MAANA YA KIAMBAJENGO KIFUASI.
Besha (1990). kifuasi ni sehemu ya sentensi inayosaidia kuelezea
maana ya msingi ya kiambajengo kikuu.
Mfano: "Mwanafunzi anaandika kitabu."
Kiambajengo kikuu: "Mwanafunzi"
Kifuasi: "anaandika kitabu" kinaeleza tendo linalofanywa
na kiambajengo kikuu.
Matinde (2015). Matinde anasisitiza kwamba kifuasi ni sehemu
inayokamilisha au kuongeza maana ya kiambajengo kikuu. Analeta wazo kwamba bila
kifuasi, sentensi inaweza kukosa uwazi wa maana.
Mfano. Mgeni alifika Jana usiku.
Kiambajengo kikuu ni "Mgeni"
Kifuasi . Alifika Jana usiku.
Kamusi la kiswahili fasaha. (2010).Kiambajengo ni kipashio
kinachoungana na chengine katika sentensi.
Nida(1949). Kiambajengo kifuasi ni sehemu ya mnyambuliko wa neno
inayobeba taarifa za kisarufi zinazohitajika kukamilisha maana ya neno katika
muktadha wa sentensi.
Mfano. neno anacheza , kiambajengo kifuasi ni " a"
kinaonesha Hali ya wakati uliopo. Katika neno shuleni, kiambajengo kifuasi ni
"ni", inaonesha mahali.
Kwa hivyo mkabala wa kiambajengo kifuasi ni mbinu ya uchambuzi wa
lugha inayozingatia vipashio vya kisarufi vinavyofuata kiambajengo kikuu kwa
lengo la kuelezea maana na uhusiano wa vipas nohio hivyo katika sentensi.
CHIMBUKO LA MKABALA WA KIAMBAJENGO KIFUASI.
Kwa mujibu wa Wana miundo kama vile (Frednand Saussue ) Wanaeleza
kuwa istilahi ya kiambajengo kifuasi ilibuniwa na Bloom field (1953).
Wanamiundo hawa walitumia mbinu ya uchanganuzi kiambajengo kifuasi ( immidiant
constituent analysis.ICA.) na kueleza kuwa bloom field alitambua kwamba
sentensi huundwa na mfuatano wa viambajengo ambavyo hupishana kihadhi. Kwa
mfano.
a) Mtoto mdogo anacheza mpira.
Kiambajengo kidogo hushirikiana na kiambajengo chenye hadhi sawa
katika kuunda kiambajengo kikubwa.
Wazo kuu la mbinu hii ya uchanganuzi ni kwamba, sentensi hugawanywa
katika sehemu ndogondogo Hadi kufikia sehemu ambazo haziwezi kugawanywa tena.
Kilasehemu hudhihirisha maneno yanayokaribiana na yenye kuhusiana zaidi.
Sehemu ambayo haiwezi kugawanywa zaidi huitwa kiambajengo tamati .
mfano neno " Anacheka" " a" ni kiambajengo
tamati.
Katika isimu maumbo kiambajengo kikubwa huwa ni neno , ilhali
kiambajengo kidogo ( tamati) ni mofu. Katika sentensi kiambajengo kikubwa ni
sentensi na kiambajengo kidogo cha uchanganuzi huwa ni neno.
UTOKEAJI WA DHANA YA UNYAMBUAJI (UPANUZI) KATIKA UCHANGANUZI
WAKIAMBAJENGO KIFUASI.
Hii ni sifa ambayo huzipanua na kizipanga sintensi ili kuleta
uwiano na kukubalika katika sarufi husika. Kwa mfano
a) mtoto / amepotea .
b)mtoto mrefu/ amepotea Leo
.
c) mtoto mrefu mmnene / amepotea Leo asubuhi.
Unyambuaji huu hudhirisha uhusiano wa maneno kwa mfano Nomino na
Kivumishi kuliko Nomino na Kielezi. Kitenzi na kielezi kuliko Kitenzi na
Kivumishi.
Uhusiano wa nafasi zao
katika tungo Mfano Kiwakilishi huchukua nafasi ya Nomino ( hii huitwa
ubadilishanaji wa nafasi ya utokeaji).Mfano Juma na Ali wameenda msikitini Huwa
Wao wameenda msikitini ,
Hadhi yao na mpangilio unaoleta maana na wenye kufuata kaida za
kisarufi. Mfano, Mkulima analima
mahindi. Neno Mkulima ambalo ni kiambajengo kikuu ndilo lenye hadhi katika
sentensi hii.
Uchanganuzi wa sentensi kwa kutumia matawi hubainisha hadhi ya
vipashio katika tungo , kuanzia kipashio kikubwa Hadi kipashio kidogo kabisa.
Aidha uchanganuzi huuhutumiwa kuonesha uhusiano wa vipashio katika tungo.
UMUHIMU WA UCHAMBUZI WA KIAMBAJENGO KIFUASI
Kuonyesha viambajengo vya sentensi na kudhihirisha nafasi ya
utokeaji na uhusiano wa viambajengo hivyo. Mfano, Nomino na Kivumishi, Mwanafunzi mnene hapa
huonesha uhusiano wa vaimbajengo N+V, Kiwakilishi na Kivumishi, Mfano Wao
warefu wamekaa Mbele
Kuonyesha hadhi ya viambajengo katika tungo kutoka kiambajengo
kikubwa hadi kiambajengo kidogo.Katika kiambajengo kikubwa ni sentensi na
kiambajengo kidogo ni mofu. Mfano, Asha anasoma kitabu
Hapa kiambajengo kikuu ni "Asha" ( mhusika mkuu wa tendo
- Nomino). Pia " anasoma
kitabu" ni kiamabjaengo kifuasi
" Amelala" ni kiambajengo kikuu katika neno , ambapo
kimbajengo kidogo (mofu) ni " a"
mofu ya nafsi, " me" mofu ya wakati, "Lal" mofu ya
mzizi na " a" ni mofu tamati
Huweza kutatua utata katika sentensi mbili au zaidi kwa mfano mama
Zakaria amesafiri, sentensi hii ni tata, uchanganuzi kiambajengo kifuasi
huondoa utata huu kwa kutenganisha maneno kwa misingi na uhusiano wa
viambajengo.
Mama/Zakaria amesafiri(kumuarifu Mama kwamba Zakaria amesafiri). Mama Zakaria/amesafiri
(yaani Mama ake Zakaria amesafiri).
Kiambajengo kifuasi hujibu maswali kama nani? nini? wapi?
lini?.Mfano Baba amekwenda sokoni ( sentensi hii imejibu swali la wapi?.)
Mama amepika ( hii inauliza amepika Nini? ) na kuwa mama amepika
keki.
UDAIFU WA MKABALA WA KIAMBAJENGO KIFUASI.
1. Sentensi Zote Kuchukuliwa Kuwa na Muundo wa Kimstari
Uchanganuzi wa kiambajengo kifuasi unadhani kwamba sentensi zote
zinafuata mtiririko wa kimstari (maneno yakiungana moja kwa moja). Hii ni
changamoto kwani baadhi ya sentensi zina miundo isiyo ya kimstari, kama vile
miundo inayojumuisha vipashio vinavyorudiarudia au vifupisho vya maana.
Mfano:
"Aliyekuja jana ndiye aliyenisaidia."
Uchanganuzi wa kimstari utaiona sentensi hii kama muunganiko wa
vipashio vilivyopangwa mstari mmoja, lakini kiuhalisia, kuna kipashio cha ndani
("Aliyekuja jana") kilichounganishwa na kipashio kikuu.
2. Kushindwa Kuunganisha na Kuchanganua Sentensi Tofauti
Uchanganuzi wa kiambajengo kifuasi unalenga zaidi lugha maalum
badala ya kuweza kuunganisha sentensi kutoka lugha tofauti au hata kuchanganua
sentensi zenye muktadha wa lugha mchanganyiko.
Mfano:
Lugha tofauti: "Juma alikwenda sokoni, lakini in the evening
he returned late."
Uchanganuzi huu hauwezi kuchanganua kwa ufanisi sehemu ya Kiingereza
na Kiswahili kwa pamoja.
3. Kutoweza Kuchanganua Sentensi Zisizo Sahihi Kimuundo
Uchanganuzi huu hauwezi kufasili sentensi ambazo si sahihi kimuundo
kwa sababu unategemea muundo wa kawaida wa sarufi.
Mfano:
"Alimkimbilia mwizi mwituni mnene."
Hii ni sentensi isiyo sahihi kimuundo kwani haijulikani kama
"mnene" inamhusu mwizi au mwituni. Uchanganuzi wa kiambajengo kifuasi
hautoi ufafanuzi wa sintaksia mbadala.
4. Kushindwa Kuonyesha Uhusiano wa Sentensi Zenye Maana Tofauti
Uchanganuzi huu hauwezi kuonyesha uhusiano kati ya aina tofauti za
sentensi, kama vile mtenda na mtendewa, au sentensi yakinishi na kanushi.
Mfano:
Sentensi yakinishi: "Mtoto alikula chakula."
Sentensi kanushi: "Mtoto hakula chakula."
Uchanganuzi wa kiambajengo kifuasi hauonyeshi tofauti ya kiuhusiano
kati ya sentensi hizi.
5. Kuchanganua Sentensi za Muundo Mmoja Pekee
Uchanganuzi huu hufanya kazi vizuri kwa sentensi rahisi, lakini
unatatizika kwenye sentensi changamano au zinazohusisha vipashio vingi.
Mfano:
Sentensi rahisi: "Mama alipika chakula."
Sentensi changamano: "Mama alipika chakula wakati baba alikuwa
akifanya kazi ofisini."
Sentensi changamano ina vipashio viwili vinavyotegemeana, hali
ambayo uchanganuzi wa kiambajengo kifuasi hauwezi kuichanganua kwa ufanisi.
6. Kutobainisha Uhusiano wa Umbo la Ndani na Umbo la Nje
Uchanganuzi huu hauwezi kuonyesha uhusiano kati ya umbo la ndani
(maana ya sentensi) na umbo la nje (muundo wa sentensi). Hili linaathiri
uchambuzi wa kauli tendi (mtenda) na kauli tendwa (mtendewa).
Mfano:
Kauli tendi: "Juma alikata mti."
Kauli tendwa: "Mti ulikatwa na Juma."
Uchanganuzi wa kiambajengo kifuasi hauonyeshi uhusiano kati ya
sentensi hizi mbili, ingawa kiuhalisia zina maana moja.
Uchanganuzi wa kiambajengo kifuasi huchukulia kuwa sentensi zote
zina muundo wa kimstari, hivi ni kwamba sentensi ni muambatano wa kiambajengo
(maneno) wazo ambalo sio sahihi
Uchanganuzi kiambajengo kifuasi hauna uwezo wa kuziunganisha
sentensi na kuzichanganua bali huchanganua sentensi ambazo zipo katika lugha
husika.
Uchanganuzi huu hauwezi kutumiwa katika kuchanganua sentensi ambazo
si sahihi kimuundo.Kwa mfano alimkimbilia mwizi mwituni mnene
Haina uwezo wa kuonyesha uhusiano baina ya baadhi ya sentensi kwa
mfano sentensi ambayo kiima ni mtenda na ambayo kiima ni mtendewa,sentensi
yakinishi na sentensi kanushi
Huchanganua sentensi za muundo mmoja hivi kwamba ni vigumu kitumia
uchanganuzi huu katika kuchanganua sentensi changamano
Wanasarufi miundo hawakubainisha uhusiano wa umbo la ndani na umbo
la nje katika muundo wa sentensi, kwa hivyo ilikuwa vigumu katika uchanganuzi
wa sentensi zenye kauli tendi na tendwa.
0 maoni:
Post a Comment