UCHAGUZI
WA VIONGOZI WAPYA NDANI YA
CHAWAKAMA
SAUT-MWANZA
Chama
Cha Wanafunzi Wanaosoma Kiswahili Vyuo Vikuu Afrika
Mashariki(CHAWAKAMA) tawi la SAUT-MWANZA linatarajia kufanya uchaguzi
wa viongozi wa chama hicho tarehe 16/04/2016 siku ya jumamosi hii ni katika kutekereza matakwa ya katiba ya chama hicho kama inavyosomeka katika sura nne kifungu kidogo( muda wa
uongozi 4.4. )“kamati
tendaji itakuwa madarakani kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya hapo
uongozi utaitisha uchaguzi tena………”.
. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi bwana Anodius Kakuba amesema
maandilizi yapo vizuri na watu wameanza kuchukua fumu za kuwania
nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuzingatia vigezo, sifa na masharti
ya kuwa kiongozi ndani ya Chawakama kama katiba ya CHAWAKAMA-SAUT
inavyojieleza.
Mwisho
wa kuchukua na kurukua fomu ni ijumaa ya tarehe 8/04/2016 kutafuatiwa na usaili
wa wagombea hao siku ya jumamosi ya tarehe 9/04/2016.
Siku
ya tarehe 16/04/2016 ndio siku ya Uchaguzi wenyewe hapo ndipo uongozi
mpya wa CHAWAKAMA – SAUT(MWANZA) utakabidhiwa madaraka .
Kama
unajiona una sifa za kuwa kiongozi kama katiba inavyojieleza katika
sura ya nne kifungu kidogo 4.5 (masharti ya uongozi) Unakaribishwa
kuchukua fomu ya kugombea nafasi unayoitaka. Fomu zinapatikana kwa
mwenyekiti pamoja na katibu wake wa tume ya uchaguzi CHAWAKAMA SAUT.
Mawasiliano:
Mwenyekiti
wa tume :0765 367 768
Katibu
wa tume : 0764 832 106.
KUMBUKA
Taarifa
zote kuhusu uchanguzi utaendelelea kuzipata kupitia blog hii
0 maoni:
Post a Comment