Imeandaliwa na Mtila Mswahili
Mbinu za ufundishaji
ni njia au mbinu ambazo walimu wanazitumia katika mchakato wa kutoa elimu kwa
wanafunzi. Zinatoa ramani jinsi mwalimu anavyopanga, kutekeleza na kusimamia
mchakato wa kufikisha maarifa, ujuzi na mitazamo kwa wanafunzi. Lengo kuu la
mbinu za ufundishaji ni kuwasaidia wanafunzi kufikia malengo ya kujifunza
yaliyowekwa.
Mbinu zisizoshirikishi ni
mbinu ambazo huweka msisitizo kwa walimu kama mtoaji mkuu wa maarifa, huku
mwanafunzi akiwa mpokeaji zaidi. Hizi zinaweza kujumuisha matumizi ya data
zilizokusanywa awali,tafiti za maktaba na uchambuzi wa takwimu.
Sifa za mbinu zisizoshirikishi
v Mwalimu
ni kituo kikuu cha maarifa na habari: Jukumu lake ni kusambaza taarifa huku
wanafunzi wakitegemea yeye kwa kila kitu wanachojifunza.
Mfano-:
Mwalimu
akitoa mhadhara darasani kuhusu sifa za sayari huku wanafunzi wakibaki kimya na
kuandika maelezo tu.
v Ufanisi
katika kusambaa kwa tarifa nyingi: Mbinu hizi huruhusu kwa kiasi kikubwa cha
habari kusambazwa kwa wanafunzi wengi kwa muda mfupijambo linalofaa kwa mada
pana au darasa kubwa.
Mfano-:
Mhadhara
wa utangulizi wa somo jipya katika chuo kikuu, ambapo profesa anatoa muhtasari
wa kozi nzima kwa muda mfupi.
v Msisitizo
kwenye kukariri ukweli na dhana: Lengo kuu mara nyingi ni kuhakikisha wanafunzi
wanakariri ukweli, kanuni au fomula.Uelewa wa kina au matumizi ya maarifa
hayapewi kipao mbele.
Mfano-:
Mwalimu
akirudia mara kwa mara fomula za fizikia na kutaka wanafunzi wazikariri kwa
ajili ya mitihani, bila ya kuwapa matatizo ya vitendo ya kuvitumia.
v Udhibiti
kamili wa walimu: Mwalimu ana udhibiti kamili wa mtaala, kasi ya ufundishaji na
shuguli zote za darasani. Anaamua nini kifundishwe, linin a jinsi gani.
Mfano-:
Mwalimu
anapanha darasa lake lote na kufuata kitabu cha kiada kwa ukamilifu, akitoa
maelekezo ya moja kwa moja bila ya kutoa nafasi au shughuli za hiari za
wanafunzi.
v Mpangilio
maalumu wa kimya kimya darasani: Mazingira ya darasani mara nyingi huwa tulivu
na yamepangwa ambapo wanafunzi wanakaa kimya na kumsikiliza mwalimu, kelele na
mijadala isiyo na mpangilio hupunguzwa.
Mfano-:
Darasa
likiwa kimya kabisa wakati mwalimu anaandika maelezo muhimu kwenye ubao , huku wanafunzi wakinakili tu.
Ubora wa mbinu zisizoshirikishi
v Kujifunza
kwa kutazama bila ya kujaribu chochote: Mbinu hii wanafunzi wanatazama
maonyesho au video bila ya kushiriki moja kwa moja na kike mwalimu
anachokionesha na kukifundisha.
Mfano-:
Wanafunzi
wanaweza kutazama maonyesho ya majaribio ya kisayansi bila ya kufanya majaribio
wenyewe.
v Usambazaji
wa haraka wa taarifa nyingi: Mbinu zisizoshirikishi kama vile mihadhara
huruhusu mwalimu kusambaza kiasi kikubwa cha tarifa kwa wanafunzi weni kwa muda
mfupi.
Mfano-:
Katika
chuo kikuu Profesa anaweza kutoa mhadhara wa saa mbili unaofunika mada nzima ya
Hisroria ya uchumi wa Dunia akiwasilisha matukio muhimu na nadharia bila ya
kusitisha na mijadala mingi.
v Rahisi
kutekeleza na rasilimali chache: Mbinu hizi hazihitaji rasilimali nyingi za
ziada kama vile vifaa maalumu, vitabu vingi vya rejea au teknolojia ya hali ya
juu na kutekelezwa hata katika rasilimali chache.
Mfano-:
Skuli
iliyo na rasilimali chache inaweza kutumia mbinu ya walimu kutoa maelezo kwa
kutumia chaki na ubao pekee bila kuhitaji vitabu vya ziada au kompyuta nabado
kufikisha ujumbe muhimu.
v Rahisi
kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya utulivu: Baadhi ya wanafunzi hasa wenye
mahitaji maalum kama vile tawahudi, wanaweza kustawi vizuri zaidi katika
mazingira tulivu na wenye mpangilio wa moja kwa moja unaopatikana katika mbinu
zisizoshirikishi.
Mfano-;
Mwanafunzi
mwenye tawahudi anaweza kunufaika zaidi na maelezo ya moja kwa moja kutoka kwa
mwalimu bila ya usumbufu wa shughuli za kikundi kwani inamruhusu kujikita
kikamilifu kwenye maelezo.
v Kutoa
msingi wa maarifa kwa haraka kwa mada mpya au changamoto ambazo wanafunzi
hawana ufahamu wowote:Mbinu hizi zinaweza kutoa msingi wa maarifa kwa haraka
kabla ya kuanza shuguli shirikishi zenye kina zaidi.
Mfano-:
Kabla
ya kuanza mradi wa kikundi kuhusu mfumo wa juu mwalimu anaweza kutoa mhadhara
mfupi wa kueleza dhana za msingi za sayari, nyota, galaksi ili wanafunzi waw na
msingi wa kuanzia.
Udhaifu wa mbinu zisizoshirikishi
v Ukosefu
wa ushiriki na uchochezi kwa wanafunzi: Wanafunzi hukaa kimya wakisikiliza au
kuandika tu hawapati fursa ya kuuliza maswali, kujadili au kuunganisha mada na
maisha yao na kupunguza umakini wa kujifunza.
Mfano-:
Mwalimu
anatoa hutuba ndefu kuhusu historia bila ya kuwapa wanafunzi nafasi ya kujadili
au kutoa maoni, wanafunzi wengi hupoteza umakini na hawaelewi kikamilifu.
v Kutoweza
kugundua udhaifu wa kujifunza kwa haraka: Mwalimu huwa na ugumu wa kujua mapema
wapi wanafunzi wanashindwakuelewa, makosa yanaweza kujengeka nbila ya
kushughulikiwa na kuacha mapengo makubwa katika ujifunzaji.
Mfano-:
Mwalimu
anaeleza sheria za sarufi bila ya kuwapa wanafunzi mazoezi au maswali ya
haraka. Wakati wa mitihani matokeo mabaya hufichuo mapengo ambayo yangekuwa
yamegundulika mapema kwa ushiriki.
v Ukosefu
wa ustadi wa mawasiliano na ushirikiano: Mbinu hizi hazitoi fursa kwa wanafunzi
kukuza ustadi muhimu wa mawasiliano na kufanya kazi kwa pamoja.
Mfano-:Mwalimu
anafanya jaribio la sayansi mbele ya darasa na kueleza matokeo bila ya kuwapa
wanafunzi fursa ya kujadili jinsi ya kupanga jaribio au kuchambua data kwa
pamoja na husababisha kuwanyima wanafunzi ustadi wa ushirikiano.
v Kuchosha
na kupunguza hamu ya kujifunza: Ukosefu wa shughuli za vitendo, mijadala na
mwingiliano hufanya masomo yawe kavu na yasiyovutia na kupunguza hamu ya
wanafunzi kujifunza.
Mfano-:
Mwalimu
anasoma hadithi nzima ya fasihi kwa sauti bila ya kuruhusu wanafunzi kujadili
wausika au ujumbe wa hadithi, hii inaweza kufanya somo lionekane lenye kuchosha
na lisilo na ubunifu.
v Kukosa
kukuza uwezo wa kufikiri kwa makini: Mbinu hizi hazichochei wanafunzi kufikiri
kwa kina, kudadisi, au kuhoji taarifa wanazopokea.Wanakumbuka tu kile
wanachofundishwa bila ya kuchambua.
Mfano-:
Katika
somo la uraia mwalimu anasoma katiba bila ya kuwaruhusu wanafunzi kujadili
vifungu vyake au kuunganisha na changamoto za jamii, wanafunzi hawawezi kukuza
uwezo wa kuchambua sharia au sera.
Mbinu shirikishi ni
mbinu ambazo zinawahusisha wanafunzi kikamilifu katik mchakato wa kujifunza,
badala ya kuwa wapokeaji tu wa taarifa. Mbinu hizi zinaweza kujumuisha
mahojiano, makundi ya kujadili na tafiti za uwanjani.
Sifa za mbinu shirikishi
v Mwalimu
ni kituo cha kujifunza badala ya mwalimu kuwa chanzo pekee cha maarifa:
Mwanafunzi anakuwa mjenzi na mtafiti wa maarifa yake mwenyewe, akiongozwa na
mwalimu.
Mfano-:
Badala
ya mwalimu kueleza tu mzunguko wa maji wanafunzi hupewa mradi wa kuchunguza
mzunguko huo kwa kutumia vifaa rahisi na kasha kuwasilisha matokeo yao.
v Kukuza
ustadi wa mawasiliano na ushirikiano: Wanafunzi hufanya kazi kwa pamoja,
wakijadiliana na kusaidiana, hii inawajenga uwezo wa kuwasiliana kwa ufanisi,
kusikiliza na kushirikiana.
Mfano-:
Kazi
za vikundi zenye lengo la kutatua matatizo ya kisayansi au kuandaa mada ya
kuwasilisha, huwalazimisha wanafunzi kuwasiliana na kushirikiana.
v Mwalimu
kama mwezeshaji na mshauri: Jukumu la mwalimu hubadilika kutoka kuwa mtoaji wa
maarifa na kuwa mwezeshaji anayeongoza, Iushauri, na kuhamasisha wanafunzi
katika safari yao ya kujifunza.
Mfano-:
Mwalimu
anasimamia mijadala, anatoa muongozo, na anahakikisha wanafunzi wanapata
rasilimali sahihi wanapofanya mradi wa utafiti, badala ya kuwapa majibu moja
kwa moja.
v Kuongeza
morali na kujiamini: Wanafunzi wanaposhiriki na kufanikiwa kayika shughuli
sirikishi, morali yao huongezeka na kujiamini kwao katika uwezo wao wa
kujifunza na kutatua matatizo huimarika.
Mfano-:
Mwanafunzi
anapomaliza mradi mgumu wa kikundi na kuuwasilisha kwa mafanikio darasani,
anajisikia mwenye uwezo na mwenye kujiamini zaidi.
v Kutumia
uzoefu na maarifa ya awali ya mwanafunzi: Mbinu shirikishi huthamini uzoefu na
maarifa ambayo mwanafunzi tayari anayo na kuyafanya kama msingi wa kujifunza
mada mpya.
Mfano-:
Kabla
ya kuanza somo la biashara mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi watoe mifano ya
biashara ndogondogo wanazozifahamu katika maeneo yao na kasha kuunganisha na
dhana ya kifedha.
Ubora wa mbinu shirikishi
v Hujenga
uhusiano bora kati ya mwalimu na mwanafunzi: Katika mazingira shirikishi
mwalimu huwa kama mwezeshaji na mshauri bala ya mtoaji tu wa taarifa. Hii
hujenga uhusiano mzuri wa kirafiki na wenye kuaminiana kati ya mwalimu na
mwanafunzi.
Mfano-:
Mwalimu
anayechangamana na wanafunzi katika shughuli za kikundi na kutoa msaada wa
kibinafsi huwafanya wanafunzi wajiskie huru kuuliza maswali na kutafuta msaada
wanapohitaji.
v Huwaandaa
wanafunzi kwa maisha halisi na soko la
ajira: Ujuzi kama vile mawasiliano, ushirikiano, utatuzi wa matatizo na
kufikiri kwa makiniunaosisitizwa katika mbinu shirikishi nimuhimu sana katika
maisha ya kila siku na soko la ajira la kisasa.
Mfano-:
Skuli
inayotumia miradi ya kikundi na uwasilishaji wa mada mara kwa mara inawaandaa
wanafunzi kwa mazingira ya kazi ambapo wanatakiwa kufanya kazi kwa wenzao,
kuwasilisha mawazo na kutatua changamoto za pamoja.
v Huwajenga
wanafunzi kujiamini na kujitegemea: Wanapopata fursa ya kutoa maoni, kufanya
makosa na kujifunza kutokana nayo na kutatua matatizo wenyewe, wanafunzi
hujenga kujiamini katika uwezo wao na kujifunza kujitegemea.
Mfano-:
Mwanafunzi
anayewakilisha mradi wake binafsi mbele ya darasa na kupokea maswali na maoni
huongeza kujiamini kwake katika kueleza mawazo yake na kusimamia ujifunzaji
wake.
v Huongeza
uhifadhi wa maarifa: Wanafunzi wanaposhiriki kikamilifu katika kujifunza
wanashughulikia taarifa kwa njia nyingi tofauti (kusikia, kuona, kufanya na
kujadili) na hivyo kuongeza uwezekano wa kukumbuka na kuhifadhi maarifa kwa
muda mrefu.
Mfano-:
Badala
ya kukariri matukio ya kihistoria wanafunzi wanaweza kuunda ramani za dhana au
kuwasilisha matukio hayo kupitia sanaa au tamthilia, jambo linalowasaidia
kukumbuka habari kwa ufanisi zaidi.
v Kuboresha
ustadi wa mawasiliano na ushirikiano: Shughuli shirikishi kama kazi za vikundi,
mijadala na miradi ya pamoja huwapa wanafunzi fursa ya kujifunza jinsi ya
kuwasiliana kwa ufanisi, kusikiliza wengine na kufanya kazi kwa kushirikiana.
Mfano-:
Kuwaweka
wanafunzi katika vikundi kujadili na kutatua tatizo tata la hisabati
kunawafundisha kushirikiana, kueleza mawazo yao na kujifunza kutoka kwa mawazo
ya wenzao.
Udhaifu wa mbinu shirikishi
v Zinachukua
muda mrefu: Mbinu hizi huhitaji muda mwingi wa kupanga, kutekeleza na
kusimamia. Hii ni cangamoto katika mitaala ya iliyojaa au yenye muda mfupi.
Mfano-:
Kupanga
mjadala wa kikundi au mradi wa utafiti kunaweza kuchukua saa nyingi za
maandalizi na utekelezaji na hivyo kupunguza muda wa kufundisha mada nyengine
muhimu zilizo kwenye mtaala.
v Ugumu
wa kusimamia darasa kubwa: Katika madarasa yenye wanafunzi wengi kusimamia
shughuli shirikishi kunaweza kuwa changamoto kubwa na vigumu kutoa umakini wa
kutosha.
Mfano-:
Katika
darasa la wanafunzi 80 mwalimu anaweza kupata ugumu kusimamia mijadala ya vikundi
vidogo na kuhakikisha kila mwanafunzi anapata fursa ya kutoa mchango wake.
v Baadhi
ya wanafunzi kutoshiriki kikamilifu: Sio wanafunzi wote wanajisikia huru
kushiriki katika shughuli za kikundi au mijadala. Baadhi wanaweza kuwa waoga,
wanyamavu, au hawana uhakika na uwezo wao na hivyo kubaki nyuma.
Mfano-:
Katika
mjadala wa darasa mwanafunzi mmoja mwenye aibu anaweza kutochangia chochote
hata kama ana mawazo mazuri akihofia kuchekwa au kukosea.
v Mahitaji
makubwa kwa mwalimu: Mwalimu anahitaji kuwa na ujuzi wa ziada katika
kupanga, kuwezesha, na kutathmini mbinu
shirikishi.
Mfano-:
Mwalimu
ambae hajafunzwakutosha katika kusimamia miradi ya vikundi anaweza kujikuta
akihangaika kutatua migogoro kati ya wanafunzi au kuhakikisha kazi inafanyika
kwa urahisi.
v Huweza
kulea mazingira ya kelele na fujo: Hujumuisha muingiliano mwingi na harakati
darasani, jambo ambalo linaweza kusababisha harakati na fujo endapo
halitasimamiwa vizuri na kuathiri mkusanyiko.
Mfano-:
Wakati
wa mijadala ya vikundi, darasa linaweza kuwa na kelele nyingi kiasi cha
kuvuruga madarasa mengine jirani au kupunguza uwezo wa wanafunzi kujikita
kwenye mada.
Katika kuchagua kati ya mbinu
zisizoshirikishii na shirikishi watafiti wanapaswa kuzingatia malengo ya
utafiti wao, aina ya data wanayohitaji,na rasilimali zilizopo. Kila mbinu ina
faida na changamoto zake hivyo ni muhimu kufahamu sifa hizi ili kufanya maamuzi
bora katika mchakato wa utafiti, mara nyingi matumizi ya mbinu mchanganyiko
yanawza kutoa matokeoo mazuri na yaliyo bora zaidi kwasababu huleta pamoja
faida za mbinu zote mbili.
MAREJELEO
Magare, Y, D.(2011)Matumizi ya
majadiliano ya vikundi katika kufunza stadi ya kuzungumza katika shule za upili
katika tarafa za Masocho, Kaunti ya kisii, Kenya. Nairobi:Kenyatta University.
Ndege,J.,Kea,P.,Osoro,E.,Waititu,F.,Mucheria,Z.naWafula,W.(2020).Kiswahili
Dadisi:Mwongozo wa Mwalimu Gredi ya 4.Nairobi:Oxford University Press.
Wasike,M.W.(2015).Tathmini ya
marumizi ya nyimbo za kizazi kipya kama mbinu za kufundishia masuala ibuka
katika Kiswahili kwenye shule za upili nchini Kenya.Kibabii
University.Bungoma:Kibabii University.
0 maoni:
Post a Comment