Imeandikwa na Mtila Mswahili
UTANGULIZI
Maana ya utamaduni
Ali M. Rashid (2012)
anaeleza kwamba, neno utamaduni lina asili ya lugha ya kiarabu ambalo
maana yake ya msingi ni “dini”; anaeleza kwamba baada ya kutoholewa na
kuingizwa katika lugha ya kiswahili lilichukuliwa umbo la utamaduni na baadae
kusanifishwa na kuwa utamaduni.
Anahitimisha kwa kusema neno utamaduni lina maana ya mfumo mzima
unaofuatwa na mwanadamu katika maisha yake ya kila siku.
Pia williams (2010) ameeleza
kuwa utamaduni ni njia ya maisha, sanaa na nyenzo zenye kutoa maana.
Omar (1981 : 3) akimnukuu Tylor anasema kuwa utamaduni ni maisha ya
mwanadamu ambayo yana ufahamu wa elimu, imani, sanaa,maadili, mila, sheria na
desturi.
Utamaduni wa mswahili ni utaratibu wa jumla uliowekwa na waswahili
ili kuufuata utaratibu huo.
Maana ya mswahili, kwa mujibu wa Kamusi la kiswahili fasaha lililoandikwa na BAKIZA
Mswahili ni mtu mwenye asili ya mwambao wa Afrika Mashariki na
ambae lugha yake ya awali ni kiswahili na hufuata utamaduni wake
Pia Flora Mallema, Mwenyekiti wa Chama Cha Lugha Na Fasihi Ya
Kiswahili Tanzania anasema, mswahili ni mtu ambaye anafanya mambo ya kiswahili,
anazungumza kiswahili na mambo yafananayo na uswahili.
MSWAHILI WA ZAMANI AU MSWAHILI HALISI
Ni mtu mwenye asili ya pwani ya Afrika mashariki ambaye maisha yake
yalitawaliwa na mila,desturi na utamaduni wa Mswahili. Huyu ni mtu ambaye
maisha yake yalihusiana moja kwa moja na ustaarabu na tamaduni zote za
mswahili. Mswahili halisi alikuwepo kabla ya ujio wa wakoloni . Kiswahili kichotumika na mswahili wa zamani kilikuwa
halisi na kimejaa misemo, methali na
maneno ya heshima
MSWAHILI WA LEO;
Ni mtu wa jamii ya kiswahili anayeishi
katika muktadha wa kisasa, akichanganya maisha ya kiutamaduni na athari za
maendeleo ya kiuchumi, kijamii, kiteknolojia na kiutandawazi. Huyu ni mtu
ambaye bado anaweza kuwa na mizizi ya kiutamaduni ya mswahili,lakini maisha
yake yameathiriwa na mabadiliko ya ulimwengu wa sasa.
SIFA
ZA UTAMADUNI WA MSWAHILI
Utamaduni wa mswahili una
sifa ya kuwagawa watu katika makundi. Utamaduni wa mswahili huigawa jamii
katika makundi mfano wanaume huhusika na masuala ya kutafuta rizki, wanawake
shughuli za nyumbani na watoto madrasa.
TATHMINI
Waswahili wa sasa huingiliana katika majukumu mfano zamani ilikuwa
suala la uongozi wa jamii ni la wanaume lakini sasa hata wanawake pia ni
viongozi wa jamii. Pia katika shughuli za kutafuta rizki lilikuwa ni la wanaume
lakini waswahili wa sasa wanawake pia hujishughulisha na harakati za kutafuta
rizki mfano kubeba zege nakadhalika.
kuna matabaka mingi ya kidini ambayo kila siku yanaleta migogoro
katika jamii.Na kuhusu mashirikiano ya kijamii hayapo kutokana na sasa kila mtu na familia yake. Kwa hivyo
tunaona ni kwa kiasi kikubwa waswahili wa leo hawafuati utamaduni wa zamani
unaoleta mashirikiano na umoja ndani yake.
2) Utamaduni wa Mswahili una sifa ya kubadilika kulingana na
mabadiliko ya wakati na kukua kadri nyakati zinavyosonga. Hii ina maana kuwa
Mswahili hajafungwa na mila au desturi zisizobadilika
bali huwa na uwezo wa kuchukua vipengele vipya kutoka kwa jamii
nyingine au kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, ilimradi visiathiri maadili
ya msingi ya utamaduni wake kama vile heshima, utu na mshikamano wa jamii.
mifano
kutoka kwa mswahili wa zamani.
Mavazi: Zamani, Mswahili
alivaa khanga, kanzu, na buibui. Alipokutana na Waarabu na Waajemi, mavazi hayo
yaliboreshwa – mfano: kanzu ya Kiomani au buibui ya kihijabu.
Lugha: Kiswahili kilianza kama lugha ya jamii ya Pwani, kisha
kikachukua maneno kutoka Kiarabu, Kireno, Kiingereza na Kijerumani, na hivyo
kuendelea kukua bila kupoteza kiini chake.
Sanaa: Muziki wa Taarab
ulianza kama wa Kiarabu lakini ukaboreshwa na ladha za Kiafrika na Kiswahili
TATHMINI
KWA MSWAHILI WA SASA:
Mswahili wa sasa anaendelea kuendana na sifa hii ya kubadilika,
lakini kwa kiwango kinachohitaji tahadhari. Mfano:
Mavazi – Mswahili wa sasa huvaa mavazi ya kisasa kama jeans au
t-shirt, lakini wengine bado wanavaa kanzu au khanga katika hafla za heshima.
Teknolojia – Mswahili wa sasa anatumia simu na mitandao ya kijamii kusambaza mashairi, ngoma, au hadithi – njia mpya ya kudumisha sanaa ya zamani kwa mitindo ya kisasa.
Utamaduni wa Mswahili una sifa ya kurithishana amali za jamani
kutoka kizazi hadi kizazi. Utamaduni wa mswahili huwawezesha waswahili
kurithishana;
Mila na Desturi: Jamii ya Waswahili ina mila nyingi ambazo zimekuwa
zikirithiwa, kama vile sherehe za ndoa, maulidi,mazishi, sherehe za jando na
unyago ngoma za asili na matukio mengine ya kijamii. Hizi ni sehemu muhimu ya
utambulisho wa jamii na husaidia kuimarisha mshikamano
- Mapishi na chakula:
Mapishi kama vile makopa, msambwija, vipopoo wali na vyakula vyengine. Hii si tu njia ya kuendeleza utamaduni bali
pia huonesha utambulisho wa Mswahili.
Sanaa: Sanaa za Waswahili kama vile uchoraji, uchongaji, na muziki
ni sehemu muhimu ya utamaduni wao. Waswahili hutumia sanaa hizo ili kuendeleza
urithi wao wa kifasihi na kisanaa.
Waswahili wa sasa hurithishana amali za jamii kwa kiwango khafifu
sana. Mfano katika mavazi kwa asilimia
ndogo wamerithishana.
Sanaa na miziki. Waswahili
wana mziki na sanaa walizozirithi mfano
wa sanaa hizo ni ngoma za msewe, ngoma za kibati nakadhalika
Lakini waswahili wa sasa ni
kwa asilimia ndogo sana wanasikiliza ngoma hizi kutokana na maendeleo ya
sayansi na teknolojia.
4) Utamaduni wa Mswahili una sifa ya kufungamana na dini ya
kiislamu. Utamaduni wa mswahili na dini ya kiislamu ni kama sarafu moja,
waswahili hufata mila na taratibu za kiislamu kama kuswali, kufunga,
kuhiji,kusoma Qur an na pia kuvaa mavazi kama vile shungi, baibui na kofia
Pia katika taratibu za
kula mfano kula kwa mkono wa kulia ni sheria ya kiislamu na ni moja ya taratibu
za utamaduni wa mswahili.
TATHMINI
Kutokana na jambo hilo tunaona kwamba waswahili wa sasa bado
wanafata utamaduni huu, hivyo wanaendana mno na sifa hii.
5) Utamaduni wa Mswahili una sifa ya kuwa na miiko juu ya mambo
fulani. Mfano mwanamke akiwa mjamzito ni mwiko kula mayai, mtoto akizaliwa atakuwa hana nywele, ni mwiko kukata kucha usiku,
ni mwiko chumvi kuita chumvi kwa wakati wa usiku na iitwe dawa ya jiko au
mkubwa wa jiko,pia ni mwiko kukata
nywele usiku nakadhalika.
TATHMINI
Waswahili wa zamani walikuwa wanafuata vyema na kuheshimu miiko
iliyowekwa lakini waswahili wa sasa kwa kiwango kikubwa hawaheshimu miiko mfano
suala la kukata nywele usiku, kula mayai kwa wajawazito, kukata kucha usiku na
mambo mengi waswahili wa sasa huyafanya licha yakuwa mambo hayo ni miiko
6) Utamaduni wa mswahili una sifa ya kuwafanya
waswahili wawe na umoja na ushirikiano. Katika masuala mbalimbali waswahili
huwa pamoja kwa kushirikiana kutokana na namna ambavyo utamaduni ulivyo mfano
katika chakula familia hukusanyika pamoja na kula, misiba, kushirikiana katika
malezi ya watoto nakadhalika
TATHMINI
Waswahili
wa leo wana ushirikiano katika baadhi ya sehemu mfano katika msiba, ndoa, na
baadhi ya sehemu hawana umoja na ushirikiano mfano katika kula, waswahili wa
leo wengi wao hula kila mmoja peke yake
0 maoni:
Post a Comment