SWALI
1.
Dadavua maana ya dhana mawasiliano kwa kurejelea nadharia mbalimbali.
2.
Istilahi stadi za mawasiliano hufafanuliwa kwa kuzingatia nadharia
mbalimbali.
Jadili
1. Dadavua maana ya dhana
mawasiliano kwa kurejelea nadharia mbalimbali.
Kwa
mujibu wa Kavoi na Wanjala (2013) wametafasili dhana mawasiliano ni kitendo cha uwasilishaji na ung’amuaji
wa maana kati ya watu au jamii kwa kutumia mfumo wa ishara na miondoko iliyokubalika katika
jamii mahusisi.
Dhana mawasiliano
imejaribu kuelezwa katika kitabu cha
“stadi za mawasiliano” katika nadharia kuu tatu kwa namna tofautitofauti kwa
mujibu wa vijenzi pamoja na uchangaano
wake.Nadharia hizo zinazojaribu kuelezea
maana ya dhana mawasiliano finyu,mawasiliano mauluti na mawasiliano mihamala.
Nadharia ya mawasiliano fingu;
iliyoasisiwa na Shampon,C.E na
Weaver,W(1949).walitafasili mawasiliano kwa upande mmoja tu yaani mawasiliano na
simu.Aina hii ya mawasiliano fingu inahusu vipengele vitatu ambavyo ni mtoa
ujumbe,ujumbe na mlengwa.Nadharia hii hutuumiza zaidi katika shghuli za utawala.waasisi hawa pia walibainisha kuwa kelele
ndio chanzo kikubwa
kinachokwamisha mawasiliano.vilevile nadharia hii imeshindwa kuonyesha
marejeo ya ujumbe anaotumia mtoa ujumbe
kwenda kwa mlengwa.
Pia
waitifaki wameweza kuelezea dhana ya mawasiliano kwa kutumia nadharia ya
mawasiliano mahuluti waitifaki wameichukulia aina hii ya mawasiliano kuwa kwa
kiasi fulani ni kamilifu,mawasiliano mahuluti huhusisha vipengele vitano
ambavyo ni mtoa ujumbe,ujumbe,nyenzo,mpokea ujumbe na jibu.Aina hii ya
mawasiliano huonyesha namna mtoa ujumbe
anavyogusana na kuingilia na mpokea ujumbe kupitia majibu yanavyotolewa,ili
kuwa na mawasiliano timilifu katika uhusiano wa mtagusano mtoa ujumbe na
mpokeaji ujumbe hubadilishana
nafasi.Nadharia hii ni mari zaidi ila hainyooshi uhalisia wa
uchangamani wa mchakato wa mawasiliano.
Waitifaki
wa nadharia hii ya mawasiliano mhamala wanadai kuwa wahusika katika mchakato wa
mawasiliano huwa hawapeani zamu ya kutoa ujumbe,kuupokea ujumbe wala kutoa
jibu.Waasisi hawa wanaamini kuwa hutokea
kwa wakati mmoja wao huchukulia mawasiliano kama mfumo wenye hatua madhubuti na
unaojengwa kwa mihimili
inayotegemea,mihimili hiyo ni ujumbe,nyenzo,mtoa ujumbe,mlingwa,jibu,muktadha
wa mawasiliano, idadi ya wahusika tajriba(utamaduni) ya wahusika na hali ya
upokeaji na wawasilishaji.
Kwa
ujumla mchakato wa mawasiliano unahusisha hatua saba ambazo zimefumwa katika
shuka la muktadha na wahusika
.ujumbe,nyenzo,mtoa ujumbe,usimbaji,mpokeaji ujumbe,usimbuaji na jibu kwa hiyo
stadi za mawasiliano zinahitajika muda
wote wa mchakato wa mawasiliano.
2. Istilahi stadi za mawasiliano
hufafanuliwa kwa kuzingatia nadharia mbalimbali. Jadili
Istilahi”
Stadi za mawasiliano” imetokana na tafsiri
ya istilahi “Communicaion skills” ya kiingereza ,Baaadhi ya watu
wameitafasili kama “Mbinu za
mawasiliano”Kimakosa.Istihali za “Stadi za mawasiliano” imeweza
kufafanuliwa au kutafasiliwa katika nadharia
tatu kuu zinazojaribu kuitafasisi istilahi hii ambozo ni nadharia ya
umilisi, nadharia ya ujaminishaji na nadharia ya utawala taarifa na
mawasiliano.
Katika
kitabu cha Stadi za mawasiliano waitifaki walioweza kuielezea nadharia
ya umilisi, ni pamoja na
Smith,Caput,Cupach,Spitznerg,Crettenden na Rawstone wao wanashikilia kuwa Stadi za mawasiliano humwezesha
mwasilianaji kuchajua mbinu stahili ya mawasiliano ili aitumie kuwasilisha ujumbe
kwa mujibu wa muktadha husika.Nadharia hii inashikilia kuwa mwasilianaji
anayemudu Stadi za mawasiliano anafaa
kuwa na hekima,maarifa na motisha inayomwezesha kuteua nyenzo
tatu za kubeba ujumbe katika muktadha unaofaa,Pia nadharia hii imejengwa
katika nguzo kuu nne ambazo ni hekima,motisha,maarifa na muktadha ambozo
mwasilianaji anapaswa kuzizingatia ili
aweze kufikisha ujumbe ilivyokusudiwa
Nadharia ya ujiaminishaji; nadharia
hii iliasisiwa na William Gudykunst
mwaka 1985,Waitifaki wake wanadai kuwa
maingiliano ya wawasilianaji wakiwa
katika mchakato wa mawasiliano hugubikwa na hali ya wasiwasi,uoga na mashaka
hususani katika hatua za mwanzo.Hali hii hutokea zaidi iwapo
wahusika hawafahamiani au wanatofautiana kihadhi,kiumri na kielimu au
kikabila,Nadharia hii hudai kuwa
mwasilianaji ambaye anamudu Stadi za mawasiliano anapaswa kuwa na uwezo wa
kudhibiti na kushinda hali ya mashaka udhibiti huo huwajengea wawasilianaji hali ya kujiamini.
Nadharia ya utawalaji taarifa na
mawasiliano; waasisi
wa nadharia hii ni pamoja na De
Ridder,Ballinger na De sai. Waitifaki wa nadharia hii wanashiliki kuwa Stadi za mawasiliano huwawezesha
wawasilianaji kubadilishana,kushilikishana na kutumia ujumbe husika pamoja na
kuzalisha taarifa mpiga kwa hiari katika mchakato wa mawasiliano.
Kwa
ujumla majumuisho ya nadharia hizi yanapatikana katika maoni ya mwanaisimu
Cooper (1980) anyesema kuwa mtu anayezimudu
Stadi za mawasiliano ni Yule anayeweza kusema kile anachotaka kukisema
na kumaanisha kile anachosema bila kupoteza maana au kuleta utata wowote ule.
MAREJELEO
Wanjala,
F.S na Kavoi, J. M. (2013). Stadi za
Mawasiliano na Mbinu za Kufundishia
Kiswahili.
Mwanza: Serengeti Educational
Publishers Ltd
Kiura,
M. K. & Munga, E. C. (2010). Communication
Skills. Mwanza: Serengeti Educational
Publishers Ltd.
0 maoni:
Post a Comment