17 Jun 2025

 imeandaliwa na Mtila Mswahili. 



UTANGULIZI

Kwa mujibu wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA), (2009)

Lahaja ni tafauti ya matamshi ya wasemaji wa lugha moja walio katika mazingira tafauti ya ardhi ya lugha ile.

Kwa ujumla -:

Lahaja ni vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainishwa na jamii au jiografia. Lahaja za lugha moja zinakaribiana katika matamshi, miundo ya sarufi na msamiati. Kama lugha hutofautiana katika matamshi tu tofauti hizo huitwa lafudhi sio lahaja. Ni kweli ya kwamba Kiswahili kinaathiri lahaja za Zanzibar kupitia hoja zifuatazo-:

Kiswahili  sanifu kinaathiri lahaja za Zanzibar kupitia msamiati: Kupitishwa kwa maneno mapya lahaja za Zanzibar zimeendelea kupokea maneno mengi kutoka kwa Kiswahili sanifu hasa yanayohusu dhana mpya, teknolojia, elimu na masuala ya kitaifa. Mfano badala ya kutumia neno la kienyeji kwa kompyuta moja kwa moja watu wengi sasa hutumia kompyuta moja kwa moja kutoka kiswahili sanifu vilevile maneno kama vile televisheni, simu, serikali, rais na bunge yamepenya sana katika matumizi ya kila siku na kusababisha athari katika lahaja za Zanzibar.

Kuwepo kwa utofauti wa matamshi: Kubadilika kwa matamshi ya baadhi ya maneno ingawa matamshi ndio sehemu inyobaki kuwa tofauti kwa kiasi kikubwa kati ya lahaja na Kiswahili sanifu kunaweza kua na mabadiliko kadri watu wanavyozidi kusikia na kutumia Kiswahili sanifu. Mfano sauti fulani ambazo hazipo katika Kiswahili sanifu zinaweza kuanza kutamkwa kwa namna inayokaribia zaidi matamshi ya Kiswahili sanifu hasa katika mazingira rasmi au wanapozungumza na watu kutoka sehemu nyengine.

Miundo ya sarufi ya Kiswahili: Kurahisishwa kwa miundo ya sarufi Kiswahili sanifu kina miundo ya kisarufi iliyorahisishwa kwa kiasi Fulani ikilinganishwa na baadhi ya lahaja.Watumiaji wa lahaja wanaweza kuathiriwa na urahisi huu na kuanza kutumia miundo hiyo katika mazungumzo yao. Mfano matumizi ya viambishi vya ngeli yanaweza kua tofauti kidogo kati ya Kiswahili sanifu na baadhi ya lahaja. Kunaweza kuonekana mwelekeo wa kufuata zaizdi kanuni za Kiswahili sanifu katika matumizi ya ngeli au uundaji wa sentensi.

Suala la istilahi na misemo maalumu: Elimu na utawala katika mazingira ya elimu na utawala, Kiswahili sanifu ndio lugha kuu inayotumika. Hii inasababisha kuenea kwa istilahi za kielimu na misemo katika matumizi ya kila siku ya wazungumzaji wa lahaja mbalimbali. Mfano maneno kama mwalimu mkuu, wizara bunge, mahakama yameingia katika msamiati wa kawaida na kusababishaathari katika lahaja za Zanzibar.

Uwepo wa vyombo vya habari: Ushawishi wa vyombo vya habari kama vile redio, televisheni na magazeti kwa kiasi kikubwa hutumia Kiswahili sanifu. Hii inawafanya wazungumzaj iwa lahaja kuwa wazi kwa kiasi sanifu na kuiga baadhi ya maneno, misemo, na hata miundo ya sentensi na kusababisha athari katika lahaja za Zanzibar.

Kukopa maneno ya kiteknolojia: Maendeleo ya teknolojia yamefanya maneno mengi kutoka katika lahaja za Zanzibar na kuingia katika Kiswahili sanifu na kuathiri lahaja za Zanzibar. Mfano simu, runinga, kompyuta, intanet, ukurasa wa mtandao yanatumika sana na kuathiri lahaja za Zanzibar.

Ni dhahiri kuwa Kiswahili sanifu kina ushawishi mkubwa katika lahaja za Zanzibar zina athari na inaonekana wazi katika msamiati, sarufi, matamshi kwa kiasi Fulani na hasa katika matumizi ya msimbo mchanganyiko. Ingawa lahaja zinaendelea kuwa sehemu muhimu ya utambulisho wa jamii za Zanzibar mwingiliano na Kiswahili sanifu unaendelea kuzibadilisha na kuzifanya zifanane zaidi na lugha za kitaifa na kusababisha athari katika lahaja za Zanzibar.

 


MAREJELEO

Khatib M S.(1983),Historia na maendeleo ya Kiswahili Zanzibar:Lugha ya kiswahili.Makala za semina ya kimataifa ya waandishi wa Kiswahili I.TUKI.uk19-49.

Horton,M.(1996),Shanga.London.

Temu,C.(1980),Lahaja za Kiswahili.TUKI(mimeo)

Mlacha,S.na A,Hurskainen(Wah)(1995),lugha,lahaja na fasihi ya simulizi ya kiswahili.TUKI.


0 maoni:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Wasiliana nami papo kwa papo

Name

Email *

Message *

Ads 468x60px

Breaking News

Top Featured

Featured Posts

Sample text

Sample Text

Recomended

Facebook

Advertise

Most Popular

Connect With Us

Followers

Social Icons

Pages

Pages

BTricks

Pages

Popular posts

Tafuta chochote ukiwa hapahapa

Kategori

Recent Comments

You can replace this text by going to "Layout" and then "Page Elements" section. Edit " About "

recent posts

Video Of Day

TRANSLATE

Instructions

Video

Flickr Images

FURAHIA UWEPO WAKO HAPA

Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

Imetembelewa mara

NUMBER OF VIEWERS

Popular Posts

SAJIRI

Definition List

premium-wordpress-themes.org