Imeandaliwa na Mtila Mswahili
NADHARIA ZA UANDISHI WA KAZI ZA FASIHI.
Maana ya Nadharia,
BAKIZA (2010) Nadharia ni mawazo yanayotumika kuwa ni muongozo wa
kutekeleza jambo au kutambulika kwa dhana.
Kwa ujumla nadharia ni mfululizo wa dhana au mtazamo wa kisayansi
au falsafa inayokusudiwa kuelezea na kufafanua.
Maana ya nadharia za uandishi wa kazi za fasihi.
Kwa kuangalia muktadha wa uandishi wa kazi za fasihi, nadharia ni
mfumo wa mawazo, mitazamo au falsafa zinazomwongoza mwandishi au mhakiki wa
kazi ya fasihi katika kutunga, kuchambua au kuelewa maana na madhumuni ya kazi
hiyo. Nadharia husaidia kuelewa kwa kina vipengele vya fasihi kama vile
dhamira, wahusika, mandhari, lugha, na muundo.
Mambo ambayo humuongoza Mwandishi kutokana na nadharia.
Mwongozo katika uandishi.Nadharia humwelekeza mwandishi kuandika kazi ya
fasihi kwa kuzingatia mtazamo fulani wa kijamii, kisiasa, kihistoria, au
kisaikolojia. Mfano:Mwandishi anayeandika kwa kutumia nadharia ya uhalisia
atazingatia maisha halisi ya jamii, matatizo ya kawaida na jinsi watu
wanavyoathirika.Mwandishi anayefuata nadharia ya kiisimu anaweza kuandika
akizingatia muundo wa lugha, matumizi ya tamathali, na mtindo wa mawasiliano.
Ufunuo wa Maudhui.Kwa kutumia nadharia, mwandishi anaweza kufichua
ukweli wa kijamii au kimawazo, kwa mfano:Nadharia ya kikasumba: huonyesha
dhuluma za kitabaka.Nadharia ya kifeministi: hufichua ukandamizaji wa wanawake.
Uchanganuzi wa wahusika na migogoro.Nadharia huwasaidia waandishi
kuchora wahusika na migogoro kwa njia ya kina. Wahusika wanaweza kuwakilisha
vikundi vya kijamii, mitazamo ya kifalsafa, au hali ya kisiasa.
Ujenzi wa dhamira kwa ujumla.Kila nadharia huleta ujumbe au mafunzo
mahsusi. Kwa mfano:Nadharia ya uondoaji (deconstruction) huchanganya au
kupindua maana za kawaida.Nadharia ya uhulishaji huonesha jinsi watu huathiriwa
na jamii au tamaduni zao Kwa kila jamii husika.
Nadharia ya uandishi wa kazi za fasihi kutokana na Mungu.
Nadharia ya uandishi inayotokana na Mungu inahusisha imani kwamba fasihi
imeletwa na Mungu, Mungu pia alikuwa muhusika mkuu .Pia, ilikuwa kwamba Mungu
alikuwa na matendo mengi aliyafanya huku akiwa ni muhusika mkuu wa matendo na
mndirimo wa maisha ya viumbe.Hivyo hapo ilipoibuka uandishi wa kazi za fasihi.
Udhaifu wa nadharia hii.
Nadharia hii imeibuwa maswali kadhaa wa kadhaa juu ya usanii wa
Mungu, maswali yenyewe ni kama ifuatavyo,Ni kuwa Mungu ni kitu kisichoonekana
ni kwa namna gani awe mhusika wa matukio?, Dhamira zitafikishwaje na kitu
kilichopo Nadharia hii haikubaliki kwa sababu kuna udhaifu mkubwa ndani yake.
Nadharia ya uandishi kutokana na mazingira uhalisia wa mazingira.
Nadharia ya uandishi wa kazi za fasihi kupitia uhalisia wa mazingira
inahusisha mtindo wa utunzi unaozingatia na kuakisi hali halisi ya maisha ya
jamii, mazingira yake, na matukio yanayotokea katika mazingira hayo.
Udhaifu wa nadharia hii
Nadharia
hii ya uandishi wa kazi za fasihi kutokana na uhalisia wa mazingira ina udhaifu
, Udhaifu wake ni kwamba sio kila wanachoandika waandishi kinatoka kwenye
mazingira halisi bali huwaza na kuwazua Kwa namna ya kipekee ambayo hulenga
kumfurahisha msomaji,msikilizaji.Pia hutaka kuhifadhi Utamaduni wa mtu binafsi
katika maisha yake.
Nadharia hii pia husababisha ugomvi Kwa waandishi wanapoandikia
uhalisia wa mazingira bila ya kuficha chochote.
Nadharia ya uandishi wa kazi za fasihi kutokana na wigo.
Maana ya Nadharia ya Wigo
Kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali, nadharia ya wigo inafafanuliwa
kama ifuatavyo:-
Nadharia
ya wigo ni Ile hali ambayo mwanaadamu alianza kuwa mbunifu kwa kuiga maumbile
mbalimbali yaliyomzunguka pamoja na kuiga vitu vilivyomo katika mazingira yake
kama vile miti,sauti za wanyama,watu na kadhalika.
Waasisi
wa nadharia ya wigo ni Wagiriki ambao ni Plato na Aristotle ambao ni
wasambazaji wakuu wa nadharia hii,waasisi wa nadharia hii wanadai kuwa fasihi
imetokana na mwigo,uigaji.Hii ni kwamba binaadamu alianza sanaa kwa kuwa
muigizaji wa maumbile yaliyomzunguka . Hivyo kazi za fasihi za mwanzo mara
nyingi zilijaribu kusawiri vitu vilivyomo katika mazingira kama miti , sauti za
wanyama,milio ya vitu mbalimbali.
Pia
Plato anaendelea kuifananisha dhana ya mwigo na uungu.Anasema " Vyote
binaadamu wanavyoona na kuiga ni mwigo wa vitu halisi vilivyopo kwa Mungu.
Katika nadharia hii Kuna vipengele muhimu vya nadharia ya wigo katika
fasihi (uandishi)ni hivi ifuatavyo:-
Wigo wa Maana,Mtindo wa mbinu za kifasihi,wigo wa wahusika na wigo
wa maudhui.
Udhaifu wa nadharia ya uandishi kutokana na wigo.
Nadharia hii Ina udhaifu,Sio kweli kwamba mwanaadamu anaiga kutoka kwa Mungu.Pia
hudumaza akili ya Mwandishi kwa kutoa kuhangaisha akili yake mwenyewe.
Nadharia ya Uandishi wa kazi za fasihi , Nadharia kipaji.
Nadharia ya
uandishi wa kazi za fasihi kupitia kipaji inazingatia uwezo wa kipekee wa
mwandishi katika kuunda na kuwasilisha kazi za fasihi. Kipaji hiki kinahusisha ubunifu, ufanisi
katika matumizi ya lugha, na uwezo wa kuhamasisha hisia na mawazo ya wasomi.
Mfano mzuri ni Waandishi wenye vipaji ni Said Ahmed,Shaaban Robert
na wengineo,Mwandishi kama Shaaban Robert anajulikana kwa ustadi wake katika
matumizi ya lugha na mbinu za fasihi.
Katika riwaya yake Rosa Mistika, anatumia lugha yenye uzito na mitindo
ya kipevu kuwasilisha masuala ya kijamii na kiuchumi, akionyesha ufanisi wa
kipaji chake katika uandishi.
Nadharia ya uandishi wa kazi za fasihi kupitia kipaji inasisitiza
uzuri ,na ufanisi wa kazi za uandishi wa uwezo wa kipekee wa mwandishi katika
kuunda kazi za fasihi.
Udhaifu wa nadharia hii.
Udhaifu wa nadharia hii kwamba sio waandishi wote wana kipaji bali
walianza kidogo kidogo na baadae kufikia hatua kubwa ya uandishi na mwishowe
kujulikana.
Nadharia ya kikasumba .
Nadharia hii imejikota zaidi kwa mwandishi ambae huendeahwa na
hisia zake au za watu Kwa kusikia propaganda zinazoletwa na jamii .
Udhaifu wa nadharia hii
Nadharia hii Ina
udhaifu mkubwa kwani miongoni mwa sifa za msanii ni vizuri kushughulikia
maswala yanayoikumba jamii kwa kuyaondosha au kuwaasa watu kwenye mambo hayo na
sio kuongeza chuki ndani ya jamii.
Hivyo
nadharia zote zina umuhimu fulani ambao umechochea kwa namna moja au nyengine
ambayo umeweza kuleta faida ambayo imewasaidia wanafunzi wengi katika masuala
yao ya kielimu kwenye kada tafauti tafauti.
MAREJELEO.
Wizara ya Elimu na Utamaduni,(2003).Ufundishaji unaozingatia Ujenzi
wa Maana,Chuo cha Ualimu Morogoro:
Ecoprint Ltd.
TUKI, (2004). Kamusi ya Kiswahili sanifu (toleo la pili),Nairobi:
Oxford University Press.
Mulokozi,M.M.(2017). Utangulizi wa fasihi ya Kiswahili.Dar es
salaam.Tanzania
TET, (2014). Kiswahili,kidato cha nne,Tanzania: Oxford University
limited.
Kumar,R.(2021). Research methodology,(4ed).London:SAGE Publications
India Pvt ltd.
https://www.msomibora.com/2018/06/Kiswahili -form-one-topic-4-fasihi.html?m=1.
https://learn.farmhub.ag.
https://sw.wikipedia.org.
0 maoni:
Post a Comment