingi badala ya nazi kama vile wali wa
mafuta, mchuzi wa mafuta na nyama kwa wingi.
Kutokana na hali
hii imepelekea kupotea kwa utamaduni wa zamani wa vykula kwa Waswahili.
Picha hapo chini
inaonesha jinsi utamaduni wa sasa wa Waswahili katika vyakula vyao ambapo sana
hutumia mafuta kuliko nazi ambayo ni asili kwa Waswahili.
Picha.10.1.inaonesha
vyakula.
i.Vyakula vya kisasa
Hata hivyo
Waswahili katika utamaduni wa chakula kwa kipindi hichi cha sasa hupendelea
zaidi kutumia vitoweo vya kisasa ukitoa vile vya asili vya baharini na kutumia
zaidi vinavyotengenezwa viwandani kutokana na maendeleo ya kisayansi na teknolojia
kama vile kuku aina peduu, nyama za kutengeneza viwandani na kadhalika.
13.4
MAADILI YA SASA
Kuanzia Karne
ya ishrini (20) maadili yalianza kutoweka kidogo mpaka kufikia sasa Karne ya
ishrini na moja (21) ambapo maadili hayo ya utamaduni wa mswahili yalibadilika
kutokana na maingiliano ya sayansi na teknolojia. Jambo hilo kupelekea maadili hayo kupotea kwa
kiwango kikubwa. Na kutokana na maingiliano ya sayansi na teknolojia watu wa
sasa katika zama hizi kuiga maadili ya kigeni ambapo wanaenda kinyume na
maadili yao na kusababisha maadili kupotea. Mfano ni watu kuvaa nguo ambazo
hazina maadili na utamaduni wa mswahili
Picha.10.2.mavazi ya vijana wa sasa.
Vile vile Kuna mitindo mbali mbali ya mikato ya
nywele ambayo mitindo hiyo hapo zamani ilikuwa haitumiki lakini kutokana na
utandawazi ulioingia ulimwenguni sasa vijana wakiume wanakata mitindo hiyo ambayo ni kinyume na maadili yao ya
mswahili. Mfano wa mitindo hiyo ni kama ifuatayo:
Picha.10.3.inaonesha mikato ya vija wa sasa.
Pia wanawake wanasuka mitindo mbali mbali ambayo
imeletwa na wageni mbalimbali na kutokana na utandawazi ulioingia ulimwenguni
umepelekea wanawake hao kuacha maadili ya misuko yao ya utamaduni wa msw ahili.
Mfano wa mitindo hiyo ni kama ifuatayo:
Picha.n.10.4.mitindo tofauti ya misuko ya wanawake.
Pia wanawake wanaenda kinyume na maadili ya mavazi
ya zamani ambayo yana stara na heshima kwasababu una uwezo wa kuvaa popote
lakini kutokana na utandawazi uloingia ulimwenguni sasa vijana wa kike wanavaa
nguo za mibano ambayo haziendani na utamaduni wa maadili ya mswahili.
14.1 UCHUMI WA WATU WA ZANZIBAR
WASASA.
Uchumi wa Zanzibar umekuwa ukibadilika na kuendelea
kukua kutokana na maendeleo ya sayansi katika njia kadhaa. Matumizi ya
teknolojia, mawasiliano, na mifumo ya usafirishaji yamechochea mabadiliko
makubwa. Hapa chini ni baadhi ya mambo yanayo pelekea mabadiliko na maendeleo
ya uchumi wa Zanzibar:
i.Mawasiliano
Kuongezeka
kwa upatikanaji wa simu za mkononi na intaneti Zanzibar kumeleta mapinduzi
katika jinsi biashara inavyofanyika. Wafanyabiashara sasa wanaweza kuwasiliana
kwa urahisi na wateja wao, kufanya biashara mtandaoni, na kufuatilia mwenendo
wa soko la kimataifa.
ii.Teknolojia
ya Kilimo
Maendeleo katika teknolojia ya kilimo kama vile
matumizi ya mbolea za kisasa, mifumo ya umwagiliaji, mbinu za kilimo endelevu
zimeboresha uzalishaji na ubora wa mazao Zanzibar, hivyo kuongeza fursa
mbalimbali kupitia mazao ya kilimo na kusababisha uchumi kukua.
iii.Usafirishaji.
Uboreshaji wa miundombinu ya usafirishaji kama vile
bandari, barabara, na viwanja vya ndege umefungua fursa za uzalishaji kwa watu
wa Zanzibar. Usafirishaji wa haraka na salama unarahisisha uagizaji na
usafirishaji wa bidhaa, hivyo kukuza kipato cha nchi.
Picha.n.10.5.inaonesha usafiri wa sasa waswahili.
vi.Ufugaji
na viwanda.
Sayansi imechangia sana katika kuboresha sekta ya
ufugaji na viwanda Zanzibar. Kupitia matumizi ya mbinu za kisayansi, wafugaji
na wawekezaji wa viwanda wamefaidika na maendeleo makubwa katika uzalishaji na
ubora wa bidhaa zao. Katika sekta ya ufugaji, sayansi imesaidia kuboresha
mifugo iliyopo na kuongeza uzalishaji wake. Kwa mfano, kuzaa kwa njia ya
kisayansi imesaidia kuzalisha mifugo yenye sifa nzuri za utumiaji, uzalishaji
wa maziwa, na nyama. Wanasayansi pia wamefanya utafiti wa lishe bora na mifumo
ya usimamizi wa afya ya mifugo ili kuongeza uzalishaji wao.
Picha.10.6.inaonesha ufugaji wa sasa wa waswahili.
Kwa upande wa viwanda, sayansi imeongeza ufanisi na
ubora wa bidhaa. Mbinu za kisayansi zimeboresha mchakato wa uzalishaji kwa
kufanya tafiti za kisayansi na kuweka mazingira bora ya utengenezaji wa bidhaa.
Pia, teknolojia za kisasa zimekuzwa na kutumika katika viwanda vya Zanzibar,
kama vile teknolojia ya usindikaji wa chakula na utengenezaji wa vifaa vya
kisasa.
14.2
MSIBA WA SASA.
Mzee MWITA MASEMO MAKUNGU wa makunduchi tarehe
25/4/2024 katika mahojiano ya Waswahili wa sasa wakati wa msiba alisema kuwa
waswahili wasasa wanaonekana kwa kiasi kikubwa kuwa na mabadiliko ya utamaduni
waliokuwa nao na kujiingiza katika utamaduni unaotokana na wageni katika suala
la misiba. Waswahili wa leo wakati mtu anapofariki, hukusanyika kama kawaida,
lakini kuna mambo kiutamaduni yamebadilika kama yafuatayo:
Kulipishana wakati wa kuchimba kaburi la maiti;
Uchimbaji wa makaburi kwa sasa kuna watu maalumu wanaohusika na masuala hayo,
hivyo watu hulipishwa ili wachimbiwe kaburi kwa ajili ya kumstiri maiti wao.
Hitima na dua baada ya mazishi kwasasa jamii nyingi
za waswahili zimeacha utamaduni huo. Hivyo, baada ya watu kumzika maiti
hutawanyika.
Wanaofanya matanga hujikusanya na kuona kuwa katika
siku tatu zile wamepata sehemu ya
kujistiri ( Yani kupata chakula).
15.1
SHEREHE NA MICHEZO YA SASA KATIKA TAMADUNI ZA KIZANZIBAR.
Wazanzibar wanatekeleza sherehe mbali mbali ambazo
zinatekelezwa katika kuudumisha na kuuwenzi utamaduni wao, miongoni mwa sherehe
ambazo zinatekelezwa na wana jamii wa Zanzibar ni pamoja na hizi zifuatazo.
i.Sherehe
za Harusi. Harusi ni miongoni mwa sherehe ambayo ndani yake
imeonekana kwa kiasi kikubwa kuwa inaendeshwa Katika jamii zetu za Zanzibar,
sherehe hizi za Harusi zinaambatana na tamaduni nyingi za sasa au za wakati huu
wa muelekeo wa sayansi na teknolojia miongoni mwa tamaduni hizo ni pamoja na.
Wazanzibari wa sasa wana tamaduni ya kuwaalika watu
katika sherehe zao kwa kutumia kadi maalumu; Kadi ambazo zitawatambulisha kuwa
wao ni watu halali walioalikwa katika sherehe hiyo hiyo ya harusi. Kwa namna
hii watu hupewa mualiko ili wahudhurie katika shughuli hiyo, Jambo ambalo lina
sababisha mgawanyiko wa wana jamii kwa kiasi kikubwa kwa sababu inakuwa na
ubaguzi ndani yake kwani hasa hasa kadi hupatiwa watu wa tabaka la juu na
kuachwa watu wa tabaka la chini jambo ambalo kiuhalisia hasa watu wa tabaka la
chini ndio wenye shida na mahitaji mengi katika maisha yao.
Pia sherehe
za Harusi za wakati huu zinaambatana na vazi maalumu lenye kufanana kwa
wanawake (VIJORA). Vazi hilo kwa upande mwengine linaitwa sare ambazo huamuliwa
na upande wa kike kwa kila mmoja anatakiwa awe amepata sare hiyo ya kijora kama
wanavyo iita kutokana na mazoweya yao. Hii ni miongoni mwa tamaduni zilizo anza
hivi karibuni unaoonekana kutekelezwa katika sherehe nyingi za harusi za
Zanzibar.Wanawake wanakuwa na umoja na mshikamano katika hilo, kutokana na
umoja wao wanasababisha harusi kuwa na sura yenye mafanikio kwao. Vazi hilo la
kijora linakuwa na mtandio ambao unakuwa na rangi iliyofanana sawa na kijora.
Picha.10.7.inaonesha vazi la vijora wanavyo vaa waswahili.
Aina ya kwanza ya vazi
hilo la kijora na wakati linaspovaliwa.
Aina hii
wanawake wanavaa wakati wa Asubuhi wa siku ya Harusi; Wanavaa kwa ajili ya kazi
ndogo ndogo za nyumbani ambako Harusi inafanyika kutokana na kazi hizo
zinazochukuwa nafasi wakati huo ni lazima kwa baadhi ya Harusi pawepo na vazi
maalumu litakalotawala wakati huo ili iwe rahisi kwa wakati huo kujuwa wanao
husika na shughuli hio.
Vazi la pili huvaliwa wakati wa kuchukuwa Harusi;
Huu ni wakati muhimu kwa wenye shughuli hii watu wanakuwa na sare maalumu
inayowekwa kwa ajili ya uchukuwaji wa Harusi. Mara nyingi unakuwa ni wa masafa
marefu kiasi kwamba haiwezekani kuvaa vijora ambavyo wameshinda navyo (kuvivaa)
tokea asubuhi hivyo basi wanabadilisha vazi hilo ili waweze kuwa na sura
nyengine pale wanpokwenda ugenini; Ambako wanakwenda kuchukuwa Harusi na pia
kwa Harusi ya kike inakuwa na hali hiyo hiyo ilimuradi tu waweze kuikamilisha
sherehe yao walioifanya.
Vazi la tatu linavaliwa wakati wa kwenda holini; Kwa
tamaduni nyingi za kizanzibar wanavaa nguo nyengine wakati wa kwenda holini
wakiwemo Harusi wa kike na Harusi wa kiume. Wanafanya hivyo pia ili kuuenzi na
kuendeleza utamaduni wao walionao sasa wakiachana tamaduni za zaman
zilizopitiwa na wakati.
Mashirikiano katika uchukuwaji wa harusi; Tamaduni
za sasa za kizanzibar zimekuwa zimekuwa zikifanywa na watu wenyewe kwa
kushirikiana wakati wa uchukuwaji wa harusi kwa wanaume na wanawake wanakodi
magari maalumu ambayo yanaweza kutumika wakati wa safari hizo. Mashirikiano
hayo yanaendelezwa kwa watu wote wa kinzanzibar, Hali hii ya mashirikiano
inapotekelezwa kikamilifu inapelekea kuuwenzi utamaduni wasasa wa kinzanzibar
ili uweze kubakia na kurithishwa kutoka kizazi hadi kizazi kwa namna hii, Na
kwa upande wa wanawake wanaambatanisha
safari hizo wakiwa na nyimbo za taarabu kwenye magari yao wanayopanda
kwenda kuchukuwa Harusi ambapo pia ndani yake wanakuwa na furaha kupitiliza
kiasi ambacho wanacheza muziki ndani ya gari huku gari ikiwa kwenye mwendo
mkubwa bila kukumbuka athari ambazo zinaweza kutokezea kwa kufanya hayo; Hali
hii hasa hasa kwa sehemu za mjini
inaonekana kwa kiasi kikubwa kuliko sehemu za vijijini.
Maharusi kupelekwa maholini; pia tamaduni za Sasa za
kizanzibari kwa baadhi ya wanajamii wanawapeleka maharusi wao katika holi
ambako wanafanya hivyo ili kuweza kufanya sherehe ya Harusi hiyo, inaweza kuwa
baada ya kurudi kuchukuwa Harusi au siku nyengine yeyote ya mbele kutoka siku
Ile ya Harusi, Wanakwenda huko, Sherehe hiyo ya holini inakuwa na waalikwa
mbali mbali, pia inajumuisha Wanaume, Wanawake, Wazee, Vijana na Watoto.
Shughuli hio pia inaambatana na muziki na baadhi ya kasida zinazoendana na
sherehe za harusi.
ii.Sherehe
za Maulidi, Maulidi pia ni sherehe zilizomo katika visiwa vya
Zanzibar Hivyo maulidi ni sherehe zinazoendelezwa kwa muda mrefu sana na Hivyo
sasa kwa kiasi kikubwa inaonekana kuwa, zimeshika hatamu kwa namna ambavyo
zinatekelezwa katika jamii zetu za sasa sherehe hizo zinaambatana na mambo
mengi yakitamaduni yakiwemo.
Maulidi ya
Harusi
Upigaji wa madufu: Wanajamii wa Sasa kwa kiasi
kikubwa wanaendeleza utamaduni wa kisasa hii inaendeshwa hasa katika sherehe za
harusi za wakati huu ambapo kuwa wanawake wanakuwa wanacheza uwanjani wakiwa na
sare zao walizozianda kwa ajili ya sherehe hiyo huku wakicheza kwa msongo na
furaha juu.
Maulidi ya kuzaliwa kwa mtume.
Pia katika tamaduni za sasa kuna fanyika Maulidi ya
kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W.) Maulidi hufanyika kila siku ya mwezi
12 mfunguo sita kila mwaka ambako watu wanashereheka kwa hali ya juu Maulidi
haya yanaweza kufanywa na watu wa mji na hata madrasa zilizomo ndani ya
Zanzibar na kuweza kufanya Maulidi hayo. Watu wa Miji wanafanya Maulidi ya Mji
kwa lengo la kuenzi utamaduni wa kizanzibar, Miji mbali mbali ambayo ni marufu
kwa ufanyaji wa Maulidi haya kwa kila mwaka ni pamoja na Kisiwa cha TUMBATU,
CHAANI, CHARAWE kwa UNGUJA, na CHAMBANI, MUAMBE, KOJANI, MAKANGALE, OLE KIANGA,
KIUYU MBUYUNI, MAZIWA NG'OMBE kwa upande wa PEMBA.
Na pia Madrasa mbali mbali zinaendeleza tamaduni hii
ya Maulidi mfano wa madrasa hizo ni madrasaat Kamaria, Al madrasaat Anuar ddin
Islamiyya, Al madrasaat Nnur islamila, zote hizo zinawaika watu vyuo mbali
mbali ili kusherehekea katika Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W.)
katika sherehe hii ya Maulidi, inaambatana na ratiba maalumu ambao unakuwa ni
muongozo mzima wa shughuli hii. Ratiba hii inakuwa na ufunguzi wa Qur'an
Tukufu, nasaha za Mwalimu Mkuu kwa wageni na wenyeji waliohidhuria katika
shughuli hio, Usomaji wa Kassida,Usomaji wa milango ya Maulidi, Usomaji wa
hadithi za Mtume (S.A.W) Mwisho ni ugawaji wa dhifa kwa wageni na wenyeji na
mwisho wa shughuli Dua ili kuomba kheir kwa Maulid hayo na baada ya hapo watu
wanarudi majumbani kwao kwa ajili
kuendelea na shughuli zao za kimaisha.
15.2
MICHEZO
Kwa upande wa
michezo pia ni tofauti kati ya ile ya kizamani na ya tamaduni za sasa; Michezo
ya kisasa ni kama vile:
Mchezo wa mpira wa miguu wa kisasa; Huu ni aina ya
mchezo ambao inajumuisha timu mbili na kwa kila timu moja inakuwa na Jumla ya
wachezaji kamili kumi na moja, wanakuwa na Jezi maalumu zinazowatofautisha
Wachezaji wa timu hizo mbili hii inawasaidia Wachezaji hao pamoja na washabiki
katika kujuwa wachezaji wake anaocheza nao katika mchezo na washabiki kujuwa
wachezaji wa timu anayoshabikia wakati wa mchezo huo. Mchezo huu unakuwa alama
tatu kwa kila mchezo atakapo funga goli, Lakini pia unakuwa na mabadiliko ya
wachezaji wakati ambapo mchezaji itatokea kachoka au kutokufanya vyema ndani ya
uwanja wakati mchezo unaendelea, Pia mchezo huu unakuwa na muda wa mapumziko,
Mapumziko ambayo yanawapa wachezaji kupata fursa ya kujipanga upya
kwa ajili ya mapambano ya awamu ya pili, Kwa sababu
viongozi wa timu wanatoa mafunzo ya kutosha dhidi ya wachezaji waweze kupata
mafanikio yalio mazuri katika mchezo mafanikio yenyewe ni kupata ushindi na
kuchukua alama tatu katika mchezo huo.
Mchezo wa riadha; Riadha ni mchezo ambao unachezwa
kwa kushindana wale wanao shiriki katika mchezo huo, mara nyingi mchezo huu
unakuwa na makundi wakati wa mshindano ambapo washiriki wanatakiwa kupanga
mstari uliosawa kwa ajili ya kuanza riadha, unachezwa katika viwanja vya mpira
wa miguu, makundi hayo yanazunguruka uwanja kulingana na makubaliano yao
waliokubaliana wenyewe ikiwa ni mizunguruko mitano au kumi itategemea na
wenyewe walivokubakiana.
Mashindano ya Baskeli; Mchezo huu unahusisha
washiriki mbali mbali ambao Wana uwezo wa kuendesha baskeli maeneo marefu.
Hivyo huekewa sehemu maalumu ambayo itatumika kwa ajili ya kuanzia safari ya
mashindano hayo na kuwekewa sehemu maalumu ya kufikia ili aweze kujulikana
mshindi ni nani na alieshindwa ni nani.
16.1
MAMBO YANAYO PELEKEA KUBADILIKA KWA UTAMADUNI:
Elimu.
Elimu ni moja kati ya mambo makubwa yaliosababisha
kupotea au kuachwa baadhi ya tamaduni. Kabla ya kuja kwa elimu watu walikuwa na
tamaduni zao, ambazo walikuwa wakizifuata, kwamfano kuabudia mizimu lakini
kwasasa asilimia tisiini Mungu ambae wanamuabudia kulingana na Imani zao.
Waislamu wao kwa Imani zao wanaamini kuwa mungu wakuabudiwa ni mmoja kwa viumbe
wote wala hana anaeshikiana nae katika mambo yake.
Vilevile wanaamini kuwa elimu au kitabu kilichobora
ni Qur’ani tukufu. Ambayo
iliteremshwa kuja kwao kama nimuongozo wao. Kwaupande wa wakristo wanaamini
kitabu cha Bibilia ambacho
aliteremshiwa yesu. Na hawa wako wanoamini mungu mmoja na mungu watatu.
Pia elimu ya kisaikolojia ilichangia kwa kiasi
kikubwa kubadilika kwa utamaduni. Waswahili waliowengi wanajihusisha na masuala
ya kutafuta elimu na kuacha utamaduni wa kupeana hadithi za kale elimu zisizo
rasmi. Elimu hii iliwabadilisha waswahili katika masuala mbalimbali kama vile:-
i.
Namna gani
wanatakikana walime katika mashamba yao ili kuweza kuzalisha kwa kuwango chajuu
na kupata mazao yalio bora kwa afya zao.
ii.
Vipi wanyama
wanatakikana wafugwe ili waweze kupatikana wakati wowote kwa matumizi ya
wanaadamu.
Teknolojia.
Teknologia ilipoingia katika miji ya waswahili
hususan Zanzibar imeathiri sana utamaduni wa mzanzibari. Teknolojia tunaweza
kusema kuwa nibaba wa mabadiliko ya haraka kutokana nakuwa watu wengi wanatumia
teknolojia katika mambo yao na maisha yao ya kila siku. Mambo yafuatayo
yanaonesha kuwa tekknolojia imeharibu ama kubadilisha utamaduni wa mswahili:-
i.
Matumizi makubwa
ya vyakula vya kisasa kama vile peduu. Teknolojia
imekuja na mfumo wa kuzalisha kuku kwa haraka na kutumika kama chakula.
Waswahli kwa kiasi kikubwa wanatumia aina hii ya chakula.
ii.
Teknolojia
imebadilisha namna ya uvaaji. Waswahili wasasa wameacha mavazi na namna ya uvaaji
wao wa asili. Na hii nikutokana na muingiliano wa sayansi na teknolojia.
iii.
Teknolojia
imesababisha kubadilika kwa mikato ya nywele. Ukiangalia vijana wasasa
wanamikato tofauti ukilinganisha na utamaduni wao.
Mahusiano
ya kimataifa.
Mahusiano ya waswahili na nchi nyengine yanachangia
kubadilika kwa utamaduni wa waswahili. Katika uhusiano kuna namna mbalimbali,
kama vile:-
i.
Kukubaliana
kuingiza bidhaa yoyote katika nchi. Kwa mfano uingizwaji wa madawa ya kulevya ,
hii husababisha kubadilika kwa utamaduni. Zanzibar ni nchi ilio na mahusiano na
nchi nyingi hivyo kulingana na makubaliano yanapelekea kuharibika kwa utamaduni
wa wazanzibar na kuingia utamaduni mwengine.
17.1
FAIDA ZA UTAMADUNI
Utamaduni wa watu wa zamani ulikua na faida nyingi
kama vile:
- Umoja na
ushirikiano; Utamaduni ulikua na nguvu katika Kuimarisha ushirikiano na
umoja kati ya watu wa jamii moja
- Heshima kwa wazee;
Utamaduni unafanya watu kuweka heshima kubwa kwa wazee na maarifa
Yao.Wazee waliheshimiwa kama viongozi na walikua na jukumu muhimu katika
kusimamia jamii.
- Ulinzi wa
mazingira; Utamaduni ulikua na mifumo ya kuhifadhi mazingira na rasilimali
za asili.
18.1
HASARA ZA UTAMADUNI
Miongoni mwa hasara za utamaduni ni kama zifuatazo:
- Kupotea kwa lugha
na Mila; Utamaduni unakabiliwa na hatari ya kupotea kwa lugha za asili na
Mila kutokana na mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.
- Kuathiriwa kwa
teknolojia; Maendeleo ya teknolojia yameathiri utamaduni kwa njia nyingi
ikiwa ni pamoja na kusababisha kupotea kwa mazoea ya kiutamaduni na kuleta
mabadiliko katika mawasiliano na mahusiano ya kijamii.
- Mmonyoko wa
maadili; Utamaduni unakabiliwa na changamoto ya mmonyoko wa maadili kwa
jamii ambao unaweza kusababisha migogoro na vitendo viovu katika jamii.
HITIMISHO
Makala hii imelezea kwa
kina kihusiana na utamaduni wa mswahili baada ya mapinduzi ya 1964 hadi
2024.katika kipindi hichi utamaduni wa watu wa Zanzibar ulipitia katika vipindi
mbalimbali. Vipindi hivo ni kipindi cha mwanzo wakati Mzee Abeid Amani karume
baada ya mapinduzi matukufu 1964 alipowaelekeza waswahli waendeleze utamaduni
wao na kuuboresha katika vipengele mbalimbali kwa mfano Maadili, vyakula,
Elimu,Siasa nakadhalika. Kipindi cha pili niwakati teknolojia iliposambaa zaid
ndani ya Zanzibar.Hapa Utamaduni ulibadilika kwa kiasi kikubwa, mila, desturi,
maadili, vyakula, mavazi, Sanaa, na hata tabia za watu zimebadilika kwa
asilimia 80% ,licha ya kuwa baadhi ya sehemu bado watu wanayaendeleza.
Cha muhimu ni kuwa
waswahili wasiwe niwenye kukubali kirahisi kupokea utamadu ambao unaharibu
heshima na maadili ya wazanzibari.kwani kwa kufuata mambo yanayoletwa na watu
wengine ndio sababu inayopelekea kupotea kwa utamaduni wetu. “usiache mbachao
kwa masala upitao” na tukumbuke “mkataa kwao mtumwa”.
Baraza la kiswahi la
Zanzibar. (BAKIZA). (2008).Utamaduni wa mzanzibar. Zanzibar.Baraza la
Kiswahili la Zanzibar.
Kamisheni ya utamaduni
na michezo. (2012).hazina inayopotea :bodi ya sensa ya filamu na sanaa
mchezo. Chukwani Zanzibar.
Ministry of
information, culture, tourism and sport. (2013).commition of
culture:inventory of intangible cultural heritage .Zanzibar ,UNESCO;
Zanzibar Tanzania.
Mzee Mwita M asebo
Makungu. (2024). Historia ya Utamaduni wa Makunduchi. (Mahojiano ya ana
kwa ana). Makunduchi, Zanzibar.
Wizara ya elimu
utamaduni na michezo. (2005).Sera utamaduni wa Zanzibar .serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar .Zanzibar.
0 maoni:
Post a Comment