30 Apr 2014

KIMOJA
         i.            Nyumba hujengwa kwa mawe, Nawe umenijengea,
Ukaipamba vigawe, Izidi kunivutia,
Huduma zako na wewe, pesa mimi kutumia,
Kimoja umesahau, ngoja leo nikwambie.

       ii.            Ukanipatia gari, nipate kutembelea,
Ikawa kwangu fahari, kwa wazazi salimia,
Mikufu pia bangiri, mapambo kunipambia,
Kimoja umesahau,Ngoja leo nikuambie.

     iii.            Ukachimba na kisima, shida ya maji kuua,
Ukasahau heshima, na dhima ya kunioa,
Ndiyo nakupa lawama, Hujajua nini ndoa,
Kimoja umesahau, ngoja leo  nikwambie.

     iv.            Ukanipa na madini,  ukajua ndiyo penzi,
Ukaivaa miwani, ukadhani mwisho kazi,
Kumbe tatozo chumbani, mficho na nyingi tenzi,
Kimoja umesahau, ngoja leo nikwambie

       v.            Ukafungua mradi, nipate kuendeleza,
Imani na Itikadi, matatizo kupwekeza,
Maisha ninafaidi, kimoja nakipoteza,
Kimoja umesahau, ngoja leo nikwambie.

     vi.            Sasa ngoja nikwambie, hicho ulichosahau,
Usahihi jifanyie, nami nipate walau,
Nami ndani nitulie, kazi yako we mdau,
Kimoja umesahau, ngoja leo nikwambie.

   vii.            “HUBA” hujenga mahaba, ndicho  ulichosahau,
Nimekosa mi kushiba, ndiyo kisa cha dharau,
Sahihisha mara  saba, kwangu iwe angalau,
Kimoja umesahau, ngoja leo nikwambie.

 viii.            Pesa hujenga majumba, wala hajengi mapenzi,
                   Pesa hununua shamba, kwenye penzi si mjenzi,
                  HUBA ndiyo vunja mwamba, kama nazi na mkwezi,
Kimoja umesahau,  ngoja leo nikwambie.

     ix.            Wewe tajiri wa mali, maskini wa mahaba,
Mali kwangu siyo dili, Dil kubwa lako huba,
Kazi kwako kufasiri, nipatie pate shiba,
Kimoja umesahau, ngoja leo nikwambie

       x.            Kingine mkono wako, umeshindwa kukazana 
Kwangu machache mashiko, zana zinapokutana,
Kubwa tatizo ni lako, mkono kutokazana,
Kimoja umesahau, ngoje nikwambie.

     xi.            Nimeshasema machache, jaribu kuyatatua,
Taki toka nikuache, wewe ni wangu wa ndoa,
Ya zamani tuyaache, jenga yetu familia,

Sasa nimeshakwambia, kitu ulichosahau.shairi kimoja
Powered by Blogger.

Wasiliana nami papo kwa papo

Name

Email *

Message *

Ads 468x60px

Breaking News

Top Featured

Featured Posts

Sample text

Sample Text

Recomended

Facebook

Advertise

Most Popular

Connect With Us

Followers

Social Icons

Pages

Pages

BTricks

Pages

Popular posts

Tafuta chochote ukiwa hapahapa

Kategori

Recent Comments

You can replace this text by going to "Layout" and then "Page Elements" section. Edit " About "

recent posts

Video Of Day

TRANSLATE

Instructions

Video

Flickr Images

FURAHIA UWEPO WAKO HAPA

Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

Imetembelewa mara

TAKWIMU ZA WATEMBELEAJI

Popular Posts

SAJIRI

Definition List

premium-wordpress-themes.org