Imeandaliwa na Mtila Mswahili.
UTANGULIZI
Ufundishaji
ni dhana pana inayohusisha mchakato wa kuhamisha, na kuendeleza ujuzi wa lugha na mawazo mapya
kwa wanafunzi. Ufundi huu unajumuisha mbinu mbalimbali za kufundisha ili
kuyafikia malengo ya kielimu, kwa kuzingatia muktadha wa kijamii na kiutamaduni. Kwa
mujibu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)(2005), somo la Kiswahili linalenga
kumwezesha mwanafunzi kuwasiliana kwa ufasaha katika nyanja na fani mbalimbali
za kimaisha kwa kutumia lugha ya Kiswahili kupata maarifa, mielekeo, stadi za
kijamii na utamaduni, kiteknolojia na kitaaluma kutoka ndani na nje ya nchi.
Ili malengo haya yatimie, mwanafunzi anapaswa kuonesha kuwa maarifa
yanayotolewa kwenye somo la Kiswahili ameyapata kwa kufanya mtihani wa kuhitimu
elimu ya sekondari. Ufundishaji umekuwa na changamoto mbali mbali katika skuli
za Zanzibar kama ifuantavyo:
Changamoto
za Lugha: Changamoto hii hujitokeza katika matumizi ya
misamiati au maneno magumu katika kufundisha masomo mbali mbali kama kiswahili.
Maneno magumu yanaweza kumtatisha mwanafunzi juu ya jambo analojifunza walimu
wengi hasa wanzanzibar wamekuwa waliwafundiaha wanafunzi kwa kutumia istilahi
mbali mbali tofauti na yenye ugumu ndani jambo ambalo hupelekea wanafunzi wengi
kutofikia Lengo linalotakiwa na kwa kiasi kikubwa wanafunzi wanashindwa kuelewa
kinachofundishwa. Jambo hili husababisha wanafunzi kuona somo ni gumu kiasi cha
kulikatia tamaa.
Changamoto za Zana za Kufundishia
na Kujifunzia: kuwapo kwa upungufu wa vitabu vya
kufundishia na kujifunzia, hasa vya kiada na ziada. Pia, hakuna vitabu vya
kumungoza mwalimu kama vile kamusi, majarida, karatasi ngumu za kuchorea
michoro, chatipindu, vifaa vya kurekodi kama tepurekoda au kinyonyi (flashi) na
redio, ambavyo vingetumika kwaajili ya kufundishia pia kupelekea kutofikia
lengo la kufikisha ujuzi wowote kwa mwanafunzi, skuli nyingi za Zanzibar
zimekuwa zikipiga kelele juu ya kutokuwepo kwa vifaa vya kufundishia na
kujifunzia jambo hili hupelekea changamoto kubw kwa wanafunzi. Na wanafunzi
wengi wazanzibar wamekuwa wakijifunza kwa kukariri kuliko kwa Vitendo hii ni
kutokana vifaa havipatikani maskulini.
Changamoto ya walimu wenye sifa:
Katika kufikia lengo la ufundishaji huhitajika mwalimu aliebobea na mwenye sifa
juu ya ufundishaji lakini kumekuwa na changamoto kubwa ya walimu wenye sifa ya
kufundisha kwa sasa katika visiwa vya Zanzibar hii nikutokana na walimu wengi
kutokuwa na elimu ya kutosha katika ufundishaji na walimu wengi Zanzibar
waliajiriwa bila ya kuzingatia vigezo muhimu anavyopaswa kuwa navyo mwalimu
kama wa sanaa na pia wasayansi hivyo jambo hili hupelekea kutofikiwa lengo la
ufundishaji.
Changamoto ya muda mdogo wa
kujifunzia: Ufinyu wa muda wa masomo ni changamoto nyingine
inayokabili ufundishaji Katika shule nyingo za Zanzibar muda wa masomo ni
mfupi, na hii inamaanisha kuwa walimu hawana muda wa kutosha kufundisha kwa
kina. Hali hii inasababisha kukosa uelewa wa kina wanafunzi wanapokuwa na muda
mfupi wa kujifunza, wanakosa fursa ya kuelewa kwa kina dhana na kanuni za
masomo mbali mbali yanayotolewa kama vile kiswahili. Hii inawafanya wanafunzi
kutokuwa wamahiri kwa kile wanachofundishwa.
Changamoto za Taaluma/Ujuzi:
Changamoto zinazohusiana na taaluma/ujuzi ni kikwazo katika ufundishaji wa Kiswahili .Kuna baadhi ya walimu wana elimu ya vyeti ila umahiri ni sifuri
hivyo kuna changamoto ya uwezo wa kufundisha kwa walimu na tatizo hili
husababishwa na changamoto za walimu kitaaluma.pia tatizo jengine linasabishwa
na walimu kutofundisha vizuri vitabu vya fasihi kama vile tamthiliya na diwani
.Walimu wengi, hasa waliosoma zamani bado wanashikilia misimamo yao ikiwa kuna
jambo jipya hawalijui, huishia kupinga kwa kutumia mifano ya vitabu vya zamani
ambavyo hata kwenye mtaala havitumiki. Hawataki kujifunza mambo mapya kwa
kujisomea na kufuatilia tafiti.
Mtazamo Hasi kuhusu Kiswahili:
Zanzibar kuna changamoto ya mtazamo hasi kuhusu lugha ya Kiswahili ambapo
Changamoto hii inahusisha wazazi, wanajamii na wanafunzi. Wazazi huwahimiza
watoto kujifunza na kuwekeza nguvu kwenye masomo yanayofundishwa kwa
Kiingereza. Jamii imeweka mtazamo kwamba somo la Kiswahili linaeleweka; pia,
halimsaidii mwanafunzi kupata ajira akihitimu likilinganishwa na masomo ya
Kiingereza. Mtazamo huu huathiri ufundishaji.
Hivyo
changamoto hizi zinahitaji mikakati madhubuti na ushirikiaono kati ya serikali,
walimu, wazazi pamoja na wadau wengine wa elimu, ili kuhakikisha Kiswahili kinapata muamko
mzuri wenye kuleta mafanikio kwa kuboresha miundo mbinu ya skuli, kuongeza muda
wa kufundisha kwa somo la Kiswahili, kutoa elimu kwa walimu wa zamani ili
kuendana na mitaala mipya na kutoa elimu kwa wanafunzi na wazazi pamoja na
wanaja ii kuhusiana na mafanikio
yanayopatikana kwenye lugha ya Kiswahili
baada ya kuhitimu.
MAREJEO
BAMITA
(2022): Mwongozo wa Upimaji Katika Shule za Msingi. Dar es salaam.
Juma,
H.K (2017): Tathmini ya Mitaala ya Ufundishaji wa Kiswahili Ngazi ya Sekondari
katika Matumizi ya Nadharia Nchini Tanzania.
Akaka,
L. (2013): Changamoto zinazowakabili Walimu katika Ufundishaji wa Kiswahili
katika Shule za Upili nchini Kenya. Kioo cha Lugha.
0 maoni:
Post a Comment