Platt (1985) anafasili mofu kama kipashio kidogo kabisa chenye
maana katika lugha. Mofu haiwezi kugawanywa katika sehemu ndogondogo zaidi bila
kuharibu maana yake. Mofu huwakilisha maana ya kileksika na zile za kisarufi.
TUKI (1990) wanasema kuwa mofu ni kipashio cha kimofolojia kiwakilishacho
mofimu.
Baada ya kuona fasili zote tatu zilizotolewa na wataalamu
mbalimbali kuhusiana na dhana ya mofu, yapo mabo ya msingi kabisa
kuhusu sifa muhimu za kuzingatia zinazopambanua dhana ya mofu. Mambo haya ya
msingi yanaweza kuzingatiwa:
(i)Mofu ni sehemu halisi ambazo huwa tunazitamka na kuzinadika
wakati tunapoandika maneno lakini maana ambazo huwakilishwa na mofu ndizo
tunazoziita mofimu ambazo ndizo huwa dhahania kwa sababu maana hizo huwa
hazitamkwa wala kuandikwa.
(ii)Kwa kweli mofu imo katika upande wa utendaji lakini mofimu ni
dhana ya kidhahania iliyomo akilini mwa watu na ambayo ni sehemu ya umilisi wa
lugha wa kila mtu. Mofimu ni tafsiri ambayo mtu hufanya akilini mwake kuhusu
maana ambayo husetiriwa kwenye mofu.
Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa, mofimu ni kipashio kidogo sana cha
neno ambacho kina maana na pia kinaweza kubadili maana ya neno. Hebu tuone
mfano wa mofu kama ifuatavyo:
{imb}hubakia {imb} tu mahali popote inapotokea kama:
(i)imb+ a imba
(ii)si+imb+i siimbi
(iii)u+si+imb+e usiimbe
(iv)tu+ta+imb+a tutaimba
Mzizi (toto) pia una mofu moja tu ambayo haibadiliki, kwa mfano,
(i)m+toto (ii) wa+toto (iii) u+toto (iv) u+toto+ni
Mzizi
Mzizi ni mofu ambayo ni muhimu zaidi katika neno na huweza kukaa peke
yake kama neno kamili. Aidha, hii ni sehemu ya neno ambayo haibadilikibadiliki.
Katika uchanganuzi wa neno, mzizi hauwezi kuchanganuliwa katika sehemu nyingine
ndogo bila kupoteza uamilifu na maana yake. Hivyo basi, mzizi ni kiini cha neno
na ni sehemu ya neno ambayo maneno mengine huundwa kutoka kwao.
Mzizi wa Kitenzi
Mzizi wa kitenzi ni sehemu ya kitenzi ambayo haibadilikibadiliki
wakati wa mnyambuliko. Kiini ni ile sehemu kuu ya kitenzi bila kiambishi
chochote. Hii ndiyo sehemu ambayo hubeba maana halisi ya kitenzi. Kwa mfano:
Kitenzi Mzizi
Alipikika {-pik-}
Ulipika {-pik-}
Utapika {-pik-}
Mlipika {-pik-}
Kilipikwa {-pik}
Sifa za Mzizi
(i)Mzizi hufanya neno kuwa na uafifishaji mkamilifu, hivi kwamba
mzizi ukiondolewa katika neno, utakopotea.
(ii) Mzizi huweza kukaa yake kama neno kamili, kwa mfano:
baba,mbuzi n.k (mofu huru tu).
(iii)Katika lugha ya Kiswahili kuna baadhi ya maneno ambayo huundwa
na mwambatano wa mizizi miwili.
Maumbo ya Mizizi katika Lugha ya Kiswahili
(i)Mzizi unaundwa na fonimu moja
Kwa mfano: katika maneno yafuatayo:
Kufa – / f /
Kula / l /
(ii)Mzizi unaounda na fonimu mbili silabi
Mfano katika maneno
Mtu – (-tu-)
Mtoto m- (-to)
(iii)Mzizi unaoundwa na mofimu zaidi ya mbili
Kwa mfano: Cheza (–chez-)
Piga – (-pig-)
Imba (-imb-)
Tembea- (-temb-)
Aina ya Mizizi
Kuna aina kuu mbili za mizizi. Uanishaji huu umekitwa kwenye maana
na umbo la mizizi husika.
(a) Mzizi Huru
Mzizi huru ni mzizi ambao huweza kusimama peke yake kama neno lenye
uarifishaji mkamilifu ambao hauhutaji kaumbikwa viambishi. Katika lugha ya
Kiswahili, kwa mfano, mizizi ya maneno mengi huwa ni mofu huru ambazo zina
uwezo wa kukaa peke yao, kama maneno kamili kwa mfano, maneno yafuatayo:
Nomino{baba} 2. {taifa} 3. {Sungura} 4. {shati} 5. {Ndege} 6.
{kaka} 7. {Juma} 8. {Arusha} 9. {Mombasa} 10. {Tanga}
Vivumishi
Rahisi 2. chafu 3. Bora 4. {Imara} 5.{goigoi} 6.
{mwerevu}
Viwakilishi
{vile} 2. {mimi} 3. {wale} 4. {ninyi] 5. {yeye} 6. {wao}
Vielezi
{upesi} 2.{ haraka} 3. {sana} 4. {leo} 5. {jana} 6. {juzi}
Vihusishi
{pembeni} 2. {ndani} 3. {juu} 4. {nyuma} 5. {chini} 7.
{kwa} 8. {mbele}
(b) Mzizi Tegemezi
Mzizi tegemezi hauwezi kusimama peke yake bila kiambishi cha awali
au tamati na kuleta maana kamili. Kwa mfano :
(-l-) – katika neno kula
(-f-) katika neno kufa
(-j-) katika neno kuja
(-tu-) katika neno mtu
(-pig-) katika nenno piga
Shina
Shina ni mzizi ambao umeambikwa kiambishi tamati. Aidha ni sehemu
ya neno inayotumiwa kuunda neno jipya. Shina kamili haliwezi kuchanganuliwa
bila kupoteza maana. Kuna aina zifauatazo za shina:
(a) Shina Sahili
Shina sahili ni shina ambalo huundwa na mofu au mizizi huru. Kwa
mfano:
Shamba –mashamba
Taifa – mataifa
Shati – mashati
Jembe -majembe
(b) Shina Changamano
Shina changamano ni shina ambalo huundwa na mzizi mmoja na
viambishi, hususani viambishi tamati. Kwa mfano:
Pika – pikia, pikiwa
Piga – piga, pigia, pigana
Cheza – chezea, chezewa, chezeana
(c) Shina ambatano
Ni shina ambalo huundwa kwa muambatano wa mizizi huru miwili. Kwa
mfano:
Askari + kanzu ——————askarikanzu
Mwana+ hewa ——————-mwanahewa
Bata + mzinga —————— batamzinga
1.2 Kubainisha uhusiano wa mofu na
mofimu
Mofu ni sehemu halisi ambazo huwa tunazitamka na kuzinadika wakati
tunapoandika maneno lakini maana ambazo huwakilishwa na mofu ndizo tunazoziita
mofimu ambazo ndizo huwa dhahania kwa sababu maana hizo huwa hazitamkwa wala
kuandikwa.
Kwa kweli mofu imo katika upande wa utendaji lakini mofimu ni dhana
ya kidhahania iliyomo akilini mwa watu na ambayo ni sehemu ya umilisi wa lugha
wa kila mtu. Mofimu ni tafsiri ambayo mtu hufanya akilini mwake kuhusu maana
ambayo husetiriwa kwenye mofu. Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa, mofimu ni
kipashio kidogo sana cha neno ambacho kina maana na pia kinaweza kubadili maana
ya neno.
1.3 Kubainisha aina za Mofu katika Kiswahili Sanifu
Ndugu mwanafunzi, kabla hatujabainisha aina za mofu katika lugha ya
Kiswahili, hebu sasa tuchunguze sifa mbalimbali za mofu kama ifuatavyo:
Sifa Mbalimbali za Mofu
Zipo sifa mbalimbali za mofu katika lugha ya Kiswahili. Sifa hizo
ni
(i)Mofu kama sehemu halisi ya neno
Hii ina maana kwamba mofu ni maumbo halisi ya maneno ambayo
hutamkwa wakati watu wanapozungumza au kuandikwa wakati watu wanapoandika
maneno. Kwa mantiki hiyo basi, mofu ni umboa halisi ambalo tunaweza kulisikia
linapotamkwa na kuliona linappokuwa limeandikwa.
(ii) Mofu hudhihirika kifonolojia na kiothografia
Kwa kuwa mofu ni umbo halisi la neno, basi mofu mbalimbali hudhihirika
kifonolojia zinapotamkwa na pia kimaandishi zinapoandikwa yaani kiothografia.
(iii)Mofu huwakilisha maana
Hapa tunasisitiza kuwa mofu huwakilisha maana fulani katika neno
lolote katika lugha katika lugha yoyote patakuwepo maana na maana hizo huwa
zimesetiriwa katika mofu zilizopo katika neno. Hii ina maana kwamba kama kila
neno huwa na maana fulani, basi maana hiyo itakuwa imewakilishwa na mofu
fulani. Hii ina maana kuwa hakuna neno lolote katika lugha yoyote ambalo
linaweza kuwa ni neno lenye maana bila kuwa na mofu angalau moja. Kwa hiyo
tunaweza kusema kuwa kila neno lenye maana katika lugha, litakuwa na mofu
angalau moja.
(iv) Mofu ni kipashio kidogo kabisa cha neno chenye maana
Hapa kinachotiliwa mkazo ni ule ukweli kuwa, mofu ni sehemu ndogo
kabisa ambayo hubeba maana na kuwa sehemu hiyo haiwezi kugawanywa katika sehemu
ndogo zaidi zilizo na maana kuliko. Hapa tungeweza kusema kuwa kwa ukubwa mofu
ni umbo ambalo hudhaniwa kuwa ni kubwa kuliko fonimu na ni ndogo kuliko neno.
Aina za Mofu
Aina za mofu zinaweza huanishwa kwa kutumia vingezo vya
maana na mofolojia katika Kiswahili Sanifu. Kwa kutumia kigezo cha
maana zipo mofu za aina tatu ambazo ni:
(a) Mofu Huru ( free mofu)
(b) Mofu funge (bound morphs)
(c) Mofu tata (ambiguous morphs
(a) Mofu huru
Weber (1985) anasema ya kuwa mofu huru ni zile mofu ambazo zinaweza
kukaa peke yake kama maneno kamili. Mofu huru ni mofu zilizo na uwezo wa kukaa
peke yake na zikawa maneno kamili yenye maana.. Mara nyingi mizizi ya baadhi ya
maneno ndiyo ambayo ina uwezo wa kukaa peke yake na yakawa maneno kamili
yanayojitosheleza. Mizizi ya aina hiyo si lazima iwekwe viambishi ndipo iwe
maneno. Katika lugha ya Kiswahili, kwa mfano, mizizi ya maneno mengi huwa ni
mofu huru ambazo zina uwezo wa kukaa peke yao, kama maneno kamili kwa mfano,
maneno yafuatayo:
Nomino
{baba} 2. {Kuku} 3. {Sungura} 4. {Kalamu} 5. {Ndege} 6.
{Dada} 7. {Juma} 8. {Kilimnajaro} 9. {Nairobi} 10.
{morogoro
Vivumishi
Ghali 2. Safi 3. Dhaifu 4. {Imara} 5.{goigoi} 6. {hodari}
Viwakilishi
{mimi} 2. {sisi} 3. {wewe} 4. {ninyi] 5. {yeye} 6. {wao}
Vielezi
{upesi} 2.{ haraka} 3. {sana} 4. {leo} 5. {jana} 6. {juzi}
Vihusishi
{nje} 2. {ndani} 3. {juu} 4. {nyuma} 5. {chini} 6. {ya} 7.
{kwa} 8. {mbele}
Viunganishi
na, 2. {halafu} 3.{bila} 4. {ila} 5. {aidha} 6.{pia}
Tanbihi
Vitezni vyenye asili ya Kibantu, wakati wote huwa ni tegemezi kwa
sababu huhitaji angalau kiambishi tamati kimoja ndipo viwe neno kamili. Namba
kwenye mabano inaonyesha idadi ya mofu katika neno. Kwa mfano,
{ruk}+ {a} ruka (2)
2. {chez} + {a} cheza (2)
{andik} + {a} andika (2)
{imb} + {a} imba (2)
(b) Mofu Funge
Richards et al. (1985) wanaeleza kuwa, mofu funge ni kipashio cha
kiisimu ambacho huwa hakikai peke yake bali ni lazima kiandamane na mofu
nyingine. Hartman (1972) anasema kwamba, mofu funge ni mofu ambayo haiwezi kutumiwa
peke yake kama neno kamili lililo na maana yake bainifu, bali daima hutumiwa
kama kiambishi tu kinachoambatana na mzizi au viambishi vingine ili kukamilisha
neno. Maana ya mofu funge hutegemea muktadha wa mofu. Kwa hiyo sifa kubwa ya
mofu funge ni kuwa mofu funge haiwezi kukaa peke yake ikawa neno kamili. Sifa
hii inatofautisha mofu funge na mofu huru kuwa mofu huru ina uwezo wa kukaa
peke yake. Mofu funge lazima ziwekwe pamoja na mofu nyingine moja ili kuleta
maana kamili ya neno. Hii huwafanya wanaisimu wengine kuziita mofu hizi
tegemezi. Mara nyingi hizi mofu funge huwakilisha maana za kisarufi. Kwa mfano
katika nomino huweza kuwakilisha maana zifuatazo:
Idadi ya Umoja
(i) M+ toto (m)
(ii) Ki+tabu (ki)
(iii)ji+ cho (ji)
2.Ukubwa wa Nomino
Ji+tu (ji)
Ji +su (ji)
3.Idadi ya Wingi
Wa +toto (wa)
Vi + tabu (vi)
Ma + cho (Ma)
4.Udogo wa Nomino
Ki+ji+tu (ki)
Ki+ji+su (ki)
Ki+ji+ti (ki)
Katika mifano hiyo hapo juu tuanaona kuwa mofu ya ukubwa katika
lugha ya Kiswahili huwa ni {ji} ambayo huwekwa pamoja na mzizi wa nomino.
Lakini wakati wa kukifanya kitu mkiwe kidogo, mofu mbili hutumika kwa pamoja
yaani mofi {ki} ya udogo pamoja na mofu {ji} ya ukubwa, ambapo zikiandamana na
mzizi wa nomino ndipo tunapata ile hali ya udogo.
5.Unominshaji wa aina zingine za maneno:
Lima (i) Ku+lim+ a (1) {ku} (2) {a}
(ii)U+ku+lim+a (1) {u} (2) {ku} (3) {a}
(iii)Wa+ku+lim+a
(c) Mofu Tata
Weber (1985) anaeleza mofu tata kama kipashio cha kiisimu
ambacho kinaweza kupewa maana ya moja, yaani maana kauanzia mbili
na kuendelea. Vipashio vya kiisimu ambavyo huweza kuwa tata ni mofu, maneno,
virai na sentensi. Kwa kuzingatia fasili ya Weber, mofu tata ni mofu ambazo
huwa na maana zaidi ya moja, tuseme labda maana kuanzia mbili na kuendelea.
Hapa inafaa tutoe mfano wa mofu tata katika lugha ya Kiswahili. Tazama sentensi
ifuatayo:
Pendo alimpiga Noel mpira
Sentensi hii ni tata kwa sababu, ina maana au tafsiri zaidi ya
moja. Utata wa sentensi hiii si wa kisarufi bali upo katika kitenzi. Kitenzi
hiki kina mofu sita.
Aina za mofu kwa kuzingatia Uanishaji kwa kigezo cha
Kimofolojia
Zipo aina mbili za mofu, ambazo ni: (i) Mofu changamani
(ii) Mofu kapa
Mofu changamani
ni mofu inayoundwa kutokana maumbatana wa
mizizi huru miwili au (mashina mawili). Mashina hayo huwa na
usafairishaji mkamilifu. Kwa hiyo, kila shina huweza kusimama
kama neno kamili lenye kujitosheleza kimuundo na kimaana. Kwa
mfano:
(a) Mwana + jeshi ———————-mwanajeshi
{mw-} – ngeli ya kwanza; idadi ya umoja
{-ana-}- mzizi
{jeshi} – mzizi huru
(b) Mwana +idara –mwanaidara
{-mw-} –idadi (umoja)
{-ana-} – mzizi
{idara}- mzizi huru
Mofu Kapa
Mofu kapa haiwakilishwi na kitu au alama yoyote dhahiri. Kwa mujibu
wa Massamba (2004) anasema kuwa katika lugha ya Kibantu, viambishi vya ngeli
vya nomino zilizomo katika ngeli huwa haviko dhahiri katika neno na katika
umoja au wingi. Mofu hizi hazina umbo na hazionekani, haziandikwi wala kutamkwa
ila ni sehemu ya umilisi wa watumiaji wa lugha husika. Ijapokuwa mofu hizi
hazionekani wala kutamkwa, huwa na maana katika neno
husika. Kwa mfano:
Umoja Wingi
Ukucha kucha
Ukiangalia katika mfano wa hapo juu katika wingi, kiambishi cha
wingi hakijitokezi bayana ilhali kiambishi cha cha umoja (-u-) ni bayana.
Dhana ya Alomofu
Richards na wenzake (1985) wanafasiri alomofu kama umbo
mojawapo kati ya maumbo kadhaa tofauti yanayoiwakilisha
mofimu moja. Hartman (1970) anafasiri alomofu kama umbo
badala ya mofimu fulani ambalo halibadili maana. Bauer (1983) ni
mofu mojawapo katika seti ya mofu zinazoiwakilisha mofimu fulani ambayo ina mazingira
yake ya kifonetiki, kileksika au kisintaksia (kisarufi).
Tukiangalia fasili hizo hapo juu, tunaona kuwa zinaeleza sifa
muhimu zinazofafanua alomofu. Zifa hizo ni kama ifuatavyo:
(i)Alomofu ni umbo halisi ambalo ni sehemu ya neno fulani na mbalo hutamkwa
kwa kuandikwa. Kwa hiyo alomofu ni mofu na sifa tulizozitoa kuhusu mofu ndizo
ndizo zinazofaa pia keuelezea alomofu.
(ii) Alomofu ni mofu mojawapo miongoni mwa mofu za mofimu moja
kwani zina sura moja tu.. Popote zinapotokea hutokea na sura ileile na
hazibadiliki.
Kwa mfano katika lugha ya Kiingereza kwa mfano, kiambishi tamati
/s/ cha wingi kina maumbo mbadala yafuatayo:
/s/ kama katika maneno cats, books
/z/ kama katika maneno dogs, bags
/iz/ kama katika maneno classes, boxes, flies
/ / kama katika neno sheep
Alomofu ni umbo jingine la mofu ileile moja kama
inavyojidhihirisha katika maneno motto, muuguzi na mwanafunzi.
Tunaona kwamba, viambishi awali (m-), (mw-) na (mu-) vyote vinawakilisha mofimu
moja ya ngeli ya kwanza. Katika lugha za Kibantu. Kwa hivyo, maumbo {m-},
{mu-}, na {mw-} ni alomofu zinazokilisha mofimu moja. Hivyo basi, alomofu ni
maumbo mawili au zaidi yanayowakilisha mofimu moja. Alomofu hutokea katika
mazingira maalum katika maneno. Mifano ufuatao unaonyesha alomofu katika lugha
ya Kiswahili:
Mofimu ya umoja {mu}- {m}
{mu}
{mw}
Mifano ya Alomofu
(a) Mofu za wingi katika lugha ya Kiswahili
{wa-}- katika maneno wachawi, wanafiki, wanyonge
{mi-} – katika maneno miti, miembe, michoro n.k
{ma} – katika maneno matunda, mawele
{vi-} – katika maneno vikombe, vijiko, vichwa n.k
(b) Mifano ifutayo hudhurisha mofimu za njeo
Anacheza
Alicheza
Atachez
Katika mifano hiyo hapo juu, maumbo {-na-}, {-li-}, na {-ta-}
nialomofu ambazo husetiri
Mofimu ya njeo.
(c)Vitenzi vifuatavyo hudhihirisha mofimu ya kutendea:
Kulia
Somea
Lilia
Lelea
Katika mifano hiyo hapo juu, maumbo {-i-}, {-e}, {-le} ni alomofu
ambazo husetiri mofimu ya kutendea.
Kwa machache hayo napenda kuwatikia kila la heri wapenzi wa somaji
wa tovuti hii.
0 maoni:
Post a Comment