Imeandaliwa na Mtila Mswahili.
UTANGULIZI
Utafiti kisayansi ni mchakato wa kuchunguza, kugundua, na kuelewa mambo
mbalimbali ya asili kwa kutumia mbinu za kisayansi. Huu ni mchakato wa mfumo
ambao unajumuisha hatua kadhaa.kama ifuatavyo:-
Hatua za utafiti kisayansi.
Kubainisha tatizo au swali la utafiti.Katika hatua hii ya mwanzo Mtafiti
huanza na swali au tatizo ambalo linahitaji ufafanuzi zaidi.Mbinu hii ya
kisayansi huhitaji utulivu zaidi ili isitokezee tatizo kutojulikana.
Kufanya mapitio.Mapitio hayo
huhusisha kubaini kinachofanyiwa utafiti ni cha kweli na kina uhakika,mapitio
hayo hupitia njia mbalimbali ikiwemo kupitia zaidi ya mara moja na kupitiwa /
kuangaliwa na mtu mwengine.
Kubainisha malengo ya utafiti.Malengo ya utafiti ni lazima yabainishwa kuwa ni malengo makuu na
malengo mahususi na baada ya kugawanywa namna hiyo yapendekezwe mahali husika.
Kufanya usanifu wa utafiti.Usanifu wa utafiti ni hali ya kuteua swali
kutumika na kufanyiwa marekebisho ili itumike rasmi, katika hatua hii tafiti
iliyopitia usanifu huwa bora zaidi kwa vile imepitia usanifu wake.
Kukusanya taarifa/data.Taarifa mbalimbali hutafutwa na kukusanywa kwa
kupitia utafutaji, Uchunguzi,uulizaji wa maswali,kufika eneo husika na vyanzo
vyengine na baadae taarifa hizo huwekwa pamoja.
Uwasilishaji wa taarifa na uchambuzi.Taarifa hizo baada ya kukusanywa
huwasilishwa na kufanyiwa uchambuzi ili kubaini kama zina ukweli na uhakika
ndani yake ,endapo ikifika kwa jamii wasipate uduwanzi kwa taarifa
zilizopatikana kwenye huo utafiti.
Uandishi wa ripoti.Baada ya kutoka hatua zote hizo ripoti huandikwa
ambayo ni nadhifu na yenye ukweli mtupu,ripoti hiyo hutumiwa na watu mbalimbali
ambao hutaka kujiridhisha na wengine kwa lengo la kujifunzia.
Kanuni na Misingi ya utafiti kisayansi.
Kanuni na misingi ya utafiti
kisayansi ni muhimu ili kuelewa jinsi ya kufanya utafiti kwa ufanisi.
Zifuatazo ni kanuni na misingi ya
utafiti kisayansi ni hivi ifuatavyo:-
Kuwepo na ushahidi wa Kitaalamu.Utafiti unapaswa kuwa na msingi wa kutumia ushahidi wa kitaalamu(scientific
evidence). Hii inamaanisha kutumia vyanzo vilivyothibitishwa na wataalamu wa
fani husika na kuaminika kwa data zinazopatokana.
Kutumia mbinu bora za
Utafiti.inashauriwa kuwa ni muhimu
kuchagua mbinu sahihi za utafiti, kama vile utafiti wa majaribio, utafiti
wa ulinganifu, au utafiti wa kiwango hizi ndio husababisha kutoa utafiti mzuri.
Kupatikane uwazi na uaminifu.Utafiti unapaswa kuwa wazi, na matokeo yake
yanapaswa kuwa yaaminifu. Hii hujumuisha
kutoa taarifa zote muhimu na kutangaza njia zilizotumika katika tafiti
hiyo.
Kuandaa ukurasa wa maswali.
Kuunda na kuandaa maswali sahihi
na yaliyowazi ni muhimu katika kukusanya taarifa, maswali yanapaswa kuwa ya
moja kwa moja na kueleweka kabisa bila ya utata wowote.
Kuchambua taarifa. Baada ya kukusanya data/taarifa inapaswa kuchambuliwa
kwa njia sahihi na inayokubalika mbinu za takwimu zinaweza kutumika ili kupata
matokeo ya maana na sahihi.
Kutoa hitimisho na mapendekezo ya utafiti. Matokeo yanapaswa
kutoa hitimisho lililo wazi na mapendekezo yanayoweza kutekelezeka,hii
inamaanisha kuwa matokeo sahihi hutoa hitimisho na mapendekezo yaliyowazi
kabisa.
Maadili ya Utafiti. Utafiti unapaswa
kufanywa kwa kuzingatia maadili, ikiwa ni pamoja na kuheshimu haki za
washiriki, kuepusha udanganyifu,kutoa taarifa zilizochambuliwa vizuri na
kadhalika.
Kutumia rejea na uteuzi wa Vyanzo.Ni vizuri kutoa rejea sahihi kwa
vyanzo vyote vilivyotumika katika utafiti, ili kuimarisha uhalali na
uthibitisho wa kazi yako.
Kwa kutumia kanuni na misingi hii ya utafiti kisayansi hufanya kazi
kuwa nzuri na yenye kufahamika .
Maana ya lugha.
Nkwera,lugha ni utaratibu maalum wa sauti nasibu zenye maana ambazo
hutumiwa miongoni mwa wanaadamu kwa mawasiliano.
TUKI (2004).lugha ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana
ambao hutumiwa na watu wa Taifa fulani au kikundi fulani kwa ajili ya mawasiliano.
Masamba (2004).lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo zimetumiwa na
jamii Kwa madhumuni ya mawasiliano katika jamii.
Kwa ujumla,lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na
wanajamii kwa ajili ya kuwasiliana.
Uhusiano wa Lugha na utafiti.
Lugha ni njia muhimu katika
utafiti wa kisayansi, kwani huruhusu mawasiliano, uelewa, na ushirikiano baina ya watafiti.
Uhusiano huu ni wa kimsingi katika mchakato wa kisayansi, na unajitokeza
katika nyanja tafauti ufuatao ni uhusiano wa lugha na utafiti kisayansi ni hivi
ifuatavyo:-
Mawasiliano
katika Sayansi.Utafiti kisayansi hutumia
lugha kuwa ni nyezo kuu ya mawasiliano yake,Katika muktadha wa kimataifa, lugha
yaKiingereza imekuwa lugha kuu ya mawasiliano na kuwasiliana katika sayansi, ndio hivyo watafiti wengi
hutumia lugha ya Kiingereza ili kufikia hadhira kubwa na pana. Hali hii inaweza kuwa changamoto kwa watafiti
kutoka maeneo yasiyokuwa na ufanisi mkubwa katika lugha ya Kiengereza na hivyo
kuathiri ushiriki katika maswala ya kisayansi.
Uundaji wa Nadharia na Ufafanuzi wa tafiti.Lugha
huwezesha watafiti kuunda na kuelezea nadharia, dhana, na mifano ambayo inayosaidia katika utafiti kisayansi kwa
matukio na maswala yaliyopo. Kwa
kutumia lugha, watafiti wanaweza kuwasilisha mawazo yao kwa uwazi na usahihi,
na hivyo kuchangia katika maendeleo ya maarifa mapya.
Uainishaji wa kisayansi.Katika utafiti kisayansi , lugha hutumika
kuainisha na vitu mbalimbali,kama vile viumbe hai, kemikali, na dhana nyingine
zilizopitia usayansi , Hiiinahusisha matumizi ya istilahi maalum na mifumo ya
uainishaji kisayansi ambayo huwezesha watafiti kuelewa na kushirikiana katika vipengele maalum na vyenginevyo vya utafiti.
Uimarishaji wa uhusiano
na ushirikiano kutoka maeneo tafauti ya dunia.Lugha inarahisisha ushirikiano
kati ya watafiti kutoka tamaduni na maeneo tafauti ,Hata hivyo, kutegemea lugha
moja kama Kiingereza kunaweza kuleta changamoto kwa watafiti kutoka maeneo
yasiyo na ufanisi mkubwa katika lugha hiyo, na hivyo kuathiri ushiriki wao
katika jamii ya kisayansi.
Hali ya upatikanaji wa maarifa.Hali
hii huchochea uhusiano wa lugha na utafiti ,Lugha inaathiri upatikanaji wa maarifa
matokeo ya utafiti yanayochapishwa katika lugha moja yanaweza kuwa vigumu
kupatikana kwa wale wasio na ufanisi katika lugha iliyotumika na hivyo kuzuia
upatikanaji wa maarifa muhimu. Hii ni
muhimu hasa katika muktadha wa Afrika, ambapo lugha za kienyeji zinaweza
kutumika zaidi katika utafiti na mawasiliano.
Maana ya fasihi.
Sengo na kiango (1973).Fasihi ni mwamvuli wa mtu ,jamii na watu.
Nkwera .Fasihi ni kioo cha maisha.
Taasisi ya elimu (2014). Fasihi ni sanaa itumiayo lugha kuibua
hisia.
Hivyo Inapuzungumzwa Fasihi ni sanaa itumiayo lugha ili kufikisha
ujumbe kwa jamii fulani.ujumbe huo huasa jamii au kuelekeza jambo fulani kwa
jamii lengwa .
Uhusiano wa Fasihi na utafiti.
Fasihi na utafiti ni nyanja mbili zinazohusiana kwa karibu, ambapo
fasihi hutumika kama nyenzo muhimu katika mchakato wa utafiti, na utafiti
unachangia katika kuelewa na kuchambua kazi za kifasihi.
Fasihi
kama chanzo na kichocheo cha Utafiti.Fasihi zote mbili ,fasihi simulizi na
fasihi andishi, hutumika kama chanzo cha utafiti katika maeneo tafauti tafauti,Kwa
mfano, kazi za kifasihi kutumika kuchambua historia, tamaduni (mila na desturi)
na itikadi za jamii husika. Hii inaonyesha jinsi fasihi inavyoweza kuwa
nyenzo muhimu katika kuelewa muktadha wa kijamii na kihistoria.
Mbinu
ya uchambuzi wa kazi za fasihi katika Fasihi .Katika utafiti wa kifasihi
wataalamu hutumia mbinu kadhaa wa kadhaa za utafiti ikiwa ni pamoja na
uchambuzi wa maandishi (lugha ya kifasihi), tafsiri, Uchunguzi na uchambuzi wa muktadha
na wahihistoria ya kijamii, mbinu hizo husaidia
katika kuelewa undani wa kazi za kifasihi na jinsi zinavyohusiana na jamii na
kuzipokea kazi hizo.
Fasihi
kama zana ya Utafiti.Fasihi hutumika pia kuwa zana ya utafiti katika vitengo vya kijamii na kisayansi. Kwa mfano, fasihi
inaweza kutumika kuchunguza mitindo ya kijamii, mabadiliko ya kimaadili, na
athari za kisiasa na kiuchumi katika jamii. Hii husaidia kuonyesha mabadiliko
na huonyesha uwezo wa kuzikabili changamoto zinazojitokeza katika jamii.
Kuhifadhi Utamaduni wa jamii .Fasihi inasaidia kuhifadhi na kuwasilisha
tamaduni na historia za jamii mbalimbali. Utafiti unachangia katika kuelewa na
kuchambua kazi hizi za kifasihi, hivyo kuleta maono na mwanga mpya Kwa jamii.
Maendeleo ya nadharia mbalimbali .Utafiti katika fasihi unasaidia
kuendeleza nadharia mbalimbali za fasihi, kama vile nadharia ya ufeministi,
nadharia ya mfumo dume na nadharia ya semiotiki nadharia hizi husaidia watafiti
na waandishi kuelewa na kuchambua kazi za fasihi kwa kina zaidi na kutunza kwa
muda mrefu.
Kuibua
maswali mapya.Fasihi inaweza kuibua maswali mapya ambayo yanahitaji utafiti
zaidi. Hii inachangia katika ukuzaji wa maarifa mapya na ufahamu wa kibinadamu. Kwa ujumla uhusiano kati ya fasihi na
utafiti ni wa karibu na wenye umuhimu mkubwa katika maendeleo ya maarifa na
utamaduni. Hivyo fasihi na utafiti ni vyenye kujenga ustawi mkubwa kwa jamii.
Kwa ujumla dhana ya utafiti kisayansi ,
lugha,fasihi ni vitu vyenye umuhimu kwa binaadamu na jamii yake
kiujumla.husaidia kujenga ustawi Katika hatua mbalimbali za maisha na utafiti .
MAREJELEO.
Wizara ya Elimu na Utamaduni,(2003).Ufundishaji unaozingatia Ujenzi
wa Maana,Chuo cha Ualimu Morogoro:
Ecoprint Ltd.
TUKI, (2004). Kamusi ya Kiswahili sanifu (toleo la pili),Nairobi:
Oxford University Press.
TET, (2014). Kiswahili,kidato cha nne,Tanzania: Oxford University
limited.
Kumar,R.(2021). Research methodology,(4ed).London:SAGE Publications
India Pvt ltd.
https://www.msomibora.com/2018/06/Kiswahili
-form-one-topic-4-fasihi.html?m=1.
https://learn.farmhub.ag.
https://sw.wikipedia.org.
0 maoni:
Post a Comment